OgwaluMapesa
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 10,942
- 428
Shinikizo la mkakati wa kumng'oa mwenyekiti wa NCCR -Mageuzi James Mbatia'' limeiva '' baada ya makada wa chama hicho 'kushikilia' bango msimamo wao wa kutaka Mbatia kujiuzulu pasipo shuruti
Safari hii makada hao wakiongozwa na Kamishna wa NCCR-Mageuzi mkoa wa Tanga Mbwana Hassan ,wameueleza kinagaubaga uongozi wa chama hicho Taifa Kuhusu msimamo wao wa kumtaka Mbatia kujiuzulu nafasi hiyo katika chama kwa hiari yake
Msimamo huo wameuweka wazi kupipia barua ya Sept 5 2011 waloyomwandikia katibu mkuu wa chama hicho Samuel Ruhuza. Mbwana katika barua hiyo ya kurasa tatu anamtaka mbatia kujiuzulu kwa madai kwamba amepoteza uhalali wa kuwa mwenyekiti wa chama Taifa. Anasema vikao vimeshafanyika kumwomba Mbatia na kumshauri ajiuzulu .Anasema kipindi walichokutana na mbatia Ruhuza hakuwapo alikuwa mkoani Kigoma.Anasema walikutana kwenye kikao cha pamoja Bagamoyo naviongozi wakuu wa chama isipokuwa Ruhuza
Mbwana anasema kinachomponza mbatia ni matamko yake mwenyewe na jinsi ambavyo amekuwa akishindwa mfululizo katika chaguzi za ubunge majimbo aliyopata kugombea Nchini ''labda nikikumbushe tu kuwa huyu mwenyekiti ndiye ,ambaye amekifikisha chama mahala kinawatatiza wananchi kutokana na misimamo yake ya kuwa wakili au mtetezi wa CCM na mafisadi'' Anasema mbwana akijibu barua aliyoandikiwa na Ruhuza
Kwa mfano anasema wakati katibu mkuu wa CHADEMA Dr Slaa na Mbunge wa singida mashariki (CHADEMA) Tundu Lissu walipotangaza orodha ya mafisadi mwaka 2007 Mbatia aliibuka na tamko kuwa watanzania wote ni mafisadi isipokuwa wanatofautiana tu viwango vya ufisadi ''Huu ni ushaidi wa kutetea mafisadi wa CCM kwa kutaka kupunguza hasira za wananchi dhidi ya mafisadi'' Anasema Mbwana Katika barua hiyo pia anasema mwaka 2010 chama cha wananchi (CUF) kilikataa kumtambua Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume,kufuatia uchaguzu uliotangazwa duniani kote kuwa haukuwa huru na wa haki,lakini Mbatia aliibuka na tamko kuwa kitendo cha CUF kutomtambua Karume kilikuwa ni uhaini' ''Hii inadhiirisha kuwa mtu huyu alikuwa anafanya kazi ya kutetea Ushindi wa CCM'' Anasema Mbwana.Anadai kwenye kikao kimojawapo cha Halmashauri kuu ya Taifa (NEC) ya NCCR- Mageuzi,aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu wa 2010 Hashim Rungwe ,alikijulisha kikao hicho kuwa wakati wa kampeni ,Mbatia alimkataza kuisema vibaya CCM anapohutubia mikutano katika jimbo la kawe
Rungwe ambaye ni mwanasheria maarufu Nchini,alithibitisha madai hayo ya Mbwana Alipohojiwa na Nipashe ''Huu ni ushaidi mwingine wa namna Mwenyekiti (Mbatia) anavyofanya kazi ya CCM ,anadai Mbwana. Mbatia aliwania ubunge kupitia NCCR -Mageuzi katika uchaguzi mkuu jimbo la kawe akaangushwa na aliyegombea kiti hicho kwa tiketi ya CHADEMA ,Halima Mdee.
Mbwana anasema hivi karibuni Mbatia pia alikaririwa na vyombo vya habari akiunga mkono mtazamo wa CCM kuwa wabunge vijana ni tatizo bungeni ,hawaelewi walichotumwa na wananchi na kwamba inaonyesha hawakuandaliwa kuwa viongozi.
''Kwa mantiki hizo zote ,naendelea kusimamia Msimamo wangu kwamba ,kwa busara za kawaida ,tena pasipo shuruti ,James Mbatia angejiuzulu.Kwani amepoteza uhalali wa kuwa mwenyekiti wa chama Taifa kwa matamko yake mwenyewe ,lakini zaidi kwa namna anavyoshindwa mfululizo katika chaguzi za ubunge.
Kila jimbo ambalo aligombea ,watu walikuwa na imani na upinzani lakini hawakuwa na Imani na James Mbatia.Ndio sababu walichagua TLP vunjo mwaka 2000 na CHADEMA kawe 2010.Katika uchaguzi wa kawe ,Mbatia hakutoa ushindani mkubwa ,badala yake alishindwa kwa tofauti ya kura 33,000 na Mdee
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana ,wenyeviti wanne wa vyama vya upinzani John Cheyo (UDP, Augustine Mrema (TLP) Freeman Mbowe (CHADEMA) ,Waligombea ubunge lakini ni Mbatia peke yake ndiye aliyeshindwa Uchaguzi.
Mbwana anasema uamuzi wa kufungua kesi dhidi ya mpinzani mwenzake katika jimbo la kawe ,unakinzana na misingi ya maamuzi ya chamakukataa kuweka mgombea katika jimbo la Igunga ili kuongeza idadi ya wabunge wa upinzani Bungeni