Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumloga Diamond Platnumz

jahanbaksh

Member
Sep 4, 2018
16
45
Miaka miwili iliyopita, Harmonize aliachana na lebo ya WCB, akasema menejimenti ya WCB ilimtaka staa huyo wa umakondeni alipe Sh500 milioni aweze kung’oka.

Ametumbua jipu, kwamba ilibidi auze nyumba zake tatu apate pesa za kuwalipa WCB. Kwamba yalikuwa masharti ya mkataba, Harmonize akitaka kuondoka WCB, alipe Sh500 milioni na gharama za utengenezaji wa nyimbo zote.

Hivi karibuni Harmonize amesema alihaha kupata fedha za kulipa WCB. Kampuni ya vinywaji ya Sayona na Benki ya CRDB ndio walimpa fedha za kukamilisha Sh500 milioni. Hata hivyo, akatakiwa aongeze Sh100 milioni, alizopewa na meneja wake, Sebastian Ndege.

Mchanganuo wa 2021

Harmonize aliuza nyumba yake ambayo haikuwa imekamilika kwa Sh100 milioni. Sayona wakampa Sh200 milioni, halafu CRDB wakampa Sh200 milioni. Seba akaweka Sh100 milioni. Jumla Sh600 milioni.

Lipi sahihi? Nyumba tatu alizouza mwaka 2019 au fedha za CRDB, Sayona na Seba? Mpaka hapo utaona kwamba kuna mahali Harmonize hasemi ukweli.

Sisahau taarifa ya mwaka huu, Harmonize alisema angeongea kila kitu. Kama mwaka huu ndio alisema ukweli, basi 2019 aliongopa.

Hata hivyo, lipo ambalo halibishaniwi. Ni Harmonize kulipa Sh500 milioni. WCB hawajawahi kukanusha. Kiulizo kipo kwenye Sh100 milioni.

Mwaka 2019, Harmonize alisema alilipa WCB Sh500 milioni. Mwaka huu, amesema alizolipa ni Sh600 milioni. Kwa nini mwaka 2019 alipunguza?

Stori ya Harmonize na Bosi kubwa wa WCB, Diamond Platnumz ina matege mno. Utaona inazingirwa na wivu, uongo, tamaa na kufanya kazi kiswahili.

Kwa nini waligombana? Jibu ni vipengele vya mkataba (contractual terms). Kuna mkataba (makubaliano) yenye utashi wa pande zote zenye kusaini na ulaghai au shuruti. Wanasheria huliweka vizuri kwa lugha yao. Huita duress contracts, yaani mikataba isiyo na utashi au ufahamu.

Tafsiri ya duress ni nguvu, lazima au ushawishi wa kumfanya mtu atende jambo bila ridhaa yake. Mathalani, mtu anasaini mkataba akiwa ameshikiwa bunduki, anaambiwa asiposaini atauawa.

Anatekwa mwanaye, mkewe au mumewe, mzazi wake au ndugu yake, halafu anaambiwa asaini mkataba, vinginevyo mateka atauawa. Mikataba ya aina hiyo ni duress.

Kusaini mkataba na mtoto au mtu asiye na ufahamu wa kutosha kuhusu vipengele vya mkataba, hutafsiriwa kuwa aina nyingine ya duress.

Mwaka 2015

Harmonize ni kijana mdogo. Masikini sana. Ndoto yake ni kuwa mwanamuziki. Anaishi mjini Dar es Salaam na Diamond Platnumz ni staa aliyekaa juu ya nchi.

Huwezi kupata picha ya duress katika mikataba ya wasanii kama hutavaa viatu vya msanii underground anayetamani kutoka kimuziki. Ukimuuliza Afande Sele alivyomwona Sugu enzi hizo akitaka asaidiwe kimuziki, akiwa mkweli, utaelewa maana yake.

Jicho la msanii underground kwa msanii aliyefanikiwa ni kama malaika wa pepo. Kwa mantiki hiyo, mwaka 2015, Harmonize ambaye hakuwa akijua chochote, alimwona Diamond ni malaika wa pepo yake.

Jiulize, siku ya kiyama unaona jehanamu ilivyo halafu unaitwa na malaika wa pepo, anakwambia saini mkataba uingie, utapoteza muda? Tusiongopeane, utasaini haraka haraka na kuingia.

Ukishaingia peponi na kuijua pepo ilivyo, ndipo unaweza kumwona malaika wako wa pepo alikupiga, kwamba ulistahili zaidi.

Kumbuka pia kuwa wakati unasaini mkataba wa kuingia peponi, utakuwa na furaha iliyopitiliza, umakini hautakuwepo. Utataka usaini ili ukajionee yaliyomo. Ufaidi simulizi za mito ya maziwa na asali.

Njoo kwa Harmonize. Hajui pepo ya muziki ilivyo ila alifahamu kuwa Diamond yupo peponi na ni malaika wa pepo. Akatokeza kumvuta peponi, unadhani Harmonize angedengua?

Harmonize alipoambiwa na Diamond asaini mkataba aingie kwenye pepo ya muziki, angelaza damu? Bila shaka, alisaini akiwa na furaha iliyopitiliza.

Mwaka 2015 akatoa Aiyola, jamii ikamjua. Mwaka 2016 Bado ilifuata kisha Matatizo. Mpaka hapo Harmonize alikuwa ameshaijua pepo ya muziki. Hakuwa mshamba tena. Kipindi hicho angeambiwa asaini upya mkataba wake na WCB, Kuna vipengele angevikataa. Kumbe sasa, kiuhalisia, mkataba wa Harmonize na WCB, kwenye fikra za Harmonize, ulivunjika tangu mwaka 2016.

Tafsiri nzuri ya mkataba wa duress ni ule ambao anayesaini, muda mrefu unaofuata akiambiwa asaini upya, lazima akatae. Ni kama Harmonize, akili yake ya sasa inamwambia alikosea kusaini.

Dhambi ya mkataba

Mkataba ni makubaliano ya kisheria. Na asili ya mikataba ya muziki ni wajibu wa kila upande. Unachotoa na unachoingiza. Masharti lazima yawe sawa kuhusu mzigo ambao kila upande utabeba kwa kuvunja mkataba.

Mathalani, iliandikwa kuwa Harmonize alitakiwa kulipa Sh500 milioni na kurejesha gharama zote za nyimbo ambazo zilirekodiwa chini ya Wasafi ili kuvunja mkataba.

Sawa! Je, wajibu wa Wasafi kuvunja mkataba ni upi? Kama wao wangeamua kuachana na Harmonize, wangepaswa kumlipa nini? Mkataba wa masharti ya upande mmoja, ni aina nyingine ya duress.

Harmonize kasaidiwa?

Kampuni ya kusimamia muziki huwekeza katika maeneo ya aina mbili; label (utengenezaji na usimamizi wa muziki) na imprint (masoko ya muziki na mwanamuziki).

Kampuni kama Wasafi inapomchukua msanii, inabeba maudhui ya kutengeza na kusimamia muziki pamoja na masoko. Hufanya hivyo kupata faida. Sio msaada!

Wasanii wengi chipukizi wanapochukuliwa na mastaa wakubwa, hudhani wanasaidiwa, hivyo hunyenyekea na kusaini kiholela. Wafahamu kuwa hakuna recording company ya usamaria wema. Husaka fedha.

Kampuni inapofikia hatua ya kukusaini, maana yake huona faida ndani yako, kwa hiyo hupaswi kwenda kikondoo, kudhani unasaidiwa. Ni biashara. Soma vingele bila ushawishi, amua kwa maisha yako. Tena, shirikisha wanasheria.

Kingine, recording company nyingi hutaka kummiliki msanii muda mrefu, ipo hivyo. Mikataba ya muziki huwa haiendi kwa umri, bali kazi.

Wasiseme unasainiwa kwa miaka 20, kama WCB na Harmonize, bali, mnatengeneza albamu ngapi au nyimbo ngapi. Siku hizi soko la kidigitali, zinaangaliwa nyimbo zaidi kuliko albamu.

Suge Knight alipomtoa Tupac jela mwaka 1995 na kumlipia dhamana ya dola milioni moia, Tupac hakusaini umri wa kukaa Death Row Records miaka mingapi, bali walisaini albamu tatu.

Februari 2014, 50 Cent, alipokuwa anasaini mkataba na kampuni ya usambazaji ya Caroline, inayomilikiwa na taasisi ya Universal Music Group (UMG), alisema, alikuwa bado anadaiwa albamu moja na lebo ‘joint’ ya Shady-Aftermath, lakini alikubaliana kiroho safi na Dre pamoja na Eminem.

Kama Harmonize na Wasafi wangekubaliana idadi ya nyimbo au albamu, wala wasingeingia kwenye mgogoro. Wangeachana salama. Kama kungekuwa na idadi ya nyimbo anadaiwa, Harmonize angeingia studio kumalizia. Miaka 20 au 10 ya nini? Saini idadi ya nyimbo, zikitimia, kama kuna haja, mnasaini tena

Kiini cha taarifa hii: Mwananchi
Mwandishi: Lukman Maloto

Mkuu unakosea sana unaposema mkataba ni wa shurti (dures based contract). Kwa maana hiyo basi mkataba huo si mkataba tena kisheria na harmonize angeweza shitaki na makubaliano ya huo mkataba kufanywa batili, hivyo kutokulipa 600m

Ningekuelewa kiasi fulan labda ungesema kwamba ni mkataba ambao ulikuwa na "undue influence".., na kiuhalisia maelezo yako yote katika uzi huu ndipo yalipobase wala si dures kama ulivyotanabaisha wewe

Tunapozungumzia "undue influence" kwa lugha yetu rasmi tunasema "nguvu za uchocheo" na kwa sheria yetu ya mikataba inasema hali hii ni ipo pale ambapo mahusiano baina ya wahusika mmoja ana nafasi ya kutawala hiari ya mwingine na kutumia nafasi hiyo kwa faida yake... Na ndio maelezo yako yapo hapa
Miaka miwili iliyopita, Harmonize aliachana na lebo ya WCB, akasema menejimenti ya WCB ilimtaka staa huyo wa umakondeni alipe Sh500 milioni aweze kung’oka.

Ametumbua jipu, kwamba ilibidi auze nyumba zake tatu apate pesa za kuwalipa WCB. Kwamba yalikuwa masharti ya mkataba, Harmonize akitaka kuondoka WCB, alipe Sh500 milioni na gharama za utengenezaji wa nyimbo zote.

Hivi karibuni Harmonize amesema alihaha kupata fedha za kulipa WCB. Kampuni ya vinywaji ya Sayona na Benki ya CRDB ndio walimpa fedha za kukamilisha Sh500 milioni. Hata hivyo, akatakiwa aongeze Sh100 milioni, alizopewa na meneja wake, Sebastian Ndege.

Mchanganuo wa 2021

Harmonize aliuza nyumba yake ambayo haikuwa imekamilika kwa Sh100 milioni. Sayona wakampa Sh200 milioni, halafu CRDB wakampa Sh200 milioni. Seba akaweka Sh100 milioni. Jumla Sh600 milioni.

Lipi sahihi? Nyumba tatu alizouza mwaka 2019 au fedha za CRDB, Sayona na Seba? Mpaka hapo utaona kwamba kuna mahali Harmonize hasemi ukweli.

Sisahau taarifa ya mwaka huu, Harmonize alisema angeongea kila kitu. Kama mwaka huu ndio alisema ukweli, basi 2019 aliongopa.

Hata hivyo, lipo ambalo halibishaniwi. Ni Harmonize kulipa Sh500 milioni. WCB hawajawahi kukanusha. Kiulizo kipo kwenye Sh100 milioni.

Mwaka 2019, Harmonize alisema alilipa WCB Sh500 milioni. Mwaka huu, amesema alizolipa ni Sh600 milioni. Kwa nini mwaka 2019 alipunguza?

Stori ya Harmonize na Bosi kubwa wa WCB, Diamond Platnumz ina matege mno. Utaona inazingirwa na wivu, uongo, tamaa na kufanya kazi kiswahili.

Kwa nini waligombana? Jibu ni vipengele vya mkataba (contractual terms). Kuna mkataba (makubaliano) yenye utashi wa pande zote zenye kusaini na ulaghai au shuruti. Wanasheria huliweka vizuri kwa lugha yao. Huita duress contracts, yaani mikataba isiyo na utashi au ufahamu.

Tafsiri ya duress ni nguvu, lazima au ushawishi wa kumfanya mtu atende jambo bila ridhaa yake. Mathalani, mtu anasaini mkataba akiwa ameshikiwa bunduki, anaambiwa asiposaini atauawa.

Anatekwa mwanaye, mkewe au mumewe, mzazi wake au ndugu yake, halafu anaambiwa asaini mkataba, vinginevyo mateka atauawa. Mikataba ya aina hiyo ni duress.

Kusaini mkataba na mtoto au mtu asiye na ufahamu wa kutosha kuhusu vipengele vya mkataba, hutafsiriwa kuwa aina nyingine ya duress.

Mwaka 2015

Harmonize ni kijana mdogo. Masikini sana. Ndoto yake ni kuwa mwanamuziki. Anaishi mjini Dar es Salaam na Diamond Platnumz ni staa aliyekaa juu ya nchi.

Huwezi kupata picha ya duress katika mikataba ya wasanii kama hutavaa viatu vya msanii underground anayetamani kutoka kimuziki. Ukimuuliza Afande Sele alivyomwona Sugu enzi hizo akitaka asaidiwe kimuziki, akiwa mkweli, utaelewa maana yake.

Jicho la msanii underground kwa msanii aliyefanikiwa ni kama malaika wa pepo. Kwa mantiki hiyo, mwaka 2015, Harmonize ambaye hakuwa akijua chochote, alimwona Diamond ni malaika wa pepo yake.

Jiulize, siku ya kiyama unaona jehanamu ilivyo halafu unaitwa na malaika wa pepo, anakwambia saini mkataba uingie, utapoteza muda? Tusiongopeane, utasaini haraka haraka na kuingia.

Ukishaingia peponi na kuijua pepo ilivyo, ndipo unaweza kumwona malaika wako wa pepo alikupiga, kwamba ulistahili zaidi.

Kumbuka pia kuwa wakati unasaini mkataba wa kuingia peponi, utakuwa na furaha iliyopitiliza, umakini hautakuwepo. Utataka usaini ili ukajionee yaliyomo. Ufaidi simulizi za mito ya maziwa na asali.

Njoo kwa Harmonize. Hajui pepo ya muziki ilivyo ila alifahamu kuwa Diamond yupo peponi na ni malaika wa pepo. Akatokeza kumvuta peponi, unadhani Harmonize angedengua?

Harmonize alipoambiwa na Diamond asaini mkataba aingie kwenye pepo ya muziki, angelaza damu? Bila shaka, alisaini akiwa na furaha iliyopitiliza.

Mwaka 2015 akatoa Aiyola, jamii ikamjua. Mwaka 2016 Bado ilifuata kisha Matatizo. Mpaka hapo Harmonize alikuwa ameshaijua pepo ya muziki. Hakuwa mshamba tena. Kipindi hicho angeambiwa asaini upya mkataba wake na WCB, Kuna vipengele angevikataa. Kumbe sasa, kiuhalisia, mkataba wa Harmonize na WCB, kwenye fikra za Harmonize, ulivunjika tangu mwaka 2016.

Tafsiri nzuri ya mkataba wa duress ni ule ambao anayesaini, muda mrefu unaofuata akiambiwa asaini upya, lazima akatae. Ni kama Harmonize, akili yake ya sasa inamwambia alikosea kusaini.

Dhambi ya mkataba

Mkataba ni makubaliano ya kisheria. Na asili ya mikataba ya muziki ni wajibu wa kila upande. Unachotoa na unachoingiza. Masharti lazima yawe sawa kuhusu mzigo ambao kila upande utabeba kwa kuvunja mkataba.

Mathalani, iliandikwa kuwa Harmonize alitakiwa kulipa Sh500 milioni na kurejesha gharama zote za nyimbo ambazo zilirekodiwa chini ya Wasafi ili kuvunja mkataba.

Sawa! Je, wajibu wa Wasafi kuvunja mkataba ni upi? Kama wao wangeamua kuachana na Harmonize, wangepaswa kumlipa nini? Mkataba wa masharti ya upande mmoja, ni aina nyingine ya duress.

Harmonize kasaidiwa?

Kampuni ya kusimamia muziki huwekeza katika maeneo ya aina mbili; label (utengenezaji na usimamizi wa muziki) na imprint (masoko ya muziki na mwanamuziki).

Kampuni kama Wasafi inapomchukua msanii, inabeba maudhui ya kutengeza na kusimamia muziki pamoja na masoko. Hufanya hivyo kupata faida. Sio msaada!

Wasanii wengi chipukizi wanapochukuliwa na mastaa wakubwa, hudhani wanasaidiwa, hivyo hunyenyekea na kusaini kiholela. Wafahamu kuwa hakuna recording company ya usamaria wema. Husaka fedha.

Kampuni inapofikia hatua ya kukusaini, maana yake huona faida ndani yako, kwa hiyo hupaswi kwenda kikondoo, kudhani unasaidiwa. Ni biashara. Soma vingele bila ushawishi, amua kwa maisha yako. Tena, shirikisha wanasheria.

Kingine, recording company nyingi hutaka kummiliki msanii muda mrefu, ipo hivyo. Mikataba ya muziki huwa haiendi kwa umri, bali kazi.

Wasiseme unasainiwa kwa miaka 20, kama WCB na Harmonize, bali, mnatengeneza albamu ngapi au nyimbo ngapi. Siku hizi soko la kidigitali, zinaangaliwa nyimbo zaidi kuliko albamu.

Suge Knight alipomtoa Tupac jela mwaka 1995 na kumlipia dhamana ya dola milioni moia, Tupac hakusaini umri wa kukaa Death Row Records miaka mingapi, bali walisaini albamu tatu.

Februari 2014, 50 Cent, alipokuwa anasaini mkataba na kampuni ya usambazaji ya Caroline, inayomilikiwa na taasisi ya Universal Music Group (UMG), alisema, alikuwa bado anadaiwa albamu moja na lebo ‘joint’ ya Shady-Aftermath, lakini alikubaliana kiroho safi na Dre pamoja na Eminem.

Kama Harmonize na Wasafi wangekubaliana idadi ya nyimbo au albamu, wala wasingeingia kwenye mgogoro. Wangeachana salama. Kama kungekuwa na idadi ya nyimbo anadaiwa, Harmonize angeingia studio kumalizia. Miaka 20 au 10 ya nini? Saini idadi ya nyimbo, zikitimia, kama kuna haja, mnasaini tena

Kiini cha taarifa hii: Mwananchi
Mwandishi: Lukman Maloto

hakuna dures apo mwandishi arejee sheria ya mikaba vizuri maana yote aliyoiongelea hapo ni "undue influence" Kiswahili fasaha ni "Nguvu ya uchochezi "
 
Msolo

JF-Expert Member
Oct 19, 2008
1,818
2,000
Tumemsikia Hamornize akilalamika, hatujasikia Diamond akijibu chochote. Nadhani kunyamaza ni hekima kuliko kujibu.

Ukweli mwingine ni kuwa habari nyingi zina trend zinapohusishwa na Diamond tu.
 
Mayu

JF-Expert Member
May 11, 2010
4,316
2,000
Kiasili mikataba ya aina hii huwa inavi elements vya unyonyaji
Hata mbele huko inatokea sana

Lakini kwa huu mkataba wa Konde na Wasafi na level alizofikia Konde kwa kuwa Wasafi ........ sioni kwanini Konde bado analia lia kila siku na jambo hili

Mimi naamini Konde anathamani kubwa zaidi ya hiyo ml500
Ni wanamuziki wangapi nje ya Wasafi au Kiba labda Nandy na Marioo? anaweza kudhaninika na kupewa ml500 kama alivyopewa Konde?.......... Hii ni thamani kubwa sana kwake

Binafsi naona kama Konde hatambui ukubwa wake uliotengenezwa na juhudi zake na kubebwa pakukubwa na Wasafi

Leo hii Konde anamiliki lebel, kasaini wasanii wakubwa sasa, anafanya events zake mwenyewe, anaingia mikataba yake kwa lebel yake na hakika ana “wanyonya” pia wasanii wake na ameingia nao mikataba jamii hiyo hiyo tu sababu huwezi kumtengenezea Ibra video ya mill80 kumsaidia wala kumgharamia Cheed, Angela nk mamilioni ya sh kuwasaidia tu wakati hiyo ni biashara na inataka faida kujiendesha
Hii yote ni matunda ya yeye kutokea wasafi

Nikichukua mizania ya kimantiki kisha nikapima mabaya yote Konde anayolalamikia Wasafi kisha nikalinganisha na mazuri yote Konde aliyopata Wasafi na akiyatumia vizuri for the rest of his life basi mzania unaniambia Mmakonde karamba karata dume...... anafaida zaidi ya wasafi

Nadhani anahitaji watu makini kumuelimisha kuhusu hili
Au labda anajua ila akiona kama anayumba basi inabidi atumie jambo hili kama “kiki” ili kumboost

Ni almost miaka mitatu sasa toka aondoke Wasafi. Ni wakati wa ku move on na kuacha kazi zishindane na sio vilio na lawama utafikiri Wasafi walimng’oa koromea la kuimbia
 
Satan

JF-Expert Member
Aug 9, 2017
564
500
Mtu akiwekeza 100M lazima Apate faida ya 1B. Ukilielewa hili, utapaswa utimize.
Tofauti na hapo, umeamzisha uhasama. Ilipaswa ufanye maamuzi kabla ujajihusisha. Maisha yetu waswahili ndivyo yalivo.
 
Najiona Mimi

Member
Aug 15, 2020
53
125
Hakuna shughuli hapo

Harmonize inabidi atoe respect kwa mtu aliyemuokota baada ya kuambiwa na BSS kuwa hajui kuimba ila Diamond akaamini kipaji chake na kumsaidia kufika alipofika leo hii

Huyo rayvanny mwenyewe alikuwa ameachwa na Madee kwenye ile label yao kwa kuambiwa hajui kitu ila Simba akamchukua na kuamini kipaji chake na leo hii yupo juu

Muangalie Mbosso khan leo hii wenzake wa kundi la Ya moto band wapo wapi na wanafanya nini kwenye industry? Aslay na yule Beka flavour

Tuje tumsuguse Zuchu right now, one of the top female artist in East and Central Africa

Ooooh!, This Dude Simba need appreciation kwa kutengeneza wasanii wakubwa ambao wanaweza kufanya competition na yy mwenyewe coz label nyingi hapa bongo wameshindwa kufanya ambacho amekifanya yy

Pia wakumbuke ile music label yake sio kwa ajili ya social charity Ila ipo for profit gain

Kuna kitu nafkiri bado watu weng hatuelewi,diamond n msanii aliydjitengenezea tayar mashabik zake weng na weng n wakudumu,so automatically ukishasainiwa wcb unasupportiwa na mashabik wote wa diamond.
Hii haimaaniahi ww n bora,hapana,nafkiri hakuna msanii wa wcb ambae anaweza akatoa ngoma af isifike views 1m youtube kwa muda mfupi au isipate airtime.
So hao hao wasanii unao waona wakali wakija kutoka wcb automatic mashabik wa diamond wanaacha kumshabikia na kuonekana hajui,hii ni kitu mbaya sana.
Mziki wetu una safari ndefu sana kufika walipofika wenzetu mfano wanaija af kitu nachoona tunakosea kwenye hizi tunazoita lebels hasa za bongo ni kwamba lebel inaendeshwa kama groups kitu amabacho sio.
Since kwenye lebel kila msanii ana mkataba wa kivyake so kila mtu inabid asimamiwe na aishi kivyake ikiwezekana hata msipofahamiana n fresh ndo wanavofanya wenzetu mbele huko,kuendesha kama group ndo mwanzo wa kuonekana mmoja anapendelea kuliko mwengine
 
ni ngumu

JF-Expert Member
Sep 25, 2016
4,155
2,000
Ukisikiliza story ya mtu anayelalamikia jambo kuna njia moja ya kujua kama huyu mtu anaongea ukweli tupu au kachanganya na agenda nyingine

Niseme tu ukisikiliza video ya harmonise utagundua vitu viwili vikubwa

1.Hana alilokosea kabisaaaaaaaa kitu ambacho sio ukweli kibinadamu alipaswa kuwa na kipande ambacho alitakiwa kukubali kabisa niliteleza nikafanya kitu flani baada ya kuona hivi na hivi au kupandwa na hasira.Story nzima harmonise ni victim,huu ni uongo

2.Harmonise anatafuta huruma ya jamii
Hii ni tabia ya wasanii wetu kibongobongo ht mond anafanyaga hivi

Dogo kaelezea vizuri sana ila mistake kubwa aliyofanya ambayo mwenye uelewa mkubwa yeyote ataelewa ni kushindwa ku admit hata mistake yake moja ndogo tu ambayo labda kwa namna moja au nyingine ilileta migogoro.

Harmo amepikwa na mond akapikika,Anajua ku trend na wabongo tunapenda trending cha kuzingatia asisahau kutunga nyimbo zinazotrend.Mond ana trend kwenye music platforms na ujinga ujinga.Harmo amefanikiwa ku trend kwenye social networks awe makini sana kwenye music platforms maana data zinasema anashukaa.
 
Insigne

JF-Expert Member
Jul 3, 2021
2,634
2,000
Kuna kitu nafkiri bado watu weng hatuelewi,diamond n msanii aliydjitengenezea tayar mashabik zake weng na weng n wakudumu,so automatically ukishasainiwa wcb unasupportiwa na mashabik wote wa diamond.
Hii haimaaniahi ww n bora,hapana,nafkiri hakuna msanii wa wcb ambae anaweza akatoa ngoma af isifike views 1m youtube kwa muda mfupi au isipate airtime.
So hao hao wasanii unao waona wakali wakija kutoka wcb automatic mashabik wa diamond wanaacha kumshabikia na kuonekana hajui,hii ni kitu mbaya sana.
Mziki wetu una safari ndefu sana kufika walipofika wenzetu mfano wanaija af kitu nachoona tunakosea kwenye hizi tunazoita lebels hasa za bongo ni kwamba lebel inaendeshwa kama groups kitu amabacho sio.
Since kwenye lebel kila msanii ana mkataba wa kivyake so kila mtu inabid asimamiwe na aishi kivyake ikiwezekana hata msipofahamiana n fresh ndo wanavofanya wenzetu mbele huko,kuendesha kama group ndo mwanzo wa kuonekana mmoja anapendelea kuliko mwengine
Aya sawa
 
goroko77

JF-Expert Member
Jul 9, 2019
1,274
2,000
Kaongeza misamiati siku hizi kuna matusi , huu ndio wimbo wake wa kwanza kwenye album katoa video juzi juzi, haueleweki anaimba nini, hapo kwenye sleep sleep nafikiri alimaanisha halali lali, hiyo outside sijui ndio ametoka

"Yeah hustle everyday I never sleep sleep coz am outside
When am falling love I go deep deep coz am outsidee
Time for the money two for the show enzi za kuuza maji na wanangu wa kariakoo
That was before long time ago I wish you know I wish you know yeaah
"

Chorus:
"We are outside outside outside outside
B*tch am outside outside outside outside
Am outside outside outside (Eeeh)
Kondegang we are outside outside outside (Yah yah yah)
"
Ahahaahah upuuz mtupu
 
Kilaba

Senior Member
Apr 8, 2021
135
250

Mwanamuziki wa kizazi kipya, Harmonize afunguka kuhusu mkataba alioingia na WCB amesema alikuwa akipewa 40% ya mapato yoyote anayoingiza na WCB kuchukua 60% ameamua kuelezea hayo yote kutokana na watu kuwa dhana ya kwamba yeye ni msaliti. Amesema alifanyiwa fitna nyingi zilizopelekea yeye kuondoka kwenye record label hiyo.

Amesema management nzima ya WCB walikuwa wanamuogopa yeye (Harmonize) kwamba anaelekea kumshinda Diamond Platnumz kimuziki, amenongezea pia baba yake Harmonize alivyokuwa akija kumtembelea nyumbani WCB walikuwa wanasema kwamba alikuwa anakwenda kumroga Diamond.

Harmonize ameongezea pia alikwenda Nigeria kwa gharama zake kufanya collabo na Reekado Banks nchini Nigeria na akakatwa dola 5000 na WCB. Alipoona fitna zimezidi alijaribu kutafuta amani lakini ilishindikana, amesema mkataba wake na WCB alishauriwa na Joseph Kusaga kwamba akitafuta mwanasheria asingelipa chochote lakini hakutaka kupambana kwa njia hiyo na akaamua kulipa hela tu (Milioni 600) ili tu kupata amani.

------ Maoni ya Wadau -----------

KuLe juu umeandika vzr sana..huku chini umeishiwa maneno.... Sisi ni binadamu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom