Harmonize anahamasisha matumizi ya madawa ya kulevya kwenye nyimbo zake. Serikali hamlioni hili?

Harmonize ametoa wimbo unaohamasisha matumizi ya bange lakini cha ajabu mpaka sasa serikali bado haijamchukulia hatua zozote za kinidhamu.

Huyu jamaa ulimbukeni na ushamba vinampeleka puta sana, hayo mambo ya mabangi yake angebaki nayo huko huko lakini si kuja kututangazia upumbavu wake.
Wanasubiri atoe Diamond ndo wafunge. Harmo kaimba pambio mbona
 
Jipige do** kisha sema kwa nguvu kwamba wewe mleta mada ni Upinde wa Mvua
 
Si yeye tu, kariba ya wasanii wote wanaimba mambo ya kuhamasisha maovu na machafu... asipodhihirika kwenye sauti utampata kwenye video ukimkosa kwenye video utamshika kwenye jina utampata kwenye maudhui na kama ukimkosa kwenye vyote utampata kwenye lifestyle mfano chakula, mavazi, lugha, hobby, na kadhalika

ngalia orodha

"Nikishalewa sitaki nighasiwe..."

"Bora/acha nilewe..."

"Je watakubali... kula kwangu hadi nikimbizwe..."

"Raha nikikuta simba wanacheza... nitakula jicho..."

"Mimi ndo rafiki wa Lucifer utaniambia nini?..."

"Shetani mwenyewe akiniona anatoka mkuku..."

"Man down..."

"Masikini jeuri..."

"Kasimama dede..."

"Mbona hutokei..."

"Mitungi mikasi"

"Sukari..."

"Kamatia chini..."

"Mwagia ndani..."

Orodha ni ndefu lakini kiujumla hawa wasanii ukiangalia vizuri vaa yao ongea yao na kazi wanazofanya ndo utagundua kwanini wajanja wanakwambia MZIKI DHAMBI
Utaskia " kanipa kisamvu kipapatio nyama ya njiwa"
Mara "chomeka chomoa mwenzako nawashwaa"
Mara njoo nikupe mhogo ukaugulie chumbani

Weka mate niteleze kama nyoka pangoni

Nashukuru Mungu siangalii tv mana nyimbo ukiziskia tu ni aibu
 
Mengine yoote sawa ila jamani mmea wangeuacha tu maana ni unstopable, rejea Adam mwenyewe pale Bustanini jani alilikuta na alikuwa akiburudika nalo maana ni kitu Natural, hakijapitia maabara kile.
 
Koh Koh yeeoow yeeoow wakat wanagombea kitii🎶🎶 mi jicho liko nyanya nishakula kijitiii🎵🎶
 
Mr Kusaya ameishatoa tangazo waache kutaja hizo habari za madawa kwenye nyimbo. Wakikaza ubongo, Kusaya show zake ni speed ya mwanga ataruka nao wote kimya kimya
 
Harmonize ametoa wimbo unaohamasisha matumizi ya bange lakini cha ajabu mpaka sasa serikali bado haijamchukulia hatua zozote za kinidhamu.

Huyu jamaa ulimbukeni na ushamba vinampeleka puta sana, hayo mambo ya mabangi yake angebaki nayo huko huko lakini si kuja kututangazia upumbavu wake.
Hivi mim hua naishi nchi ipi, Mbona hizi nyimbo sijawai zisikia
 
Back
Top Bottom