Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,938
25,279





Mwanamuziki wa kizazi kipya, Harmonize afunguka kuhusu mkataba alioingia na WCB amesema alikuwa akipewa 40% ya mapato yoyote anayoingiza na WCB kuchukua 60% ameamua kuelezea hayo yote kutokana na watu kuwa dhana ya kwamba yeye ni msaliti. Amesema alifanyiwa fitna nyingi zilizopelekea yeye kuondoka kwenye record label hiyo.

Amesema management nzima ya WCB walikuwa wanamuogopa yeye (Harmonize) kwamba anaelekea kumshinda Diamond Platnumz kimuziki, amenongezea pia baba yake Harmonize alivyokuwa akija kumtembelea nyumbani WCB walikuwa wanasema kwamba alikuwa anakwenda kumroga Diamond.

Harmonize ameongezea pia alikwenda Nigeria kwa gharama zake kufanya collabo na Reekado Banks nchini Nigeria na akakatwa dola 5000 na WCB. Alipoona fitna zimezidi alijaribu kutafuta amani lakini ilishindikana, amesema mkataba wake na WCB alishauriwa na Joseph Kusaga kwamba akitafuta mwanasheria asingelipa chochote lakini hakutaka kupambana kwa njia hiyo na akaamua kulipa hela tu (Milioni 600) ili tu kupata amani.

------ Maoni ya Wadau -----------

Miaka miwili iliyopita, Harmonize aliachana na lebo ya WCB, akasema menejimenti ya WCB ilimtaka staa huyo wa umakondeni alipe Sh500 milioni aweze kung’oka.

Ametumbua jipu, kwamba ilibidi auze nyumba zake tatu apate pesa za kuwalipa WCB. Kwamba yalikuwa masharti ya mkataba, Harmonize akitaka kuondoka WCB, alipe Sh500 milioni na gharama za utengenezaji wa nyimbo zote.

Hivi karibuni Harmonize amesema alihaha kupata fedha za kulipa WCB. Kampuni ya vinywaji ya Sayona na Benki ya CRDB ndio walimpa fedha za kukamilisha Sh500 milioni. Hata hivyo, akatakiwa aongeze Sh100 milioni, alizopewa na meneja wake, Sebastian Ndege.

Mchanganuo wa 2021

Harmonize aliuza nyumba yake ambayo haikuwa imekamilika kwa Sh100 milioni. Sayona wakampa Sh200 milioni, halafu CRDB wakampa Sh200 milioni. Seba akaweka Sh100 milioni. Jumla Sh600 milioni.

Lipi sahihi? Nyumba tatu alizouza mwaka 2019 au fedha za CRDB, Sayona na Seba? Mpaka hapo utaona kwamba kuna mahali Harmonize hasemi ukweli.

Sisahau taarifa ya mwaka huu, Harmonize alisema angeongea kila kitu. Kama mwaka huu ndio alisema ukweli, basi 2019 aliongopa.

Hata hivyo, lipo ambalo halibishaniwi. Ni Harmonize kulipa Sh500 milioni. WCB hawajawahi kukanusha. Kiulizo kipo kwenye Sh100 milioni.

Mwaka 2019, Harmonize alisema alilipa WCB Sh500 milioni. Mwaka huu, amesema alizolipa ni Sh600 milioni. Kwa nini mwaka 2019 alipunguza?

Stori ya Harmonize na Bosi kubwa wa WCB, Diamond Platnumz ina matege mno. Utaona inazingirwa na wivu, uongo, tamaa na kufanya kazi kiswahili.

Kwa nini waligombana? Jibu ni vipengele vya mkataba (contractual terms). Kuna mkataba (makubaliano) yenye utashi wa pande zote zenye kusaini na ulaghai au shuruti. Wanasheria huliweka vizuri kwa lugha yao. Huita duress contracts, yaani mikataba isiyo na utashi au ufahamu.

Tafsiri ya duress ni nguvu, lazima au ushawishi wa kumfanya mtu atende jambo bila ridhaa yake. Mathalani, mtu anasaini mkataba akiwa ameshikiwa bunduki, anaambiwa asiposaini atauawa.

Anatekwa mwanaye, mkewe au mumewe, mzazi wake au ndugu yake, halafu anaambiwa asaini mkataba, vinginevyo mateka atauawa. Mikataba ya aina hiyo ni duress.

Kusaini mkataba na mtoto au mtu asiye na ufahamu wa kutosha kuhusu vipengele vya mkataba, hutafsiriwa kuwa aina nyingine ya duress.

Mwaka 2015

Harmonize ni kijana mdogo. Masikini sana. Ndoto yake ni kuwa mwanamuziki. Anaishi mjini Dar es Salaam na Diamond Platnumz ni staa aliyekaa juu ya nchi.

Huwezi kupata picha ya duress katika mikataba ya wasanii kama hutavaa viatu vya msanii underground anayetamani kutoka kimuziki. Ukimuuliza Afande Sele alivyomwona Sugu enzi hizo akitaka asaidiwe kimuziki, akiwa mkweli, utaelewa maana yake.

Jicho la msanii underground kwa msanii aliyefanikiwa ni kama malaika wa pepo. Kwa mantiki hiyo, mwaka 2015, Harmonize ambaye hakuwa akijua chochote, alimwona Diamond ni malaika wa pepo yake.

Jiulize, siku ya kiyama unaona jehanamu ilivyo halafu unaitwa na malaika wa pepo, anakwambia saini mkataba uingie, utapoteza muda? Tusiongopeane, utasaini haraka haraka na kuingia.

Ukishaingia peponi na kuijua pepo ilivyo, ndipo unaweza kumwona malaika wako wa pepo alikupiga, kwamba ulistahili zaidi.

Kumbuka pia kuwa wakati unasaini mkataba wa kuingia peponi, utakuwa na furaha iliyopitiliza, umakini hautakuwepo. Utataka usaini ili ukajionee yaliyomo. Ufaidi simulizi za mito ya maziwa na asali.

Njoo kwa Harmonize. Hajui pepo ya muziki ilivyo ila alifahamu kuwa Diamond yupo peponi na ni malaika wa pepo. Akatokeza kumvuta peponi, unadhani Harmonize angedengua?

Harmonize alipoambiwa na Diamond asaini mkataba aingie kwenye pepo ya muziki, angelaza damu? Bila shaka, alisaini akiwa na furaha iliyopitiliza.

Mwaka 2015 akatoa Aiyola, jamii ikamjua. Mwaka 2016 Bado ilifuata kisha Matatizo. Mpaka hapo Harmonize alikuwa ameshaijua pepo ya muziki. Hakuwa mshamba tena. Kipindi hicho angeambiwa asaini upya mkataba wake na WCB, Kuna vipengele angevikataa. Kumbe sasa, kiuhalisia, mkataba wa Harmonize na WCB, kwenye fikra za Harmonize, ulivunjika tangu mwaka 2016.

Tafsiri nzuri ya mkataba wa duress ni ule ambao anayesaini, muda mrefu unaofuata akiambiwa asaini upya, lazima akatae. Ni kama Harmonize, akili yake ya sasa inamwambia alikosea kusaini.

Dhambi ya mkataba

Mkataba ni makubaliano ya kisheria. Na asili ya mikataba ya muziki ni wajibu wa kila upande. Unachotoa na unachoingiza. Masharti lazima yawe sawa kuhusu mzigo ambao kila upande utabeba kwa kuvunja mkataba.

Mathalani, iliandikwa kuwa Harmonize alitakiwa kulipa Sh500 milioni na kurejesha gharama zote za nyimbo ambazo zilirekodiwa chini ya Wasafi ili kuvunja mkataba.

Sawa! Je, wajibu wa Wasafi kuvunja mkataba ni upi? Kama wao wangeamua kuachana na Harmonize, wangepaswa kumlipa nini? Mkataba wa masharti ya upande mmoja, ni aina nyingine ya duress.

Harmonize kasaidiwa?

Kampuni ya kusimamia muziki huwekeza katika maeneo ya aina mbili; label (utengenezaji na usimamizi wa muziki) na imprint (masoko ya muziki na mwanamuziki).

Kampuni kama Wasafi inapomchukua msanii, inabeba maudhui ya kutengeza na kusimamia muziki pamoja na masoko. Hufanya hivyo kupata faida. Sio msaada!

Wasanii wengi chipukizi wanapochukuliwa na mastaa wakubwa, hudhani wanasaidiwa, hivyo hunyenyekea na kusaini kiholela. Wafahamu kuwa hakuna recording company ya usamaria wema. Husaka fedha.

Kampuni inapofikia hatua ya kukusaini, maana yake huona faida ndani yako, kwa hiyo hupaswi kwenda kikondoo, kudhani unasaidiwa. Ni biashara. Soma vingele bila ushawishi, amua kwa maisha yako. Tena, shirikisha wanasheria.

Kingine, recording company nyingi hutaka kummiliki msanii muda mrefu, ipo hivyo. Mikataba ya muziki huwa haiendi kwa umri, bali kazi.

Wasiseme unasainiwa kwa miaka 20, kama WCB na Harmonize, bali, mnatengeneza albamu ngapi au nyimbo ngapi. Siku hizi soko la kidigitali, zinaangaliwa nyimbo zaidi kuliko albamu.

Suge Knight alipomtoa Tupac jela mwaka 1995 na kumlipia dhamana ya dola milioni moia, Tupac hakusaini umri wa kukaa Death Row Records miaka mingapi, bali walisaini albamu tatu.

Februari 2014, 50 Cent, alipokuwa anasaini mkataba na kampuni ya usambazaji ya Caroline, inayomilikiwa na taasisi ya Universal Music Group (UMG), alisema, alikuwa bado anadaiwa albamu moja na lebo ‘joint’ ya Shady-Aftermath, lakini alikubaliana kiroho safi na Dre pamoja na Eminem.

Kama Harmonize na Wasafi wangekubaliana idadi ya nyimbo au albamu, wala wasingeingia kwenye mgogoro. Wangeachana salama. Kama kungekuwa na idadi ya nyimbo anadaiwa, Harmonize angeingia studio kumalizia. Miaka 20 au 10 ya nini? Saini idadi ya nyimbo, zikitimia, kama kuna haja, mnasaini tena

Kiini cha taarifa hii: Mwananchi
Mwandishi: Lukman Maloto

View attachment 2019980


Naomba kuweka wazi kabisa kwamba mimi si mpenzi wa Muziki wa Tanzania na wala siwapendi wanamuziki wa Tanzania , hii ni kwa vile wamekuwa mara zote wakitumika na CCM kuwapotosha wananchi , na hasa hawa wanaoitwa Wanamuziki wa kizazi kipya , ambao pia wanatuhumiwa kusafirisha na kusambaza madawa ya kulevya hivyo kuharibu nguvu kazi ya Taifa.

Bali nimesononeshwa sana na yaliyojitokeza kwenye mgogoro wa Harmonize na Diamond , pale huyo Harmonize alipokuwa anaomba kujitoa kwenye lebo ya WASAFI , mengi sana ameongea mwenyewe kila mtu kayasikia wala sina haja ya kuyarudia , bali nitagusia kidogo maeneo mawili tu.

Kwamba Diamond alimwambia Harmonize kwamba anaweza asimkamilishie kile anachotaka na wala hatomfanya chochote na kokote atakakoenda hatofanikiwa , kwa vile HAMUWEZI KISERIKALI , KIFEDHA NA KIUCHAWI , hii ni kauli ya kijinga sana kutolewa na anayeitwa msanii mkubwa , ni kauli ya kishamba sana iliyojaa Utanzania mtupu!

Jambo lingine linalotia aibu ni kitendo cha Harmonize Kuomba msaada kwa Magufuli moja kwa moja baada ya ngazi za chini ikiwemo wizara kumgwaya Diamond , Yaani Rais wa nchi ampigie simu Msela Diamond na kumbembeleza ili akubali kuterminate mkataba wa Harmonize na Wasafi ! hili ni jambo la kutia aibu sana , Yaani inawezekanaje Wizara na BASATA kutiwa mfukoni na msanii mmoja?

Haya mambo yakiachwa iko siku yatakuja kufedhesha mamlaka ya Rais , na sisi kama wananchi hatutakubali.

Mambo yanakwenda kasi sana, joto linazidi kukimbiza huku jua likichoma kishenzi. Wakati tukifikiria ni kwa namna gani tunaweza kusurvive huku maji na umeme vikiwa shida, wasanii nao wanaibuka na mambo yao, yaani ni shida juu ya shida.

Haya! Wengi mmeniambia nije na makala kuhusu jambo hilo, basi niseme ninakuja na hii makala, ila kabla ya kuendelea, weka uteam pembeni kwanza, tuzungumzie mambo halisi.

Mimi sina timu, huwa ninazungumza kitu ambacho ni cha kweli, kile kilichokuwa kwenye mtazamo wangu, kubwa zaidi, huwa si mpenzi wa miziki ya Bongo fleva, hata simu yangu, huwezi kukuta ngoma za hapa Bongo.

Lakini kwenye yote, acha nijaribu kuelezea kile nilichokiona tangu siku ya kwanza Harmonize anapoondoka WCB mpaka leo, nitajaribu kufafanua ninayoyaona, kama una yako, basi na wewe kaandae makala tuje kusoma.

MKATABA WA 40%
Nianze na suala la mkataba. Kwanza kitu cha kwanza tujue unapokuwa huna pesa, una maisha magumu, ukiletewa mkataba wowote ule ambao unaonyesha utakuwa unaingiza pesa ni lazima utausaini kwa sababu usipousaini, inamaanisha unakubaliana na maisha ya dhiki unayoishi.

Leo nikisema ninahitaji waigizaji kwenye filamu yangu, halafu nikisema bwana mimi sina hela ya kumlipa msanii, ila ukifanya kazi na mimi, utapata jina na kuitwa kwenye muvi za watu wengine, utaacha nafasi hiyo kwa sababu hutolipwa? Je, utaendelea kukaa kwenye maisha hayo na kuachana na opportunity ambayo itakufanya kujulikana?

Kwenye hili! Kwanza tusimlaumu Harmonize kwamba kwa nini amesaini mkataba wa kulipwa asilimia 40 kwa sababu naamini hata ungekuwa wewe, kwa maisha ya dhiki, halafu unajua nikifanya kazi na Mondi, nitajulikana na kutengeneza pesa, kwa nini usikubali?

Kampuni nyingi za Tanzania zina mikataba mibovu na tunaiingia kwa sababu tuna shida ya pesa, tupo kwenye maisha ya kimasikini sana, unakubali kusaini mikataba mibovu kwa sababu unataka pesa, ama umaarufu ili baadaye utusue.

Unapoingia kwenye mikataba hiyo, unaona kabisa unanyonywa, ila huna ujanja, kuna kitu unakitafuta lakini moyo wako unasema siku moja nitaondoka tu, nikishapata pesa za kutosha nasepa.

Hilo ndilo wamekuwa wakilisema hata wajasiriamali, unapotaka kuanzisha biashara yako, kwanza anza kuajiriwa, upate pesa kisha ondoka ukaanzishe biashara yako, ndivyo ilivyokuwa kwa Harmonize.

Asingeweza kukaa WCB milele, ilikuwa ni lazima siku moja aondoke. Ukishapata pesa na umaarufu uliokuwa unautaka, sasa unasema huu ndiyo muda wa kuondoka, unaondoka zako, kuna watu wengi wamefanya hivyo, yeye si wa kwanza.

Kosa kubwa wanalofanya WCB ni aina ya mikataba wanayoingia na wasanii, msanii akiondoka, akilipia pesa, imekula kwao ila si kama lebo nyingi za Marekani.

Leo hii Drake, Nicki Minaj hawapo Young Money, ila kwenye kila pesa wanayotengeneza huko walipo, kuna asilimia inaingia kwenye lebo hiyo na maisha yanasonga.

Suala la Harmonize kuingia mkataba wa aina hiyo, simlaumu kwa sababu hata wewe unayesoma hapa, huko kazini kwako umeingia mkataba wa aina hii hii, hujilaumu wewe, unamlaumu Harmonize.

Kijana wa Kitanzania anapotaka kutafuta jina ama pesa, anakuwa tayari kufanya jambo lolote lile. Nilipokea meseji nyingi tu, mtu anakwambia “Bro! Natamani kuigiza, nitaigiza hata bure.”

Unajua anamaanisha nini? Anachohitaji ni kutafuta jina, anaamini hapo baadaye atakuja kuwa na jina na atapiga pesa tu kwani akihitaji pesa sasa hivi, anaweza asizipate na ukawa mwisho wa ndoto zake.

Sasa mtu huyu akikubali kuigiza bure ama kwa malipo madogo, siku akipata jina na kutaka kuondoka, cha kwanza tutatakiwa kupitia mkataba wake, tufanye tulichokubaliana na tuache aondoke.

Maisha popote pale.

HARMONIZE VIJEMBE KWA MONDI
Harmonize aliondoka WCB na kilichofuata ni kutoa vijembe na matatizo yaliyokuwepo hapo. Kuna wengi walisema kwa nini asingesema akiwa hapo? Kama wewe unajiuliza swali hilo, jishike kifuani na sema mimi ni mjinga sana.

Kuna wachezaji wengi wa mpira wakiwa timu fulani, hawazungumzi mbovu, ila wakiondoka ndipo utasikia ile timu mbaya sana, kocha magumashi na mengine mengi.

Ukiwa kwenye nyumba mbaya, husemi kwa watu kwamba ni mbaya, utataka uondoke halafu ndiyo useme ilikuwa nyumba mbaya.

Leo umeoa, huwaambii watu kama mkeo ni malaya, unasubiri umuache ndiyo uanze kusema yule mwanamke alikuwa malaya, halafu hajui kupika, kikojozi na kitandani gogo. Kwa nini usiseme wakati akiwa ndani?

Madhaifu ya sehemu tunayasema tukishaondoka sehemu hiyo.

Suala la Harminize kumpiga vijembe Mondi ni kawaida kila kona. Bado ana hasira, labda kwa yale aliyowahi kutendewa ambayo aliona hayafai, taswira ikimjia, anakuwa na hasira na kujikuta ameropoka hili na lile.

Mtu akiondoka sehemu kwa vita, atahitaji kukaa muda mrefu mpaka akili yake kuja kukaa sawa.

HARMONIZE AMEKOSEA?
Jibu ni ndiyo! Wakati mwingine unapoondoka sehemu, achana na kila kitu, nenda kafanye mambo yako, achana na yaliyopita. Harmonize alishindwa kufanya mambo yake.

Alimkalia Diamond kooni, akaikalia WCB kooni, akawa anatoa vijembe kutwa. Nikahisi labda naye Diamond kwa kuwa amekuwa mkongwe angekaa kimya, ila cha ajabu naye akaanza kumrushia vijembe hasa kwenye nyimbo ambazo alishirikishwa, nikajua wote bado ni watoto ama kila mtu hataki kuonekana mpole kwa mwenzake.

MONDI AMEKOSEA?
Kuna msemo wa Kitanzania unasema ukigombana na mtu mmoja halafu ukasema ana matatizo, basi tunaweza kuamini kwamba kweli ana matatizo, ila ukigombana na watu watano, tutashindwa kukuelewa ukisema wana matatizo, tutakwambia kwamba wewe ndiye una matatizo.

Leo ukiniambia Mondi ana matatizo, nitakataa hilo, yeye hana matatizo bali watu waliomzunguka ndiyo wana matatizo. Namfahamu msela, nimekua naye mtaa mmoja, tangu kishuleshule mpaka alipoanza muziki japo sisi wengine tulikuwa bize na shule.

Jamaa ana uswahili kama sisi ila kuhusu roho mbaya, kwa mchizi hilo nakataa kwa kuwa tabia ni kama ngozi, huwa haijifichi, ningeliona hilo tangu kipindi kile alipokuwa akitoroka shule na kwenda kuimbaimba kila alipoona muziki ama kutafuta hela kwa kuuza nguo kwa kudandia Tandale sokoni.

Unapokuwa unakutana na watu ambao wanaweza kuibadilisha akili yako na kukupa nyingine kabisa. Ukiwapa nafasi, wanachukua maamuzi yao mabovu na kuwa yako, na wanafanya lolote lile ambalo mwisho wa siku litaonyesha taswira mbaya juu yako.

Kama ulifuatilia mwanzoni, vijembe vingi vya Harmonize havikuwa kwa Mondi moja kwa moja, alijua kabisa mchizi alikuwa mtu poa ila kuna mtu ambaye hakuwa poa, na ndiye aliyekuwa akimpiga vita sana.

Na ninadhani baada ya kuonekana hajibu kitu, ni kama akashinikizwa kujibu, naye ndipo alipoanza kujibu.

Kosa la Diamond ni kuanza kujibizana na Harmonize. Angekaa kimya tu, mtu umekwishamtoa, umemfanya kujulikana kupitia wewe, ana kitu gani cha kujimwambafai kwako? Wewe nyamaza tu, dunia itaendelea kujua kwamba bila wewe, yeye asingekuwepo hapo alipokuwa.

Kumjibu Harmonize ni jambo baya sana ambalo Diamond amelifanya, alitakiwa kuwa kimya tu, aendelee kufanya mishe zake kama kawaida kwa sababu siku zote huwezi kumfananisha yeye na Harmonize, bado ni kijana mdogo sana kwenye mafanikio ya muziki.

Kinyago umekichonga mwenyewe, kinakutishaje? Unakiogopea nini? Kama ningekuwa Mondi, nisingemjibu Harmonize ama kumpa kijembe kwenye wimbo wowote ule, ningewakataza Juma Lokole na Baba Levo kumuongelea Harmonize, yaani ningeachana naye mazima. Kumuongelea na kumtupia vijembe inaonyesha kabisa naye Mondi anatamani kusikika mitandaoni akibishana na Harmonize ambaye kiukweli ni mdogo mno kwake.

NI KWELI HARMONIZE AMEBADILIKA?
Bado najiuliza swali hilo. Nakumbuka kipindi cha nyuma wakati akiwa WCB, wakati huo nikiwa mwandishi wa habari. Hakuna kitu ambacho Harmonize anakikataa kama kumuona mtu akipiga picha na Diamond. Yaani alikuwa anakukazia ileile.

Harmonize alikuwa maana halisi ya mringaji, alijua kufanya kitu chochote kile usimfikie Diamond kwa lolote lile, hata ukiwa shabiki wake kwa namna gani, ila leo namuona si Harmonize yule, amekuwa mnyenyekevu, mpole na amekuwa na moyo wa kusaidia wengine, huwa ninajiuliza kutoka WCB kumembadilisha kuwa hivyo ama kule aliambiwa awe na maisha yale hata kuwabania watu kupiga picha na Mondi? Sijapata jibu.

KOVU LA HARMONIZE LITAMTESA MONDI MILELE
Harmonize alikuwa msanii wa Mondi, yaani yeye ndiye ambaye alimchukua yeye kama yeye, si kama hao wengine ambao ameletewa. Harmonize alikuwa kipenzi cha Mondi, aliaminiwa na kuonyeshwa chocho zote.

Kipindi kile Mondi alipokuwa akisafiri, alikuwa akiongozana na Harmonize kila kona, alimtambulisha kwa kila mtu, kwa kifupi alimwamini kwa kuwa alikuwa msanii wake, hakuletewa kama ilivyokuwa kwa hao wengine.

Ukiangalia kipindi hicho, Mondi alikuwa akisafiri sana na Harmonize kuliko hata Rayvanny, alijua kwamba huyu ni msanii wangu mimi, mrithi wangu, halafu ghafla tu, huyo mrithi akasepa zake. Kama ni kupigwa na kitu kizito kichwani, basi Harmonize amejua kumpiga nacho Mondi.

Suala la Harmonize litaendelea kumtesa, kama ni mzimu wake basi utaendelea kumtokea. Rich Mavoko ameondoka WCB lakini humsikii Mondi akimzungumzia, wengine watakuja na kuondoka, hatowazungumzia, ila kwa Harmonize, hatoweza kujishika hata kidogo.

Alitumia pesa na muda kwa ajili yake, alimwamini, akampa kila kitu ili dogo atusuea, kipindi kile akampa mpaka mademu wa kupiga nao skendo, mara katoka na Wolper, mara na huyu, yaani yote ilikuwa ni kumtengenezea jina dogo ili afuatiliwe, mwisho wa siku kilichotokea, kimemuumiza mno mno mno.

HIVI MMEMFIKIRIA RAYVANNY YUPO KWENYE HALI GANI?
Huyu amesahaulika. Jana baada ya kusikia mahojiano ya Harmonize na kuplay ile voice record, nikaanza kumfikiria Rayvanny yupo kwenye hali gani. Kuna jamaa mmoja mpenzi wa WCB aliweka video zikimuonyesha Rayvanny akiwa kwenye mahojiano kipindi cha nyuma akisema alihisi anarekodiwa na Harmonize, nikamuuliza jamaa maswali kadhaa.

Mtu ameondoka WCB kwa ugomvi mzito, leo anaongea na wewe, unajua kabisa unarekodiwa, je, ungeweza kumtemea shit bosi wako? Yaani mimi nimeondoka kwa ugomvi, halafu unaongea na mimi, unajua kabisa nakurekodi, je, ungeongea shit kwa bosi? Jibu ni hapana.

Rayvanny hakuwa akijua hilo ila baadaye akasanuka kwamba inawezekana yale mazungumzo yake na Harmonize yalikuwa yakirekodiwa, akaamua kujitetea mapema kabisa ili siku yatakapokuja kuwekwa hadharani basi tuseme jamaa alijua kama alikuwa akirekodiwa. Wakati mwingine inahitaji akili kubwa kucheza michezo ya kijanja.

CHUKI, HOFU VIMETAWALA BONGO
Kitu ambacho nakataa na nitaendelea kukataa ni pale mtu akiniambia kuna siku muziki wetu utasikika duniani kama ulivyo muziki wa Nigeria, hicho kitu sahau bro!

Sisi tumejaza chuki mioyoni mwetu, Watanzania hatupendani, unaweza kuzungumza na mtu vizuri, kumbe anakuchukia na hujui, anaziba baraka zako na hujui kabisa.

Wanamuziki wanachukiana wao kwa wao, mbaya zaidi kwa sasa wapo kimakundi, yaani kuna Team Mondi, Team Harmonize na Team Kiba, kwa staili hiyo tutafika vipi huko mbele? Hatuwezi.

Leo tutawaona wasanii wakigombea tuzo, bila aibu, nampigia kura msanii wa nje na kumuacha wa ndani, hiki ni kitu ambacho Wanigeria hawakifanyi, wanapoamua kusapotiana, wanasapotiana kwa asilimia mia moja.

Leo Burna Boy anakwenda Marekani kuperform, anawachukua maunderground wake anapaa nao kwenda huko, anawatambulisha jukwaani na ngoma zao zinapigwa, na hata kuperform, wanatangazana tu baadate tunasema huyu Burna Boy na Mondi, Mondi mkongwe, ila leo ukiuliza nani mwanamuziki mkubwa, utasema Burna ni mkubwa mara kumi ya Mondi.

Hatuwezi kufika mbele bila kusapotiana. Kwa kitendo cha Mondi kwenda Marekani bila kuwa na msanii yeyote yule ni kosa, analeta ubinafsi lakini simlaumu sana kwa kuwa yamekwishamtokea puani kwa Harmonize, alimuonyesha njia mwisho wa siku akaachwa kwenye mataa, wakati mwingine bora uonekane mbinafsi kuliko mjinga.

Kwa maelezo ya Harmo kipindi cha nyuma alisema kwamba ukienda Nigeria, ni vigumu sana kusikia klabu wakipiga ngoma za Tanzania, ila cha ajabu, sisi tunaongoza kupiga ngoma zao.

Niwaambie tu, ili muziki wetu ufike mbali, tusubiri hizi zama za Mondi, Kiba na Harmonize zipite, waje wengine wenye kiu ya kuwainua wengine kimataifa, kidogo tutaweza kusogea.

JPM ALIWEKEWA WAKATI MGUMU
Hayati JPM alikuwa kwenye wakati mgumu sana. Mondi na Harmonize walikuwa vijana wake, aliwapenda na kuwapamba wote wawili, mwisho wa siku akapokea simu kutoka kwa Harmonize na kuombwa msaada wa kitu ambacho Mondi hakuwa akikitaka bila shaka.

Kama mzazi, lazima utakuwa na wakati mgumu, hapo ni lazima umfurahishe mmoja na kumliza mmoja, ila alichokiangalia na kukifanya, ni hekima kama mtu mzima, simu yake moja kwa Waziri Mwakyembe ikamuweka Harmonize huru. Pongezi sana kwake kwa hekima zake.

Kuna kila sababu ya Harmonize kulia sana msibani mpaka kuchora tattoo ya Hayati JPM. Alimfanyia mambo mazuri likiwemo hilo, na kwa kile alichomfanyia, tattoo hiyo haitakiwi kufutwa mwilini mwake mpaka kifo chake. Bila yeye, inawezekana asingekuwa huru mpaka leo.

NB: Kweli Konde Jeshi, yaani amekaa na haya yote kwa miaka mitatu na wakati Manara alishindwa kukaa nayo hata kwa wiki moja tu.
 
Huyu mziki ushamshinda,album inafanya vibaya.

Sasa Diamond kama angetaka kila siku kuwa yy.

Kaanzisha lebo ambayo imemtoa yy.
Kampeleka nje kufanya video kubwa.
Kamkutanisha na wasanii wakubwa Africa.
Kamtoa Rayvanny mpaka kufikia hatua ya Colabo na Maluma na kuchukua BET,Tz hii Rayvanny ndiye mwenye nyimbo yenye streams nyingi, kapiga show jukwaa la essence, mafanikio ambayo Diamond hajawahi kuya fikia.

Angeamua kuto kuanzisha label tusinge mjua na Diamond ni mfanyabiashara, always ana angalia faida na label zote duniani zina angalia faida, hata yy na JembeniJembe wanaangalia faida.

Yeye mwenyewe kuimba aliambiwa hajui, Diamond kakaa nae zaidi ya miaka mitatu, akimfundisha na kumpika kimuziki na kuna watu walimwambia hajui kuimba ila Mondi hakukata nae tamaa, kula,kuvaa na kulala kwa Diamond.

Anadai WCB walikuwa wana muogopa yy, haya leo zaidi ya miaka miwili nje ya WCB, yupo yy peke yake,free habanwi je kafika wapi,kampita Diamond?Anapata airtime ktk media zote kubwa zilizo kuwa hazipigi nyimbo zake.

Halafu haja tuambia wasanii wake wanapata kiasi gani, mikataba yao miaka mingapi,wana miaka miwili hawa heleweki wanafanya nini.
 
Huyu mziki ushamshinda,album inafanya vibaya.

Sasa Diamond kama angetaka kila siku kuwa yy.

Kaanzisha lebo ambayo imemtoa yy.
Kampeleka nje kufanya video kubwa.
Kamkutanisha na wasanii wakubwa Africa.
Kamtoa Rayvanny mpaka kufikia hatua ya Colabo na Maluma.

Angeamua tu kuto kuanzisha label tusinge mjua na Diamond mfanyabiashara, always ana angalia faida na label zote duniani zina angalia faida, hata yy na JembeniJembe wanaangalia faida.

Yeye mwenyewe kuimba aliambiwa hajui, Diamond kakaa nae zaidi ya miaka mitatu, akimfundisha na kumpika kimuziki na kuna watu walimwambia hajui kuimba ila Mondi hakukata nae tamaa, kula kulala kwa Diamond.

Anadai WCB walikuwa wana muogopa yy, haya leo zaidi ya mwaka wa pili, yupo yy peke yake je kafika wapi,kampita Diamond?Anapata airtime ktk media zote kubwa zilizo kuwa hazipigi nyimbo zake.

Halafu haja tuambia wasanii wake wanapata kiasi gani, mikataba yao miaka mingapi,wana miaka miwili hawa heleweki wanafanya nini.

Asante kwa kumaliza kila kitu mdau
 
Huyu mziki ushamshinda,album inafanya vibaya.

Sasa Diamond kama angetaka kila siku kuwa yy.

Kaanzisha lebo ambayo imemtoa yy.
Kampeleka nje kufanya video kubwa.
Kamkutanisha na wasanii wakubwa Africa.
Kamtoa Rayvanny mpaka kufikia hatua ya Colabo na Maluma.

Angeamua tu kuto kuanzisha label tusinge mjua na Diamond mfanyabiashara, always ana angalia faida na label zote duniani zina angalia faida, hata yy na JembeniJembe wanaangalia faida.

Yeye mwenyewe kuimba aliambiwa hajui, Diamond kakaa nae zaidi ya miaka mitatu, akimfundisha na kumpika kimuziki na kuna watu walimwambia hajui kuimba ila Mondi hakukata nae tamaa, kula kulala kwa Diamond.

Anadai WCB walikuwa wana muogopa yy, haya leo zaidi ya mwaka wa pili, yupo yy peke yake je kafika wapi,kampita Diamond?Anapata airtime ktk media zote kubwa zilizo kuwa hazipigi nyimbo zake.

Halafu haja tuambia wasanii wake wanapata kiasi gani, mikataba yao miaka mingapi,wana miaka miwili hawa heleweki wanafanya nini.
Hii fungulia thread mpya.
 
Huyu mziki ushamshinda,album inafanya vibaya.

Sasa Diamond kama angetaka kila siku kuwa yy.

Kaanzisha lebo ambayo imemtoa yy.
Kampeleka nje kufanya video kubwa.
Kamkutanisha na wasanii wakubwa Africa.
Kamtoa Rayvanny mpaka kufikia hatua ya Colabo na Maluma na kuchukua BET, mafanikio ambayo Diamond hajawahi kuya fikia.

Angeamua kuto kuanzisha label tusinge mjua na Diamond ni mfanyabiashara, always ana angalia faida na label zote duniani zina angalia faida, hata yy na JembeniJembe wanaangalia faida.

Yeye mwenyewe kuimba aliambiwa hajui, Diamond kakaa nae zaidi ya miaka mitatu, akimfundisha na kumpika kimuziki na kuna watu walimwambia hajui kuimba ila Mondi hakukata nae tamaa, kula,kuvaa na kulala kwa Diamond.

Anadai WCB walikuwa wana muogopa yy, haya leo zaidi ya mwaka wa pili nje ya WCB, yupo yy peke yake,free habanwi je kafika wapi,kampita Diamond?Anapata airtime ktk media zote kubwa zilizo kuwa hazipigi nyimbo zake.

Halafu haja tuambia wasanii wake wanapata kiasi gani, mikataba yao miaka mingapi,wana miaka miwili hawa heleweki wanafanya nini.
Mwenye akili hapa atakuelewa mkuu
 
Anadai WCB walikuwa wana muogopa yy, haya leo zaidi ya mwaka wa pili, yupo yy peke yake,free habanwi je kafika wapi,kampita Diamond?Anapata airtime ktk media zote kubwa zilizo kuwa hazipigi nyimbo zake.
Mashabiki wake wanamdanganya kwa sasa yeye ndo msanii mkubwa zaidi Tanzania...

Anasahau hata huku kufurukuta kwake ni kwa sababu tu Kiba amelala usingizi...

Wiki chache zilizopita Kiba akaamua kutoka usingizini na hapo hapo Harmonize akaanza kusahaulika... thanks to Kiba kajirudia zake kuvuta shuka!!

Harmonize ashukuru sana relaxation ya Kiba lakini Kiba akirudisha nguvy japo kwa 50%, Harmonize atabaki kushindana na akina Rayvanny!
 
Mashabiki wake wanamdanganya kwa sasa yeye ndo msanii mkubwa zaidi Tanzania...

Anasahau hata huku kufurukuta kwake ni kwa sababu tu Kiba amelala usingizi...

Wiki chache zilizopita Kiba akaamua kutoka usingizini na hapo hapo Harmonize akaanza kusahaulika... thanks to Kiba kajirudia zake kuvuta shuka!!

Harmonize ashukuru sana relaxation ya Kiba lakini Kiba akirudisha nguvy japo kwa 50%, Harmonize atabaki kushindana na akina Rayvanny!

Rayvanny yupo Maili 100 mbali mno
 
Nimeamini kuna watu wanaweza kukuchukia na hujawafanyia lolote baya,

Harmonize
1. Aliutekeleza mkataba wake WCB vizuri
2. Waliposhindwana wakamalizana vizuri na wcb wakavuta pesa waliyokuwa wanaitaka (600M)

Choko choko za nini sasa?mtu ana demand respect kwa mtu ambaye alitaka kumuangusha??? Naamini mmoja wenu hapa ndiye angekuwa Harmonize uvuliwe milioni 600 si ajabu hata mngekuwa mmeshamloga Diamond kafia mbali
 
Rayvanny yupo Maili 100 mbali mno
Hilo nalifahamu fika...

Tangu enzi Harmonize yupo Wasafi, nilikuwa namkubali Rayvann mara 100 kumlinganisha na Harmonize

Na kilichokuwa kinanikera zaidi kuhusu Harmonize ni ile kuiga kila kitu toka kwa Diamond.... yaani alikuwa Clone ya Diamond; hakuwa unique kama Rayvann ambae hata kama umepiga mtungi na kuzima, ukisikia ngoma mpya ya Rayvann utajua tu huyo ni Rayvann!!
 
Pale ambapo mziki unagoma, na kuamua kuzigeukia kiki....
Hakuna shughuli hapo

Harmonize inabidi atoe respect kwa mtu aliyemuokota baada ya kuambiwa na BSS kuwa hajui kuimba ila Diamond akaamini kipaji chake na kumsaidia kufika alipofika leo hii

Huyo rayvanny mwenyewe alikuwa ameachwa na Madee kwenye ile label yao kwa kuambiwa hajui kitu ila Simba akamchukua na kuamini kipaji chake na leo hii yupo juu

Muangalie Mbosso khan leo hii wenzake wa kundi la Ya moto band wapo wapi na wanafanya nini kwenye industry? Aslay na yule Beka flavour

Tuje tumsuguse Zuchu right now, one of the top female artist in East and Central Africa

Ooooh!, This Dude Simba need appreciation kwa kutengeneza wasanii wakubwa ambao wanaweza kufanya competition na yy mwenyewe coz label nyingi hapa bongo wameshindwa kufanya ambacho amekifanya yy

Pia wakumbuke ile music label yake sio kwa ajili ya social charity Ila ipo for profit gain
 
Sijasikiliza hata nyimbo zake....ndo kile kiingereza cha ago kill u??? Akankill ma self???
Kaongeza misamiati siku hizi kuna matusi , huu ndio wimbo wake wa kwanza kwenye album katoa video juzi juzi, haueleweki anaimba nini, hapo kwenye sleep sleep nafikiri alimaanisha halali lali, hiyo outside sijui ndio ametoka😆

"Yeah hustle everyday I never sleep sleep coz am outside
When am falling love I go deep deep coz am outsidee
Time for the money two for the show enzi za kuuza maji na wanangu wa kariakoo
That was before long time ago I wish you know I wish you know yeaah
"

Chorus:
"We are outside outside outside outside
B*tch am outside outside outside outside
Am outside outside outside (Eeeh)
Kondegang we are outside outside outside (Yah yah yah)
"
 
Hakuna shughuli hapo

Harmonize inabidi atoe respect kwa mtu aliyemuokota baada ya kuambiwa na BSS kuwa hajui kuimba ila Diamond akaamini kipaji chake na kumsaidia kufika alipofika leo hii

Huyo rayvanny mwenyewe alikuwa ameachwa na Madee kwenye ile label yao kwa kuambiwa hajui kitu ila Simba akamchukua na kuamini kipaji chake na leo hii yupo juu

Muangalie Mbosso khan leo hii wenzake wa kundi la Ya moto band wapo wapi na wanafanya nini kwenye industry? Aslay na yule Beka flavour

Tuje tumsuguse Zuchu right now, one of the top female artist in East and Central Africa

Ooooh!, This Dude Simba need appreciation kwa kutengeneza wasanii wakubwa ambao wanaweza kufanya competition na yy mwenyewe coz label nyingi hapa bongo wameshindwa kufanya ambacho amekifanya yy

Pia wakumbuke ile music label yake sio kwa ajili ya social charity Ila ipo for profit gain
Summer Walker ni msanii mkubwa tu Marekani kwa sasa kwenye mkataba wake kapewa advance ya $110,000, kwenye mauzo ya album kwa kila $1 atakayotengeneza yeye atapewa 16 cents baada ya kuirudisha advance aliyopewa. Record labels hazina huruma, ndio soko la kibepari hapo penyewe bongo bado mziki unapelekwa kishikaji na kibinadamu sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom