Kichankuli
JF-Expert Member
- Dec 18, 2008
- 887
- 190
Kuna watu ambao wamekuwa na udhaifu wa kuchanganya matamshi ya herufi kadhaa. Kwa Wamakonde M wao huitamka kama N (mathalan, mtu wao husema ntu) kuna wengine kwenye R wao huweka L na kinyume chake (kuna mwalimu wetu wa shule ya msingi alituchapa kutokana naudhaifu wake wa kuchanganya R na L. Aliandika ubaoni neno MAPERA; sasa akawa analisoma ili nasisi tumfuatilizie, yeye akitamka alikuwa anasema MAPELA na sisi tukawa tunamfuatishia hivyo hivyo. Tulipokuwa tunatamka MAPELA akawa anatwambia tume kosea na kutusahihisha kwa kusema SIYO MAPELA ni MAPELA. Hatimaye tukaishia kuchapwa viboko) Utawasikia wengi wa Wakurya wanakwambi HARO badala ya HALO.
Hivi huu udhaifu chanzo chake ni nini? Je, hauwezi kurekebishika?
Hivi huu udhaifu chanzo chake ni nini? Je, hauwezi kurekebishika?