Harakati za wanawake zimeishia kwenye sakata la 'Babu Seya'

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,297
12,597
Juhudi haishindani na kudra.

Msamaha wa akina babu Seya umetia maji na doa harakati za vikundi vya wanawake kupambana na uonevu mkubwa dhidi ya watoto wa kike. Nia ya kuwasamehe ni nzuri sana lakini haikuzingatia maslahi mapana ya mtoto wa kike.

Lakini pia ni kengele kwa mhili wa sheria kutoa hukumu zisizoacha mashaka na kuigawa jamii kama ilivyotokea kwenye hukumu ya babu seya.

Jamii inafahamu ukweli wa mambo yanayotokea kwenye jamii yao kuliko mahakama, hivyo hukumu zenu lazima zifanane na kinachofahamika kwenye jamii na wanajamii wenyewe.

Kulikuwa na mgawanyiko mkubwa kati ya hukumu na jamii inachokifahamu hivyo kusababisha mgawanyiko.
 
Hili jambo la kuwaachia huru limefanyika kisiasa japo na EL nalo alilizungumzia kisiasa 2015.

Sasa huyu JPM ameonesha dhahiri kumkoa EL.
 
Hakuna sababu ya kuwafukuza Mashuleni Mabinti wanao beba Ujauzito.

Kubwa, Serikali iwajengee Shule maalumu.
 
Ktk nchi za Kiafrika,siasa huathiri kila kitu mpaka mfumo wa maisha!
Siyo nchi za kiafrika ni dunia nzima siasa inaathiri mfumo wa maisha.

Bunge la Marekani lilivyopitisha sera ya Obama care waliathiri maisha ya watu.

Bunge la S. Africa lilivyopitisha sheria ya kuruhusu ndoa za jinsia moja waliathiri maisha ya watu.

Bunge la Tanzania lilivyopitisha sheria ya makosa ya mtandao wameathiri maisha ya watu.

Raia wa Kenya walivyomchagua Uhuru waliamua nani awaathiri kwa maamuzi yake.
 
Juhudi haishindani na kudra.

Msamaha wa akina babu Seya umetia maji na doa harakati za vikundi vya wanawake kupambana na uonevu mkubwa dhidi ya watoto wa kike. Nia ya kuwasamehe ni nzuri sana lakini haikuzingatia maslahi mapana ya mtoto wa kike. Lakini pia ni kengele kwa mhili wa sheria kutoa hukumu zisizoacha mashaka na kuigawa jamii kama ilivyotokea kwenye hukumu ya babu seya.
Jamii inafahamu ukweli wa mambo yanayotokea kwenye jamii yao kuliko mahakama, hivyo hukumu zenu lazima zifanane na kinachofahamika kwenye jamii na wanajamii wenyewe. Kulikuwa na mgawanyiko mkubwa kati ya hukumu na jamii inachokifahamu hivyo kusababisha mgawanyiko.
Wazo langu wale waliosamehewa wasingekubaliwa kwenda Ikulu na pia wasingerudi kwenye muziki wa jinsi hiyo tena. Wangetulia kimya katika jamii wafanye shughuli zao za kawaida kimya. Miaka iliyopita Bw. Fischer aliyekuwa mdunguaji mkuu wa BOSS ya Afrika Kusini enzi hizo alisamehewa katika ule mpango wa Ukweli na Upatanisho baada ya sera za ubaguzi kufutwa nchini humo. Fischer alienda kwa jamaa za wahanga wake wengi na kuomba radhi. Mwaka 2006 huyo bwana alionekana katika karakana moja ya kituo cha kikristo Durban akifanya kazi za kujitolea kama toba. Wananchi walimwelewa. Ukisamehewa kwa makosa ya jinsi hiyo na kutolewa jela unahitaji ushaurj mzuri sana ili usipotoshe dhana njema ya kusamehewa huko. Usiendeleze ustaa wako bali ishi maisha ya kimya kimya. Maisha ya mtu aliyetubu.
 
Mwenyekiti wa UWT hana kauli kwa bwana yule aliyewakmbatia wabakaji.
Hahahaha mkuu mbona hata yule mgombea wenu alitia nia kuwa acha huru hao wabakaji? au kwa sababu kafanya mwingine ndio imekuwa nongwa?
 
Back
Top Bottom