Harmonize kwa mbwembwe hizi!

Lihakanga

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
4,829
6,376
Mara nyingi na kwa tabia za binadamu tulio wengi, kila mambo yanapotuendea vema tunaongeza au kubadili namna zetu za kuishi. Si kosa wala vibaya. Lakini huwa nahofia sana ikitokea kushuka kwa kipato ambako hulazimisha kushuka kwa viwango vya namna za kuishi.

Harmonize anakufuru. Ana ulinzi wa sifa au mbwembwe. Kwa kipi hadi alindwe na walinzi wanne kwa wakati mmoja? Nadhani hawezi kumzidi platnumz kwa umaarufu na nguvu za uchumi, lakini platnumz hana ulinzi kiasi kile.

Nakumbuka tu mbwembwe za Mr Nice, na yaliyoendelea baadaye. Kutoka gari hadi kutembea kwa miguu na kuombaomba vijisenti.

Kwa ujumla tusikufuru kwa kuwa tumefanikiwa, tusijekuumbuka tukishuka.
 
Halafu ni ushamba wa hali ya juu.

Anafanya shoo ulinzi unambana na kumkimbiza kimbiza mpaka huwa nashangaa , why muda wa kazi ulinzi usikae pembeni?

Anaenda msibani kwanini hao walinzi asiwaache huko kwenye gari. Anaingia nao kwa mbwembwe hadi kwenye maombolezo.
Kiukweli ni kama kazuzuka mno.
 
Wabongo bwana..
Mtu akiwa hana pesa mnasema , akiwa nazo mnasema .asipotumia mtasema ,akitumia mnasema.

Tufanye vitu viwe simple... tafuta pesa yako kodi walinzi uwaache kwenye magari... muache huyo mayonaiza afanya anavyotaka na pesa yake...

Kupanga matumizi ya pesa usiyoitafuta ndio ushamba wenyewe
 
Mara nyingi na kwa tabia za binadamu tulio wengi, kila mambo yanapotuendea vema tunaongeza au kubadili namna zetu za kuishi. Si kosa wala vibaya. Lakini huwa nahofia sana ikitokea kushuka kwa kipato ambako hulazimisha kushuka kwa viwango vya namna za kuishi.

Harmonize anakufuru. Ana ulinzi wa sifa au mbwembwe. Kwa kipi hadi alindwe na walinzi wanne kwa wakati mmoja? Nadhani hawezi kumzidi platnumz kwa umaarufu na nguvu za uchumi, lakini platnumz hana ulinzi kiasi kile.

Nakumbuka tu mbwembwe za Mr Nice, na yaliyoendelea baadaye. Kutoka gari hadi kutembea kwa miguu na kuombaomba vijisenti.

Kwa ujumla tusikufuru kwa kuwa tumefanikiwa, tusijekuumbuka tukishuka.
kila mtu aishi maisha yake.
 
Back
Top Bottom