Harmonize amtumia Diamond Platinumz ujumbe wa mwaka mpya kuhusu umuhimu wa wazazi

Kama vipi waandaliwe mpambano wa ngumi tuone nani mbabe, mambo ya kupigana vijembe wawaachie dada zao
 
Watu wakasome historia ya Tajiri Namba Moja Duniani Jeff Bezos , Baba yake mpaka anakufa alishindwa hta kukutana nae
 
Baba ni baba tu hata asipokua na msaada kwako, huyu Diamond ajitathimini kwani.
 
Hamornize ndio saiz ya diamond, akileta majungu mmakonde nae anarusha yake, ila all in all Harmonize mkali sanaaaaa
Harmonize fix zote za Domo anazijua, si walikuwa wote Pa1 mwanzo, acha wavurushane ipo siku watatoa ya siri ambayo hatukupaswa kuyajua.
 
Diamond anafurahi kumuona Baba yake akiteseka mtaani wakati uwezo wa kumsaidia anao mkubwa sana. Diamond utakufa mapema kabla ya huyo mzee wako mwenye maisha magumu mtaani.
Hamjui Diamond alichokipitia kwa huyo mzee. Alikuwa anakachukulia ka-Diamond kama kachokoraa tu. Mpaka mama yake na huyo mzee ambae ni bibi yake Diamond mzaa baba,alikuwa hataki kumuona Diamond nyumbani kwao. Unaambiwa muda mwingine ilikuwa Diamond aking'aa tu hapo kwa bibi anafukuzwa kama mbwa mbele ya huyo mzee,kwa kuambiwa maneno makali. Inaumiza sana. Piga picha wewe ndio mtoto wa miaka 13 hivi,usie mbele wala nyuma,unaishi na mamako tu kwenye maisha ya uswazi. Siku unaona aaah...! Ngoja nimtokee tu mshua mwenye maisha nafuu,unafika huko unamkuta mshua,lakini unatimuliwa na mamake kama kitoto kichokoraa tu,inaumaje hapo?. Mimi ni mtu wa kusamehe sana ili maisha yaendelee,ila kwa huyo mzee siwezi kusamehe. Kama anaoza miguu,hayo hayo nyie hamjui,ndio malipo anayapata hapa hapa duniani kutokana na matendo yake. Diamond upo mzigo wake ataubeba. Kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe
 
Anatafuta huruma ya wananchi, wimbo mzima anaimba kujuhusu yy aonekane anaonewa.
Alianza kulalamika uko insta "ooh cjui baba Levo nn, wanaingia studio watengeneze nyimbo kunidis"
Ye alipomwimba mwenzake hakujibiwa zaidi ya yy mwenyewe kuanza kujitetea. Sasa leo anataka kutuaminisha kwamba anaonewa.
Aache upumbavu afanye mziki
 
Baba ni baba tu hata asipokua na msaada kwako, huyu Diamond ajitathimini kwani.
Acha mkuu baba hawezi kuwa baba tu tuseme ana kazi na mshahara yeye ni pombe na mademu we ukitoboaa utamuona kama baba
 
Single maza ndo wanajua machungu yake...nyie wengine pigen kimya tu..
Kutelekezewa mtoto inauma saana unaona mtoto anaumwa hlf huna hata shilingi na ukimuambia babake anakujibu kunya au ndo kwanza anampa mwanamke wake akujibu..

Mtoto anakosa ada ukimuomba babaake akusaidie ada hilo jibu lake utatafuta sehem ukaheme ...na siku wanaume mnajijua kuoa single maza ishakua ishu kwahiyo unajikuta unakosa mume na mtoto anakuelemea..

Hlf kishakua inakua rahis tu jamii kusema msamehe baba wakati ule mtoto anateseka hakukua na mtu wa kusema baba mtunze mwanao kwsabu aliyekukosea ni mama siyo mtoto
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom