Harakati za kulikomboa Taifa hili: Siasa ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Harakati za kulikomboa Taifa hili: Siasa ni nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gembe, Apr 27, 2009.

 1. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Heshima Mbele,

  Baada ya muda mrefu wa kupaza sauti,takribani miaka mitatu ya kueneza mapinduzi ya kidemkrosia kupitia mijadala ya moto moto,imani yetu ya kujenga uwezo wa watu kuzungumzia mambo mabaya na kukemea mambo yote ya kifisadi.

  JF imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwafanya watu kama Dr. Slaa kuweza kusema List of Shame,Tumeweza kuanika uozo wa RDC ,DOWANS na Buzwagi,siye ndiyo tulirudisha imani ya serikali hasa baada ya bunge kuvunjika.

  Ukiangalia unaweza dhani tumefanikiwa kwa kaisai kikubwa na tunaonekana kuchoka ila kimsingi la bado kuna jambo moja ambalo tunahitaji kulifanyia kazi,jambo lenyewe ni kuwaeleza wanachi juu ya ukweli kuhusiana na Siasa ya Tanzania.

  Tuwaeleze ni nini wanatakiwa kufanya mapinduzi ili wapate maisha Bora.Mie naamini kama tukiwa na mbinu bora zaidi ya hata zile za watumishiwa Mungu walioanzisha DECI basi tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko katika nchi yetu.Tunatakiwa kupanda Mbegu kwa wanachi hawa ili zizae matunda

  Kwa kuanzia tu,ikiwai ni moja za jitihada zangu za kuwakomboa watanzania naomba sasa tuanze mijadala ya kuwajenga wanachi na natoa mapendekezo ya kuandika kitabu na kukisambaza kote huko tanzania ili kuwaelimisha na kuwapa mwamko,maswali machache tu kwa maada hii ya kwanza.

  Naomba tuanze kwa kujadili kwa kupitia maswali haya

  1.Nini maana ya siasa?
  2.Je nchi hii kuna siasa safi?
  3.wanasiasa Bora wapo?
  4.Je ili uwe mwansiasa na kiongozi lazima utoke chama Tawala?
  5.Je ni sifa zipi ambzo chama cha sisa kinatakiwa kiwe nazo?
  6.Je unahisi Jambo gani linawafanya wanasiasa vijana kushindwa kuisaida nchi yao.
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mkuu,
  These are hard questions for sure. Nitajaribu kujibu suali la kwanza na la pili kwa kusema:
  1. Upo msemo maarufu kuwa siasa ni mchezo mchafu na kama ni mchezo mchafu basi uwezekano wa kuwa na siasa safi ni haba.
  2. Watu wenye mapenzi mema kwa nchi yao kama wewe, na wengineo, wanapoingia kwenye siasa,aghalabu huchafuliwa na wao.
  3. Uweze kuwa na siasa safi, basi lazima asilimia kubwa ya wanasiasa wawe wasafi.Je, inawezekana kuwa na critical mass ya wanasiasa wenye kujizuia kuwa co opted kwenye dirty games in the political arena?
   
 3. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mkuu W,

  Tuklianza na jibu lako la mwanzoni,ambalo nilipatwa kujibiwa na Mkuu Mmoja kuwa siasa ni kuchafuana na hiyo ndiyo siasa,na hili bado ni tatizo katika nchi yetu kwanini siasa iwe mchezo mchafu wakti nchi hii ni maskini?

  Una mchafua mwenzako ili wewe ufaidike na nini?ndiyo maswali ambyo yanakuja kichwani kwenye uongozi kuna nini?nini wanakitafuta?nilikuwa nasoma ile barua ya Salva yaani mei nimeshtuka kwa kweli na unaweza kuta watu hata kina kingunge huwa anaandika barua za kuomba FURSA katika serikali sababu haiingii akilini mzee kama huyu anaendela kuwa waziri au mbunge kwa maslahi ya nani?ana msaada gani?hii ndiyo aina ya wanasiasa tulionao.

  Dhana ya kujiunga nayo hata kama ni wachafu ndiyo ambayo mie naikataa siku zote,kwa kuwa wewe hauwezi ili kuna wachafu na ni wapinzani wao na hauwezi kupingana nao unaona bora ujinge nao.Sawa unaweza jiunga nao ili je umefanya nini kuwasaidia?umeweza kuwalipua?Mie kwa maoni yangu na nchii hiii ilivyo changa hakuna kuwa na siasa chafu!

  Lets back to the question,Siasa ni nini?ila nimechukua point mbili tatu hapo
   
 4. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu Gembe,
  Nakushukuru sana kwa kuleta mada hii na nakuomba ufanye rejea Waraka wa Mchungaji.Nakumbuka Rev.Kishoka alileta thread yenye kurasa 28 wanabodi tulichangia kidogo sana nafikiri ilikuwa wakati muafaka ifufuliwe ili iende sambamba na hii.
  Natanguliza shukrani!
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  I second the motion,
  its about time we go back to that discussion initiated by Rev.
   
 6. Mbute na chai

  Mbute na chai JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2013
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Tanzania tumekuwa na vuguvug la siasa za upinzani. Katika uchaguzi wa Kenya chama kimojawapo cha upinzani Tanzania kilionesha wazi kumuunga mkono mmoja wa wagombea Kenya lakini akashindwa. Katika mlorongo wa kueneza sera nchini chama hicho pionzani Tanzania kilikuwa kikirejea vuguvugu zilizomwondoa rais wa Misri na kupelekea kuchaguliwa kwa Mohamed Morsin ambeye hivi sasa nae kaachia utawala kwa lazima. Rejea zote upinzani nchini umekuwa ukifanya zimeshindwa vibaya. Swali, nini hatima ya vuguvugu (MC4) ya hiki chama chetu pinzani? Hii imerihirisha wazi kuwa akili ya kina katika siasa ina mafanikio kuliko vuguvugu za nguvu za watu kwani dola ni taasisi isiyo shindwa kiurahisi.
  Uwanja kwenu wachambuzi wa siasa
   
 7. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2013
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,394
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Siasa ni Kilimo.
   
 8. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2013
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Siasa ni SI-HASA!!!
   
 9. Mbute na chai

  Mbute na chai JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2013
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mh! Inavyoonekana wewe ni mzee sana tangu enzi za Mwalimu! Mh!
   
 10. JEKI

  JEKI JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2013
  Joined: Aug 16, 2013
  Messages: 2,231
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  Nimejiuliza kwa muda mrefu, hata kwenye mtandao huu kumekuwa na maneno ukituma kitu labda cha kimapenzi unaambiwa huku SIASA tu, unabaki unajiuliza SIASA ni nini hasa?? ninavyojua hata kutongoza ni siasa, I mean maisha ya binadamu yote ni siasa, unavyoongoza wanao nayo ni siasa, naomba mnielewesha maana ya SIASA kasha tuone kama kweli mapenzi au mahusiano ya mzazi na mtoto nayo siyo SIASA, au tutaona kuna wakati mapenzi yanakuwa SIASA, hasa unapokuwa unampiga mistari mwanamke.
   
 11. F

  FUSO JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2013
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  Siasa ni hatua za majadiliano endelevu. Majadiliano yasiyokoma.
   
 12. F

  FUSO JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2013
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  kama haya.

  [​IMG]
   
 13. M

  Mundu JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2013
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  usingeweka alama ya kuuliza, ningekupa LIKE

  hii ndio Siasa...
   
 14. F

  FUSO JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2013
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  nime-edit mkuu ha ha ha
   
 15. c

  cappo di cappi Member

  #15
  Jun 17, 2014
  Joined: Sep 17, 2013
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  kwa mtazamo wangu siasa ni nyenzo ya kudanganya wananchi, kuwagawanya, na kuwafanya waamini kuwa matatizo yao yatatatuliwa na baadhi ya watu. tutafakari pamoja, karibuni
   
Loading...