Harakati za Takukuru dhidi ya CCM: Zina udhati au ni changa la machoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Harakati za Takukuru dhidi ya CCM: Zina udhati au ni changa la machoni?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Jul 29, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Hii kamata kamata inayoendeshwa na Takukuru hivi sasa za wagombea wa CCM watoa rushwa zina udhati wowote katika kukabiliana na ufisadi uliokithiri ndani ya chama hicho au ni changa tu la macho tunalotupiwa sisi wananchi na taasisi hiyo?

  Binafsi, naona ni changa tu la machoni – la kumsaidia JK aonekane anaushughulikia uozo huo kabla ya uchaguzi. Sasa hivi tutasikia sifa kwa JK kwamba kawashughulikia watoa rushwa katika chama chake, ingawa naamini kabisa mwisho wa siku, hakuna chochote kitakachotokea – kwa maana ya wahusika kupelekwa mahakamani na kuiingia jela.

  Aidha pamoja na uchafu wote huu unaofichuliwa, baadaye CCM itajigamba na kusema “Ingekuwa siyo Takukuru, mafisadi wangejipenyeza katika uteuzi” majigambo ambayo ni upuuzi kama nitakavyoeleza hapa chini:

  Mfano mzuri ni wa yule Mama DC wa Kasulu. Pamoja na kukamatwa kwake, bado aliruhusiwa kuendelea kugombea na hatimaye kuwashinda wenziwe, kwa maelezo yaliyotolewa na viongozi wa CCM kuwa hizo zilikuwa “ni tuhuma tu, zisizothibitishwa”.

  Kama mpango ni huu, basi Takukuru wanafanya kazi ya bure tu – yaani wanamkamata mgombea kwa tuhuma za kutoarushwa halafu anaachiliwa kuendelea kugombea! Kwa mfano mgombea huyu akipitishwa na vikao vya juu vya CCM na kuwa Mbunge – Takukuru hawawezi tena kuleta fyoko – ndiyo iatkuwa imepita hiyo! It’s all nonsense!

  Pili, Hosea naye ana ajenda yake dhidi ya baadhi ya Wabunge waliokuwa mstari wa mbele kutaka ang’olewe kutokana na husika yake ya kashfa ya Richmond. Inawezekana sasa anaona amepata “another axe to grind” baada ya ile ya kuwahoji kuhusu double allowance kushindikana.

  Tatu, jee harakati hizi za Takukuru dhidi ya watoa rushwa katika teuzi ndani ya CCM, wanaweza kuzirudia katika kampeni za uchaguzi wenyewe? Mimi nadhani hawana ubavu wa kuziendeleza harakati hizi hadi huko – kwani wakifanya hivyo kuna Wagombea Ubunge wa CCM wengi tu wanaweza wakapoteza sifa za kuwania nafasi hiyo!
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ni kweli wanatoa rushwa na tunawashukuru TAKUKURU kwa kuifunua ngua ccm mbele ya jamii.
  Ingawa mafisadi wanafight back lakini ndani ya chaguzi za CCM rushwa za kila aina hutolewa.

  TAKUKURU watakamata rushwa zoooote kasoro ile ya NGONO sidhani kama kuna atakayekamatwa ingawa bado akina mama zetu wanajitoa sana hata miili yao ili wateuliwe na kuchaguliwa....
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuu Zak: Mimi nadhani harakati zote hizi za Takukuru hazitakuwa na tija yoyote kwa taifa, achilia mbali katika CCM -- iwapo watuhumiwa hawataadhibiwa kufuatana na sheria zilizopo!
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nadhani hujamuelewa sawasawa mtoa mada. Mada ni kwamba kamata-kamata bila ya kufikisha watuhumiwa mahakamani ni changa la machoni tu!
   
 5. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  hii yote ni DANGANYA TOTO hakuna kitakacho fanyika wala hatua zozote zitakzo chukuliwa kwa wagombea wote wa CCM ila ingekuwa ni vyama vya upinzani haraka sana wangepelekwa mahakamani
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Takukuru ndo mashuhuri kwa kupokea rushwa iweje wakamate rushwa? Hii yote inayo fanyika ni kwa maskini wasio na pesa za kuwapa hao takukuru.
   
Loading...