Harambee ya UVCCM yafana, michango yavuka lengo

Paul Makonda

Member
Jul 8, 2011
97
186
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Sadifah Juma Khamis wamefanya fundraising kwa ajili ya kuandaa matembezi ya mshikamano wa miaka 50 ya Mapinduzi.

harambee hiyo ambayo imehudhuriwa na Rais wa Serikali ya Mapinduz ya Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Mhe. Ally Mohamed Shein kama mgeni rasmi akiongozana na Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Mhe. Balozi Seif Alli Iddy.

harambee hiyo ambayo ililenga kukusanya kiasi cha milioni mia moja na hamsini kufanikisha shughuli hiyo inayotarajia kuanza tarehe 22 Dec 2013 mkoani Pemba ilifanikiwa sana kwa kuchangisha zaidi ya milioni mia mbili.

jumuiya hiyo imeshukuru wachangiaji ambao ni viongozi wa serikali, makada wa Chama Cha Mapinduzi na baadhi ya wanachama wa vyama vya upinzan ambao wamevutiwa na wazo la vijana la kuhamasisha mshikamano na Amani., na kwamba wanasikitishwa namatendo yanayofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na wanasiasa hapa nchini vya kubaguana kikanda na kidini.
 
Lowassa katoa ngapi? Na hizo zote ni kwa ajili ya kutembea siku moja tuu au mnaenda kuzifanyia nini?
 
Makonda bwana .Sasa JF watakusaidia nini na mambo yako haya ? CCM ina wenyewe kwani hakuna mtandao wenu wa kuelezana mambo yenu ?
 
...

jumuiya hiyo imeshukuru wachangiaji ambao ni viongozi wa serikali, makada wa Chama Cha Mapinduzi ....

Mkuu una taarifa Mwenyekiti wenu (rtd) Mkoa wa Mwanza na Diwani wa CCM Kata ya Kisesa kauwawa KWA MAWE na wananchi wenye hasira kali kwa kupora haki za wananchi? Nadhani hili ndio la muhimu zaidi kuliko hayo maigizo yenu ya "michango yavuka lengo" ilhali michango yenyewe ni fedha za wananchi walizodhulumiwa kwa njia mbalimbali - rushwa, wizi, ufisadi, n.k.
 
Huyu si Kambi ya Makonda.Makonda yeye ni Sitta na Mwakyembe .Mabina alikuwa kwa Membe .Membe ndiye kapata pigo .
 
Mkuu Pmakonda;

Fikiria jitu lenye sifa hizo hapo chini linapewa uenyekiti wa CCM wa Mkoa and funny enough linapitishwa na chama kwa nafasi ya udiwani ambapo lilifanikiwa kuwa Diwa wa Kisesa. Halafu "jambazi" kama hilo "likikichangia" chama chenu mnatuletea maigizo ya "michango yavuka lengo" hapa!

Clement Mabina:

- Alikuwa miongoni mwa watu ambao wamejijengea umaarufu mkubwa sana katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa hususani ndani ya ziwa Victoria!

- Ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wakituhumiwa na ujambazi wa kutumia silaha hasa katika miaka ya 90!

- Ni miongoni mwa watu ambao wanadaiwa kuua wavuvi ndani ya Ziwa Victoria na kuwapora fedha na mali zao nyingine!

- Ni miongoni mwa watu wanaodaiwa kufanya mauaji ndani ya Ziwa yeye na wenzake kadhaa akiwemo DC na Diwani Mmoja!

- Kifo chake pengine ni malipo ya mauaji aliyokuwa akifanya dhidi ya raia wasiokuwa na hatia.

- Ni mtu ambaye alikuwa anaogopwa hadi na maofisa wa Jeshi la Polisi, alitumia vibaya sana madaraka yake ya uenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza!

- Alijaribu kupigana sana kwenye uchaguzi wa CCM mkoa mwaka huu, na ni miongoni mwa mambo yaliyomfanya achanganyikiwe!
 
Mkuu Pmakonda;

Fikiria jitu lenye sifa hizo hapo chini linapewa uenyekiti wa CCM wa Mkoa and funny enough linapitishwa na chama kwa nafasi ya udiwani ambapo lilifanikiwa kuwa Diwa wa Kisesa. Halafu "jambazi" kama hilo "likikichangia" chama chenu mnatuletea maigizo ya "michango yavuka lengo" hapa!

hi thread uliyo iatach inatisha mkuu!
 
hi thread uliyo iatach inatisha mkuu!

Kweli kabisa Mkuu; ndio CCM hao. Ufisadi kila kona halafu wanatuletea hadithi za "michango yavuka lengo"; so what?

Upuuzi kama huu alioposti muanzisha mada unamsaidia nini mwananchi wa kawaida? Unamsaidia nini mnyonge asiye na mtetezi nchi hii?

Wananchi wanataka kusikia madhulumati kama akina Mabina wamechukuliwa hatua gani na sio kuyaacha mitaani yakitamba huku yakipewa vyeo na chama.

Wananchi wanataka kuona akina Kapuya wanachukuliwa hatua, na sio kuachwa wakitoa vitisho kwa mayatima tena mbaya zaidi baada ya "kuwabaka".

Anyway, nilicho-attach sio maneno yangu bali ni ushuhuda ulipopatikana kutoka uzi huu https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/569527-aliyekuwa-mwenyekiti-wa-ccm-mkoa-wa-mwanza-auwawa-na-wananchi-wenye-hasira-kali-kwa-kupigwa-mawe.html
 
Ni fedheha sana kwa mtu aliyemtuhumu Mwenyekiti wake aliyeshinda uchaguzi kwa rushwa kukubali kuteuliwa na kuwa katibu wa mapambio chini ya uongozi wa mtoa rushwa kwenye chaguzi.

Na wewe ni miongoni mwa wapambanaji wa ufisadi?
 
yahaya vp hatuonan?unaishi nyumba namba ngapi
 
Ni fedheha sana kwa mtu aliyemtuhumu Mwenyekiti wake aliyeshinda uchaguzi kwa rushwa kukubali kuteuliwa na kuwa katibu wa mapambio chini ya uongozi wa mtoa rushwa kwenye chaguzi.

Na wewe ni miongoni mwa wapambanaji wa ufisadi?
Daah
 
Back
Top Bottom