Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Naomba kuweka wazi kabisa kwamba mimi si mpenzi wa Muziki wa Tanzania na wala siwapendi wanamuziki wa Tanzania , hii ni kwa vile wamekuwa mara zote wakitumika na ccm kuwapotosha wananchi , na hasa hawa wanaoitwa Wanamuziki wa kizazi kipya , ambao pia wanatuhumiwa kusafirisha na kusambaza madawa ya kulevya hivyo kuharibu nguvu kazi ya Taifa.

Bali nimesononeshwa sana na yaliyojitokeza kwenye mgogoro wa Harmonize na Diamond , pale huyo Harmonize alipokuwa anaomba kujitoa kwenye lebo ya WASAFI , mengi sana ameongea mwenyewe kila mtu kayasikia wala sina haja ya kuyarudia , bali nitagusia kidogo maeneo mawili tu.

Kwamba Diamond alimwambia Harmonize kwamba anaweza asimkamilishie kile anachotaka na wala hatomfanya chochote na kokote atakakoenda hatofanikiwa , kwa vile HAMUWEZI KISERIKALI , KIFEDHA NA KIUCHAWI , hii ni kauli ya kijinga sana kutolewa na anayeitwa msanii mkubwa , ni kauli ya kishamba sana iliyojaa Utanzania mtupu!

Jambo lingine linalotia aibu ni kitendo cha Harmonize Kuomba msaada kwa Magufuli moja kwa moja baada ya ngazi za chini ikiwemo wizara kumgwaya Diamond , Yaani Rais wa nchi ampigie simu Msela Diamond na kumbembeleza ili akubali kuterminate mkataba wa Harmonize na Wasafi ! hili ni jambo la kutia aibu sana , Yaani inawezekanaje Wizara na BASATA kutiwa mfukoni na msanii mmoja?

Haya mambo yakiachwa iko siku yatakuja kufedhesha mamlaka ya Rais , na sisi kama wananchi hatutakubali.
yaani serikali ipoteze muda kuingilia ugomvi ya vimburukutu vilivyolewa umaarufu vinavyopiga picha za ngono na kutambishana wanawake? hao ni watu wa umuhimu gani kwa nchi hata kusumbua serikali kuwafikiria?
 
serikali iache kudili na masuala ya maana ianze kuhangaika na wasanii we jamaa kumbe wakat mwengine una tumia Masabuli kufikiria

ushawahi sikia serikali ya Us kuingilia ugomvi wa eastcoast na west coast?
Serikali ina Taasisi zake kama BASATA zimeundwa kwa ajili ya wasanii ndo maana unaona wengine wanafungiwa nyimbo,kwahiyo wewe ndo unaonyesha ukilaza
 
yaani serikali ipoteze muda kuingilia ugomvi ya vimburukutu vilivyolewa umaarufu vinavyopiga picha za ngono na kutambishana wanawake? hao ni watu wa umuhimu gani kwa nchi hata kusumbua serikali kuwafikiria?
Sasa Mbona Rais wa hiyo serikali aliingilia ?
 
Pole mmakonde tunajua washindani wako mond na rayvanny walikuwa huko pia,show zako US zilidorora kuliko za wenzako.Pambana na wewe uitwe kutumbuiza MTV AWARD ili uwe kama alivyofanya Vanny kule Hungary fitina hazikusaidii huko sio TZ.
 
Kiukweli nimesikitishwa sana maneno kama hayo kutolewa na msanii ambaye ni public figure, na kwa mujibu wa harmonize anadai kua hayo maneno yali rekodiwa na mpaka saizi anayo
Kunatime mtu anakukela mpaka unatoa maneno ambayo hayakustahili, jua sio bure mtu aanze tu kukuambia hayo yote, yaweza kuwa harmo kunakauli aliitoa mpaka akajibiwa hvyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom