Harakati za Chadema chuo kikuu Saut tawi la Mwanza za hujumiwa.

jembe la kigoma

Senior Member
Mar 23, 2012
119
19
wakuu ni kwa mda mrefu sasa kumekuwepo harakati za makusudi kukwamisha harakati za CHADEMA kisiasa chuoni hapa,na juhudi hizo za kuua democrasia zimekuwa zikipangwa kwa ustadi mkubwa na baadhi yaviongozi wa chuo,selikari ya wanafunzi(SAUTSO),kupitia kwa dean of students aliehamishwa (mama Nasania)waziri wa michezo (Akida)naibu waziri wa mawasiliano na hata dean wa sasa nitasema kwanini wao?

Hujuma zilianza zamani lakini zilijihilisha wazi alipokuja Mh,Tundu Lissu akakutana na makamu mkuu wa chuo ndugu Charles Kitima na kuomba apewe nafasi ya kutoa mhazara wa kisheria kuhusu elimu ya katiba na alikubaliwa na Kitima afanye kesho yake jioni ukumbi wa M13,kesho yake masaa machache akapigiwa simu kwamba hatoruhusiwa kwa sababu kuna zuio kutoka Usalama wa taifa,kamanda alilaani sana bt viongozi wa CDM tawi wakamwandalia sehemu nyingine ya dharura akashusha nondo na wanafunzi wengi walifika,hiyo ilikuwa mwanzoni mwa mwaka huu

Ziara ya katibu mkuu dk Slaa, ilitaka kuhujumiwa pia baada ya watu watu wanaojiita Usalama wa taifa kumfata mwalimu mkuu wa Nyamalango primary na kumzuia asiruhusu uwanja wake wa shule kutumika japo baadae kibali cha polisi kiliwamaliza nguvu,takribani sasa mwezi umeisha tangu imetolewa amri ya kutobandika tena matangazo ya kisiasa,amri ilitolewa na deen mpya kwa madai CDM na CCM wanasababisha vurugu,hii ilifuatia baada ya kutolewa tangazo la kulipia kila tangazo litakalobandikwa,viongozi wa CDM na CCM tawi naambiwa walilifuatilia suala hilo kwa mlezi wa wanafunzi bt aliishia kuwaonesha kifngu no53 kinachozuia harakati zozote za kisiasa vyuoni alipoulizwa why now & not before alikosa majibu coz wamekuwa wakibandika matangazo toka 2007.

kutokana na hili ilibidi nijichimbie na kuingia ndani zaidi kusaka ukweli kutoka vyanzo vyangu mbalimbali,nikaambiwa hilo limefanywa kwa ustadi mkubwa na CCM Mwanza kwa kushirikiana na waziri wa zamani wa mikopo chuoni hapa na aliyekuwa mwenyekiti wa CCM tawi la chuoni na aliyekuwa katibibu wa UVCCM Mwanza ndugu Jaredi,rais wa zamani chuoni hapa ndugu Cosmas Mataba na wwaziri wa sasa wa Michezo Akida,kwa maelekezo ya CCM mkoa,mama Nasaniana kiongozi wa juu chuoni hapa ambae pia ni padri bt sio makamu mkuu wa chuo,kwa madai kuwa harakati za kisiasa za CDM chuoni hapa zimesababisha CCMipoteze majimbo ya uchaguzi 2010 na mvuto kanda ya ziwa,ilifanywa tathimini kabla ya hatua hiyo ya kupiga marufuku matangazo ya vyama,wakagundua wao hawana cha kupoteza sana coz hawana wafuasi wengi chuoni hapa kama chadema,na ili CDM wasigundue kuwa wamefanyiwa hujuma ilikuwa ni lazma wazuie matangazo ya vyama vyote japo kimsingi CDM ndo walikuwa walengwa coz wao ndo huwa malanyingi wanatangaza mikutano na vikao vyao,CUf haipo sana chuoni hapa,wakashinikiza amri hiyo,

Na kwa taarifa ambazo bado sijazithibtisha inadaiwa kuna mkakati wa kumg`oa makamu mkuu wa chuo dk Charles Kitima kwa madai anaisapoti CDM kwa siri that why ameshindwa kukemea vitendo vya wanafunzi kuingia madarasani na magwanda na skafu za CDM,walijaribu mwanzo wakashindwa kwa madai kwamba Kitima anakubalika sana huko TEC.

Pia kuna taarifa za kutaka kumfanyia hujuma muuza magazeti chuoni hapo ndugu Musa kwa madai magazeti yake yamekuwa chanzo cha kuamsha mijadala mikali ya kisiasa ya kumpnda,kumchafua JK na serikali yake na CCM kwa ujumla,huku mama Nasania akidaiwa kutaka kuja kgombea jimbo la Wenje Nyamagana,pia kumekuwepo jitihada za makusudi za kuuikwamisha serikali ya wanafunzi (SAUTSO) inayoongzwa na ndg Malisa katibu mwenezi wa zamani wa CDM tawi,ili serikali yake ishindwe na uutishwe uchaguzi mpya au mwakani CDM isitoe rais tena that why amekuwa anahujumiwa na hata mawaziri wake wa upande wa CCM ,Akida na wenzake huku Akida akidaiwa kupokea rushwa ya hadi shilingi 40000 ili kuwachomeka watu wasikuwepo kwenye msafara wa kimasomo na michezo kwenda Rwanda,achilia mbali tuhuma za rushwa ya ngono.hata hivyo nilipo ongea na viongozi wa CDM tawi walidai kutambua na kuelewa hujma zote hizo bt wakasema CCM haiwezi kuzuia nguvu ya mabadiliko daima.
 
well said mkuu nami pia nilishawahi kuhisi kitu kama hicho kinaweza kuwa kinaendelea hapa,coz kuna siku CDM Tawi walizuiwa kufanya kikao cha ndani pale ukumbi wa quick choice ikiwa walikuwa wamelipia matangazo,wamebandika matangazo na ikiwa ni saa chache kabla ya mkutano huo kuanza uliokuwa na kibali cha mkuu wa siasa na itifaki kwa madai kuwa eneolipo ndani ya chuo.

  • :target:
 
Kwa jinsi ninavyoifahamu SAUT, ni vigumu sana kubadilisha ubongo wa wanafunzi kuwa fikra mgando.
 
  • :bowl:wanahangaika sana leo pale magazetini na kuna mtu mmoja akatamba kwamba rais wa TZ ni EL vs Magufuli, nilimshangaa coz kuna watu walikuja na hoja ya kumpinga magufuli kwa madai ni dikteta na amewadhurumu karibia wafanya kazi 60 wanofanya kazi kwenye mashamba yake na mifugo yake huko Chato.

 
Back
Top Bottom