Harakati za Kumng'oa James Mbatia ktk NCCR-Mageuzi zakolea

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,942
428
Shinikizo la mkakati wa kumng'oa mwenyekiti wa NCCR -Mageuzi James Mbatia'' limeiva '' baada ya makada wa chama hicho 'kushikilia' bango msimamo wao wa kutaka Mbatia kujiuzulu pasipo shuruti

Safari hii makada hao wakiongozwa na Kamishna wa NCCR-Mageuzi mkoa wa Tanga Mbwana Hassan ,wameueleza kinagaubaga uongozi wa chama hicho Taifa Kuhusu msimamo wao wa kumtaka Mbatia kujiuzulu nafasi hiyo katika chama kwa hiari yake

Msimamo huo wameuweka wazi kupipia barua ya Sept 5 2011 waloyomwandikia katibu mkuu wa chama hicho Samuel Ruhuza. Mbwana katika barua hiyo ya kurasa tatu anamtaka mbatia kujiuzulu kwa madai kwamba amepoteza uhalali wa kuwa mwenyekiti wa chama Taifa. Anasema vikao vimeshafanyika kumwomba Mbatia na kumshauri ajiuzulu .Anasema kipindi walichokutana na mbatia Ruhuza hakuwapo alikuwa mkoani Kigoma.Anasema walikutana kwenye kikao cha pamoja Bagamoyo naviongozi wakuu wa chama isipokuwa Ruhuza

Mbwana anasema kinachomponza mbatia ni matamko yake mwenyewe na jinsi ambavyo amekuwa akishindwa mfululizo katika chaguzi za ubunge majimbo aliyopata kugombea Nchini ''labda nikikumbushe tu kuwa huyu mwenyekiti ndiye ,ambaye amekifikisha chama mahala kinawatatiza wananchi kutokana na misimamo yake ya kuwa wakili au mtetezi wa CCM na mafisadi'' Anasema mbwana akijibu barua aliyoandikiwa na Ruhuza

Kwa mfano anasema wakati katibu mkuu wa CHADEMA Dr Slaa na Mbunge wa singida mashariki (CHADEMA) Tundu Lissu walipotangaza orodha ya mafisadi mwaka 2007 Mbatia aliibuka na tamko kuwa watanzania wote ni mafisadi isipokuwa wanatofautiana tu viwango vya ufisadi ''Huu ni ushaidi wa kutetea mafisadi wa CCM kwa kutaka kupunguza hasira za wananchi dhidi ya mafisadi'' Anasema Mbwana Katika barua hiyo pia anasema mwaka 2010 chama cha wananchi (CUF) kilikataa kumtambua Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume,kufuatia uchaguzu uliotangazwa duniani kote kuwa haukuwa huru na wa haki,lakini Mbatia aliibuka na tamko kuwa kitendo cha CUF kutomtambua Karume kilikuwa ni uhaini' ''Hii inadhiirisha kuwa mtu huyu alikuwa anafanya kazi ya kutetea Ushindi wa CCM'' Anasema Mbwana.Anadai kwenye kikao kimojawapo cha Halmashauri kuu ya Taifa (NEC) ya NCCR- Mageuzi,aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu wa 2010 Hashim Rungwe ,alikijulisha kikao hicho kuwa wakati wa kampeni ,Mbatia alimkataza kuisema vibaya CCM anapohutubia mikutano katika jimbo la kawe

Rungwe ambaye ni mwanasheria maarufu Nchini,alithibitisha madai hayo ya Mbwana Alipohojiwa na Nipashe ''Huu ni ushaidi mwingine wa namna Mwenyekiti (Mbatia) anavyofanya kazi ya CCM ,anadai Mbwana. Mbatia aliwania ubunge kupitia NCCR -Mageuzi katika uchaguzi mkuu jimbo la kawe akaangushwa na aliyegombea kiti hicho kwa tiketi ya CHADEMA ,Halima Mdee.

Mbwana anasema hivi karibuni Mbatia pia alikaririwa na vyombo vya habari akiunga mkono mtazamo wa CCM kuwa wabunge vijana ni tatizo bungeni ,hawaelewi walichotumwa na wananchi na kwamba inaonyesha hawakuandaliwa kuwa viongozi.

''Kwa mantiki hizo zote ,naendelea kusimamia Msimamo wangu kwamba ,kwa busara za kawaida ,tena pasipo shuruti ,James Mbatia angejiuzulu.Kwani amepoteza uhalali wa kuwa mwenyekiti wa chama Taifa kwa matamko yake mwenyewe ,lakini zaidi kwa namna anavyoshindwa mfululizo katika chaguzi za ubunge.

Kila jimbo ambalo aligombea ,watu walikuwa na imani na upinzani lakini hawakuwa na Imani na James Mbatia.Ndio sababu walichagua TLP vunjo mwaka 2000 na CHADEMA kawe 2010.Katika uchaguzi wa kawe ,Mbatia hakutoa ushindani mkubwa ,badala yake alishindwa kwa tofauti ya kura 33,000 na Mdee

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana ,wenyeviti wanne wa vyama vya upinzani John Cheyo (UDP, Augustine Mrema (TLP) Freeman Mbowe (CHADEMA) ,Waligombea ubunge lakini ni Mbatia peke yake ndiye aliyeshindwa Uchaguzi.

Mbwana anasema uamuzi wa kufungua kesi dhidi ya mpinzani mwenzake katika jimbo la kawe ,unakinzana na misingi ya maamuzi ya chamakukataa kuweka mgombea katika jimbo la Igunga ili kuongeza idadi ya wabunge wa upinzani Bungeni
 
Fukuzeni huyo kibaraka atawaaribia chama.kwanza mnatakiwa kuanza kuhoji mali zake kazipata wapi kama si kuongwa na magamba?
 
Mbatia,Ni kosa kubwa sana kuwa na VIONGOZI toka KIGOMA,kwa mtazamo wangu na jinsi ambavyo nimepata kuwaona watu wakigoma,ZITO,KAFULILA,RUHUZA,KAKOBE,MKUU WA CHUO CHA USTAWI hawa ni watu wa KIGOMA,,,kama hawashika nyadhifa watakuangusha tuu sababu ni watu wa madaraka zaidi..,Wakipata lazima watang'ang'ania.Sijagusa utendaji wao...nimegusia tabia zao....Kwa matazamo huu tayari MBATIA alishavuliwa uenyekiti tangu waliposhinda viti vya ubunge KIGOMA,na chanzo cha mgogoro utakuta kimeanzia kigoma HUKO TANGA zubaisha nbwege tuu.
 
Mbatia aondoke aende ccm, si mpinzani kabisa huyo. kama vipi wamfukuze kama mbwa.
 
Mbatia,Ni kosa kubwa sana kuwa na VIONGOZI toka KIGOMA,kwa mtazamo wangu na jinsi ambavyo nimepata kuwaona watu wakigoma,ZITO,KAFULILA,RUHUZA,KAKOBE,MKUU WA CHUO CHA USTAWI hawa ni watu wa KIGOMA,,,kama hawashika nyadhifa watakuangusha tuu sababu ni watu wa madaraka zaidi..,Wakipata lazima watang'ang'ania.Sijagusa utendaji wao...nimegusia tabia zao....Kwa matazamo huu tayari MBATIA alishavuliwa uenyekiti tangu waliposhinda viti vya ubunge KIGOMA,na chanzo cha mgogoro utakuta kimeanzia kigoma HUKO TANGA zubaisha nbwege tuu.
<br />
<br />acha ukabila bwana mdogo erick !mbona nyie watu wa magamba mnapenda sana kutugawa watz?
Badala ya kujenga hoja ya mtoa hoja unakimbilia kwenye ukabila .kwani mlalamikaji kuna sehemu kaongelea ukabila hapo?kama huna cha kuchangia si ukae kimya? Umekimbia fb umekuja huku jf umekosea bora ungebaki hukohuko fb maana huku lazima uwe great thinker si poyoyo wa kufikiria.nyambaf zako
 
Mbatia,Ni kosa kubwa sana kuwa na VIONGOZI toka KIGOMA,kwa mtazamo wangu na jinsi ambavyo nimepata kuwaona watu wakigoma,ZITO,KAFULILA,RUHUZA,KAKOBE,MKUU WA CHUO CHA USTAWI hawa ni watu wa KIGOMA,,,kama hawashika nyadhifa watakuangusha tuu sababu ni watu wa madaraka zaidi..,Wakipata lazima watang'ang'ania.Sijagusa utendaji wao...nimegusia tabia zao....Kwa matazamo huu tayari MBATIA alishavuliwa uenyekiti tangu waliposhinda viti vya ubunge KIGOMA,na chanzo cha mgogoro utakuta kimeanzia kigoma HUKO TANGA zubaisha nbwege tuu.
Acha ukabila wewe jadili hali ya huyu kibaraka
 
Hii tunaiita hasty generalization, ambaye ndani yake huzaa fallacies. Kila mahali kuna wazuri na wababishaji, sasa niambie ni kabila lipi ambalo watu wake wote ni safi kiasi kwamba washike wadhifa huo NCCR. We kijana vipi bana. Jenga hoja acha kabisa masuala hayo . mbona inaonesha umesoma alafu unareason kama lay man. Kabila lipi linafaa "wasukuma?''akina Shibuda? aahahahaaa, kijana hebu omba radhi fasta.
 
Mbatia,Ni kosa kubwa sana kuwa na VIONGOZI toka KIGOMA,kwa mtazamo wangu na jinsi ambavyo nimepata kuwaona watu wakigoma,ZITO,KAFULILA,RUHUZA,KAKOBE,MKUU WA CHUO CHA USTAWI hawa ni watu wa KIGOMA,,,kama hawashika nyadhifa watakuangusha tuu sababu ni watu wa madaraka zaidi..,Wakipata lazima watang'ang'ania.Sijagusa utendaji wao...nimegusia tabia zao....Kwa matazamo huu tayari MBATIA alishavuliwa uenyekiti tangu waliposhinda viti vya ubunge KIGOMA,na chanzo cha mgogoro utakuta kimeanzia kigoma HUKO TANGA zubaisha nbwege tuu.
<br />
<br />
Mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmm pumba
 
Wakati Halima Mdee anatangaza kuwa Mbatia kanunuliwa na Mfisadi ili apunguze kura za upinzani Kawe watu walichelewa kumwelewa sasa naona nccr ndo wamegutuka na bado tutayasikia mengi tu kama Rungwe ataamua kuyamwaga.
Aluta Continua...
 
mambo yote mema huishia kwenye vikao wakae naye wamweleze matatizo/mapungufu yake ndiyo njia sahihi kisha kama kuna ulazima wa kumuondoa basi ifanyike kwenye uchaguzi wa chama

kumfukuza haikuzi demokrasia ya kweli
 
Mbatia,Ni kosa kubwa sana kuwa na VIONGOZI toka KIGOMA,kwa mtazamo wangu na jinsi ambavyo nimepata kuwaona watu wakigoma,ZITO,KAFULILA,RUHUZA,KAKOBE,MKUU WA CHUO CHA USTAWI hawa ni watu wa KIGOMA,,,kama hawashika nyadhifa watakuangusha tuu sababu ni watu wa madaraka zaidi..,Wakipata lazima watang'ang'ania.Sijagusa utendaji wao...nimegusia tabia zao....Kwa matazamo huu tayari MBATIA alishavuliwa uenyekiti tangu waliposhinda viti vya ubunge KIGOMA,na chanzo cha mgogoro utakuta kimeanzia kigoma HUKO TANGA zubaisha nbwege tuu.

Bwana Mkinga una ushahidi wa hiki kitu unachoongea? Naona unataka kufanana na jirani yangu hapo jana alikuja na hoja kama hiyo. Akawa anatuhumu kigogo mmoja wa chama fulani kuwa anatafuta nafasi ya kugombea uraisi mwaka 2015. Mimi nilichofanya ni kumtaka athibitishe kwa kutoa ushahidi juu ya maelezo yake hayo... akaanza kusema "ngoja utakubaliana na mimi kuanzia mwaka keshi mambo yataanza kuwa dhahiri zaidi...". Mimi nilimwambia ni kazi bure kunieleza habari ya mambo ambayo hayajatokea, hakuna dalili za kuthibitisha kama yatatokea na ya kuwa hajuwi na mimi pia sijui kama tuakuwepo huo mwaka anaosema tuungoje.

Tuacheni uvumi, na tena uvumi unaotupeleka kwenye kuchukiana kwa misingi ya matabaka ya rangi, dini, ukabila na ukoo. Tukiendelea na mwendo huu wa kutizamana kama "hawa ni wahaya", ama "hawa ni wachagga" nk haitachukua muda tutajikuta tupo walipo Somalia sasa hivi. Naomba tuendelee kupigana na maadui aliotuacha nao Nyerere, umasikini, ujinga, maradhi na tusiongeze na ukabila, ukanda, udini, na itikadi.
 
Hata mie sinaga imani na James, dizaini kama anatumiwa vile,hata akiongea ukimwangalia kwa kina unagundua he's not serious/doesnt mean what he say. ni kama JK tu
 
Back
Top Bottom