Harakati za Mapenzi zilivyompeleka jela rafiki yangu

willpower

JF-Expert Member
Dec 3, 2019
404
2,271
Wasalaam; hii ilitokea,

Nakumbuka miaka ile, tukiwa tumehitimu kidato cha sita, mtaani kwetu tulikuwa vijana 6 ambao tulikuwa tumehitimu elimu ya sekondari.

Miaka ile utaratibu wa kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu ilikuwa unasubiri mwaka mzima nyumbani. Utamaliza kidato cha sita mwezi wa tano mwaka huu ila chuo ni mwakani mwezi 9-10 hapo.

Sasa kijana mwenzetu mmoja hapa nitamwita William, akawa ameanzisha mahusiano na binti mmoja hapo mtaani kwetu na kwa kweli mapenzi yao yalikuwa yamenoga haswa. Binti alikuwa anaishi kwa dada yake ambaye alikuwa na cheo kwenye shirika moja la umma, humo waliishi na binti mwingine ambaye alikuwa akisoma shule ya msingi darasa la nne.

Williama akafanikiwa kumpata huyu Binti mrembo na anayevutia haswa na kwa kweli hata sisi rafiki zake tuliona jamaa anafaidi.

Lakini pia maisha ya kwao na huyu binti yalikuwa mazuri sana, nyumba kubwa ndani ya uzio na miaka ile dada alikuwa ana magari kadhaa. Kwa miaka ile alionekana kuwa wana hela pale mtaani.

Wakati huo sisi wengine tulikuwa tunahangaika na akina Chausiku, watoto wa uswahilini wenzetu.

Ilikuwa ni utaratibu wa William na huyu binti kushinda wote ndani (kwao na huyu binti)maaa dada yake alikuwa anatoka asubuhi na kurudi usiku kwa sababu ya majukumu ya kikazi. Kwahiyo mara nyingi Williama alikuwa akishinda ndani ya hii nyumba na mpenzi wake.

Siku ya tukio; likizo fupi ya shule za msingi na sekondari ; sisi watoto wa uswahili tukiwa tunaelekea uwanjani kuangalia mpira tukapishana na William akiwa anafunguliwa geti na mpenzi wake, akatusalimu nasi tukamsalimu huku tukiendelea na safari; ila mazungumzo yalikuwa ni jinsi William anavyofaidi; maana wote tulikubali pale mtaani kuwa yule mpenzi wake alikuwa mzuri na anayevutia lakini zaidi anatoka kwenye familia bora (hapa ilikuwa tunakumbuka mashairi ya Mtoto wa Geti Kali - Inspector Haroon).

Tukiwa tunarudi majira ya saa moja hivi , ndipo tunakuta gari ya polisi (wakati ule zilikuwa zile Defender nyeupe) ilikuwa imepaki nje ya ile nyumba huku polisi kadhaa wakiwa wamesimama; lakini alikuwepo baba yake na William pamoja na mama yake; tulipokaribia ndipo nikasikia sauti ya mama William ''mwanangu hawezi kufanya hivyo, huyo mtoto aulizwe vizuri''.

Kilichotokea ni kwamba mama mwenye nyumba aliporudi jioni ile inasemekana kuwa katika utaratibu wa kumkagua binti yake(yule mtoto wa shule ya msingi) akagundua kuwa ameingiliwa maana alikuwa na majeraha sehemu za siri. Na yule mtoto alipoulizwa akasema kuwa aliyefanya hivyo ni William. Mama kwa nafasi yake akaita Polisi ambao walikuja na kumchukua William.

Hii ikawa stori pale mtaani kwamba William amebaka; kwa sisi tulikuwa tunamjua William ikawa ngumu kuamini; wengine pale mtaani wakaamini.

Binafsi nilipata nafasi wiki kadhaa baada ya tukio kuzungumza na aliyekuwa mpenzi wa William; kitu alichoniambia kuwa William hakumwingilia yule mtoto wa dada yake; nikauliza ilikuwaje mtoto akamtaja William? akanijibu kuwa baada ya dada yake kugundua kuwa mtoto wake ameingiliwa; swali alilomuuliza mtoto ni kuwa ''ulikuwa na nani? Mtoto akajibu ''William''.

Kwa kuwa William ndio alikuwa nyumbani muda wa mchana mpaka jioni ya siku ile.

William akawekwa mahabusu akisubiri upelelezi na masuala mengine; wiki na miezi ikapita. Akawekwa mahabusu katika jela moja hapa mjini; sisi kama marafiki tulichoweza kufanya ni kwenda kumuona mara kadhaa.

Muda ukaenda sisi wengine tukaendelea na masuala ya kuomba nafasi kwenye vyuo vikuu vya serikali.

Tukaanza na kusoma kabisa, William akiwa anashikiliwa mahabusu kama mbakaji maana kesi ilikuwa haijafikia tamati.

Miaka miwili baadaye William aliachiwa huru. Familia ya William ilihama kabisa hapa mjini.
 
Tuli kimbia fedheha ndugu yangu ila shukrani kwa mikate mlio niletea pangoni .maisha yana endelea uku tulipo
 
Aisee 🤔
Baada ya kutoka ikawaje? Aliendelea na shule ? Na huyo dada je? Na sshv Yuko wapi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom