Asha Abdala
JF-Expert Member
- Mar 21, 2007
- 1,130
- 44
Mimi Asha Abdala, nawaomba watanzania wote wenye mapenzi mema muweze kuwachangia wabunge mahiri Dr Slaa na Zitto Kabwe ili waweze kuwa na vijana wa kutosha pale bungeni Dodoma wawasadia katika masuala ya utafiti lakini pia waweze kuzunguka katika mikoa ya jirani na Dodoma wakati wa mapumziko ya wiki katika kipindi hiki cha Bunge kwenda kufikisha ujumbe wao wa mabadiliko kwa wananchi vijijini. Mchango huu ni wazi kwa wanaCHADEMA na watu wote wenye mapenzi mema. Kwa maelezo zaidi wasiliana nami kupitia ashabdala@yahoo.com naweza kupokea michango. Au tuma mchango wako moja kwa moja wa Dr Slaa kupitia 0784666995 au Kwa Zitto 0713730256. Nawaombeni sana jamani, hasa wanawake wenzangu. Lakini wakina Baba vile vile nawahimiza kufanya kazi hii. Kumbukueni wabunge wetu hawa, ofisi ya bunge haijaweza kuajiri watafiti kwa ajili yao zaidi ya mtu mmoja tu anayesaidia wabunge wote 43 wa upinzani. Pia chama chao cha CHADEMA hakina uwezo mkubwa wa kifedha. Shime mwananchi, kama unachangia harusi, kwanini usichangie harakati. Ewe baba, toa fedha yako ya bia ya siku mbili tu, isadiie kuikomboa nchi yetu.
Asha
Asha