Harambee ya wanafunzi hawa iwe changamoto kwa watanzania

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
5,521
2,000
Kupitia utv Habari tumeona harakati na msaada mkubwa walioufanya wanafunzi wa kike wa shule moja iliyoko mikoa ya kaskazini kwa kumchangia mwenzao na kufanikisha kumjengea nyumba baada ya wao kufika kwenye msiba wa baba ya rafiki yao huyo hivyo kuona Nyumba na maisha ya nyumbani kwa mwenzao ambae pia alikua Dada mkuu wa shule.

Wanasimulia kua hali waliyoikuta nyumbani pale iliwasukuma kujiorganize na kuamua kuchanga kumjengea Nyumba kama hatua yao ya mwanzo kwa msaada wao.

Binafsi niwape pongezi nyingi wanafunzi hao laakini pia kwetu watanzania tujifunze kusaidia na kutatua kero zenye msingi kwa jamii tupatapo namna.

Tuachane na tabia ya kupenda kuchangia shughuli za starehe za muda hasa maharusi.tujenge mazoea ya kuchangiana katika elimu na afya pale inapobidi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom