Harmonize amtumia Diamond Platinumz ujumbe wa mwaka mpya kuhusu umuhimu wa wazazi

Kwa hapa namtetea domo, jamaa kapata alichokitafuta. Unatelekeza mtoto usitegemee malipo mazuri mbeleni.

Domo kasota sana na mama yake, walikonda haooo mpaka mishipa ya shingo unaiona walikua weusi tii. Leo kapata hela jamaa anajitokeza kutaka shea sawa na mama mtu neeehiiii
 
Wasalaam wana jamvi
Msanii Harmonize kupitia wimbo wake mpya wa "WAPO" AMEMTUMIA salamu za Mwaka mpya 2021
Harmonize amemkumbusha Diamond kuhusu umuhimu wa wazazi wote wawili hasa wakiwa hai kabisa.

namnukuu anasema
"Kama baba na mama ndo nguzo ya dunia

Wapende wote
Sio wa kike anacheka wa kiume analialia
Bila msaada wowote"


Wapo Lyrics – Harmonize


(B Boy) Eeh
Mmmh mmh
Hivi kwanini nijitutumue
Na dunia sio makazi
Vijineno neno vinisumbue
Hadi nishindwe kazi
Mama alisema mkuku kwa nguruwe
Kuishi na watu kazi
Achambe atukane ata aniue
Nishasamehe mzani ni mzazi


Kifupi nafunika kombe
Nikiamini kesho nayo siku
Mapicha picha mapicha
Sidhani kama nitapona
Wanangu wa mtaani mniombee
Hii vita ni mchana na usiku
Oooh kuna watu na viatu
Wanatamani milele wawe wao
Ukijituma watasema
Unashinda nao


Oooh ni kama watu kumbe
Ndani wana roho za chatu
Hawatosheki na vikubwa vyao
Wanatamani hata kidogo chako kiwe chao
Mola nipe ujasiri
Kwenye kufanya maamuzi
Zidi nikomaza akili
Isinipoteze miluzi
Uniamshe alfajiri
Kama jana na juzi
Kupata kukosa ni siri
Nawe ndo Mungu baba mwamuzi
Dear Lord, wapo
Iyeiye iye, wapo
Japo ni ngumu kuwaona, wapo
Wapo wasotaka ufanikiwe
Binadamu hawana jeru, wapo
Kila utachofanya watasema, wapo


Watakuita mwanga kibonge
Tena kwa dharau wakucheke
Wanachotaka we uongee
Waseme shukrani ya punda mateke
Kama vipi dem wake tumgongee
Ndiye anayempiga chura teke
Usipoonewa ndonge
Basi ndo ujue hauna makeke
Sikia Konde kwepa bana mjini shule
Ukipata kidogo leta na nao tule
Wachana nao wamesemaga umezoea vya bure
Maana siku zote nyani halioni kundule

Kama baba na mama ndo nguzo ya dunia

Wapende wote
Sio wa kike anacheka wa kiume analialia
Bila msaada wowote

Oooh kuna watu na viatu
Wanatamani milele wawe wao
Ukijituma watasema
Unashinda nao
Oooh ni kama watu kumbe
Ndani wana roho za chatu
Hawatosheki na vikubwa vyao
Wanatamani hata kidogo chako kiwe chao
Mola nipe ujasiri
Kwenye kufanya maamuzi
Zidi nikomaza akili
Isinipoteze miluzi


Kupata kukosa ni siri
Nawe ndo Mungu baba mwamuzi
Dear Lord, wapo
Iyeiye iye, wapo
Japo ni ngumu kuwaona, wapo
Wapo wasotaka ufanikiwe
Binadamu hawana jeru, wapo
Kila utachofanya watasema, wapo
Wapo wasotaka ubarikiwe


Dear Lord
“Special message to the Youth”
It’s your time now to follow your dreams
No matter what people say stay humble
Stay positive, follow your dream
Believe in God, ease your mind
Ease your mind for Lord
(The Most Wanted Mix)




wasalaam wana jamvi
Mondi a.k.a Domo anampenda zaidi baba wa kambo anko Shamte labda alimsaidia pesa za kwenda Studio kurekodi sasa analipa labda analipa fadhira
 
Kuzalisha ni raha sio kazi; hata panya anazalisha, kazi ni kulea!!! Kama wakati wa kulea uliingia Chaka halafu unaona mambo yamejipa ndio unajisogeza!!!! Hata Mungu ataona huruma laana yake haikupati!!
Mashabiki wa diamond hebu jichangeni hata jero-jero huyu baba wa star wenu apate matibabu ya upesi kabla hajakatwa miguu.
 
Naona hii video atamtafuta Mzee Abdul rapper, kama alifofanya ktk ushamba kumweka Diamond rapper
 
Kuna kitu mnakosea sana nyie bendera fuata upepo,huyo baba yake asingekuwa na huyo mama yake angezaliwa?
haitoshi mzee, kuna kitu inaitwa bonding, usipokuwa nayo na watoto wako ujue umeshakula hasara.
 
Kwa hapa namtetea domo,jamaa kapata alichokitafuta. Unatelekeza mtoto usitegemee malipo mazuri mbeleni. Domo kasota sana na mama yake,walikonda haooo mpaka mishipa ya shingo unaiona walikua weusi tiiiiiiiii. Leo kapata hela jamaa anajitobankeza kutaka shea sawa na mama mtu neeehiiii
Hivi ikitokea huyu mzee katangulia mbele za haki kweli Diamond na mama yako watakwenda msibani? na akipewa maiki atasema nini?
 
Kutolomba haitoshi mzee, kuna kitu inaitwa bonding, usipokuwa nayo na watoto wako ujue umeshakula hasara.
kwa hyo kwakuwa hakuna bond ndio aachwe ateseke? au anasubiri akifa ndio amuhudumie?
 
Back
Top Bottom