Harufu hii inatoka wapi; ni miguu, soksi au viatu? Tiba yake nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Harufu hii inatoka wapi; ni miguu, soksi au viatu? Tiba yake nini?

Discussion in 'JF Doctor' started by Faru Kabula, Jul 31, 2009.

 1. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,876
  Trophy Points: 280
  Kwa baadhi ya watu, imekuwa kawaida kulazimika kuvua viatu unapoingia katika baadhi ya nyumba au majengo fulani. Unaweza ukakuta nyumba au ofisi ina carpet/zulia ambapo wenyeji wamejiwekea utaratibu wa kuvua viatu kwanza kabla hujaingia. Lakini imekuwa ni kero iwapo atatokea mtu akavua viatu na kuingia ndani akiwa na soksi, pale ambapo harufu mbaya/nzito inapofumuka na kuharibu hewa ya humo ndani. Sasa mimi nina swali hapa, hivi hii harufu inasababishwa na nini hasa, ni miguu, soksi au viatu? Je, nini hasa kifanyike kwa mwenye tatizo hilo ili awe huru kuingia popote bila kusimangwa?
   
 2. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mimi nafahamu tiba tu nayo ni
  a-opt kuvaa sendozi (makobazi) (yeboyebo)
  kufua soksi
  kubadlisha soksi daily kwa wale wavivu at least after days
  kunawa miguu kabla ya kulala kama una tatizo hilo

  NB
  Ukiona haya yote huyawezi acha kwenda kwa watu ambao unajua kwao kuna carpets
   
 3. tzengo

  tzengo Member

  #3
  Jul 31, 2009
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ni kawaida kwa miguu(feet) ya binadamu kuwa na sweat glands nyingi na hivyo hutokwa na jasho jingi sana kuliko sehemu nyingine nyingi za mwili.Kimsingi jasho ni mchanganyiko wa chumvi na maji.Pia ni kawaida kwa bacteria kuwepo juu ya ngozi ya binadamu,kwa hiyo bacteria hawa hula jasho la binadamu na kutoa wastes zenye harufu kali.kutokana na kuwepo kwa viatu na soksi hivyo jasho haliwezi kuescape hewani hivyo kusababisha unyevuunyevu miguuni.viatu na soksi huleta giza,giza na unyevu unaokuwepo miguuni ni mazingira mazuri sana kwa bacteria hawa kuishi,kula na kuzaliana.

  CHA KUFANYA:
  1.kupunguza kiwango cha bacteria kwenye miguu
  2.kupunguza mkusanyiko wa jasho miguuni

  kupunguza kiwango cha bacteria miguuni kwa kuvaa soksi safi kila mara,kubadili viatu mara kwa mara,kuosha miguu vizuri kwa anti-bacterial soaps.

  Kupunguza mrundikano wa jasho miguuni kwa kuvaa viatu vya wazi,kubadili soksi mara kwa mara ikiwezekana zaidi ya mara moja kwa siku,kuvaa soksi zenye kufyonza jasho zaidi ili kupunguza kiasi cha jasho linaloweza kuliwa na bacteria juu ya ngozi,kutumia antiperspirant miguuni(kwenye feet)

  NB

  Pia kufuata ushauri wa mkuu SIPO kwamba ukiona yote huyawezi acha kwenda kwa watu ambao unajua kwao kuna carpets.kwi kwi kwi...
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Simpo! kila anapotoka kukoga akaushe miguu vizuri halafu aisugulie ndimu, aiache ikauke yenyewe ndio aanze. Na kama hana kawaida ya kukoga kutwa mara tatu, basi ahakikishe anapoamka anaosha miguu, anakandamiza ndimu, kila kipande mguu mmoja, mchana, jioni na kabla ya kulala hivyo hivyo. Within few days, hali itarudi kuwa ya kawaida.

  Na hii inafaa pia kwa wale wenye harufu ya kwapa na ya mdomo. Kwapa, ni kama hapo juu lakini unapaka kwapani na mdomo ni kama hapo juu lakini unasukutuwa, ndimu asilia si ya unga.
   
Loading...