Harakati za Anna Makinda kuua Upinzani Bungeni

KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
864
Anna Makina amekuwa na maandalizi makubwa katika kuhakikisha anadhibiti upinzani Bungeni hasa kipindi hiki cha mswaada wa katiba ambapo maandalizi hayo yamewahusisha washirikina!!

Hatua ya kwanza baadaya ya kupata Usipika alisimikwa kama Chiefu kuimalisha kama mungu mke na masharti yake hatakiwi kuolewa au kukutana kimwili na watu wa size yake bali dogodogo!!
Anna makinda alisimikwa kinyume na maadaili ya ki-chief kwa Wabena ambapo mwanmke hana sifa ya kuongoza na siku hiyo viongozi wote wa dini walisusa wakidai ni Ushirikina!!!!

Pia amepeleka kondoo wawili kwa mganga aitwaye Babu Msomali anayeishi njombe karibiu na msikiti mkuu wa Njombe ambapo kondoo hao wanaishi kama watu mmoja anaitwa GEORGE na Mwingine anaitwa MICHAEL.
Kondoo hao wanaishi kama watu na wakati wa Bunge huwa kunakuwa na kazi kubwa ya kishirikina inafanyika

Pia Anna Makinda amepeleka kitabu chake cha Wasifu wa Bunge kwa Mganga huyo kwamalengo hayohayo!!
Kabla ya kuanza Bunge Anna Makinda alipeleka Nguo zote kwa Mganga huyo likiwemo Joho la Usipika ili kupata nguvu na Ujasili wa kupinga hoja za Upinzani ambazo zinajulikana kuwa na maslahi kwa Wanyonge!!!!
 
Ashindwe na alegee magoti na mazingaumbwe yake! Hta nguvu za giza anazotumia zina ukomo wake
 
Ahmad Michuzi - Nov 11, 2010 (edited) - JIACHIE
- Public
ccm yamchagua anna makinda kuwania kiti cha uspika wa bunge

Bi. Anna Makinda amechaguliwa na Wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi kwa kura 211 kwa ajili ya kuwania Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waliobwagwa katika kinyang'anyiro hicho cha akina mama watatu walioteuliwa na Kamati Kuu ya CCM hapo jana kuwania kiti hicho ni bi Kate Kamba aliyepata kura 15 na bi Anna Abdallah aliyepata kura 14.

Kinyang'anyiro hicho kinatamatia kwa Anna Makinda (CCM) kupambana na Mabere Marando (CHADEMA).from: http://www.wavuti.com.

====== ==========

Na Ripota Wetu Kutoka Dodoma.

Hatimaye chama cha Mapinduzi (CCM), kimemchagua Mbunge wa Njombe Kusini Anna Makinda kuwa mgombea wa Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano baada ya kuwashinda wenzake wawili Anna Abdallah na Kate Kamba.

Anna Makinda ambaye atapambana na Mabere marando kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo amepata kura 211, wakati Anna Abdallah akipata 14 na Kate Kamba akiondoka na kura 15 kutoka kwa wabunge wote wateule wa CCM walishiriki kikao hicho cha uchaguzi.

Akizungumza baada ya kuchaguliwa Makinda amesema iwapo atachaguliwa atahakikisha anaunda Bunge imara na la kisasa zaidi huku akiahidi kuongoza kwa kuzingatia kanuni za Bunge.

iwapo atapata nafasi hiyo na kuandaa vipindi vya lijue Bunge ili kuwezesha wananchi kujua kanuni za Bunge na kuondoa malalamiko pindi adhabu zinapotolewa kwa makosa mbalimbali.




Copyright 2007 ©MICHUZI JR
proxy


proxy





unused plural form

0 older comments

©2011 Google - Terms - Conten
 
Je "papa" wa rushwa wanajipanga kuteka bunge?

sitta%20kampeni.jpg
Wakati taswira imeanza kuoenakana kuhusu nani ataingia kwenye bunge lijalo bada ya upigaji kura mwezi Oktoba 31, 2010 kumeanza kuwa na ripoti kwenye vyombo vya habari kwamba kuna baadhi ya watu waliotuhumiwa katika tuhuma za rushwa wanafanya kazi kuhakikisha spika wa bunge lililopita, Mhe. Samuel Sitta harejei katika nyadhifa yake hiyo.

Ripoti ya mikakati ya siri ya kunyakua bunge kwa mara ya kwanza iliripotiwa na gazeti la wiki la MwanaHALISI mnamo Juni, 2010 likiwa na kichwa cha habari; "Sitta kung'olewa Uspika".

Katika makala hiyo ilibainishwa mkakati unaoandaliwa wa chini kwa chini kuwadhibiti wabunge 14 kutopata nafasi ya kurudi tena bungeni kama wabunge ambao wataondoka sambamba na spika. Wabunge hao ni ikiwemo; Bw. Samuel Sitta (Urambo Mashariki), Bi. Anna Makinda (Njombe Kusini), Dkt. Harrison Mwakyembe (Kyela) na Bw. Lucas Selelii(Nzega).


Wabunge wengine ni pamoja na; Willium Shelukindo (Bumbuli), Christopher Ole Sendeka (Simanjiro), Bi. Anna Kilango Malecela (Same Mashariki), Victor Mwambalasa (Lupa), Injinia Stella Manyanya (Viti Maalum), Bw. Said Nkumba (Sikonge), Bw. Aloyce Kimaro (Vunjo), Bw. John Shibuda (Maswa), Bw. Godfrey Zambi (Mbozi Mashariki) na Bi. Beatrice Shelukindo (Kilindi).

"Kama wakiweza vuka katika kinyang'anyiro cha kura za maoni ndani ya chama, hatua nyingine ni kuweza kupita salama katika kikao cha kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa" gazeti hilo liliripoti.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, mpango huo kabambe unaopangwa na baadhi ya wanachama wa CCM ambao hawakufurahishwa na utendaji na staili ya Bw. Sitta katika kuliongoza bunge. Kwa mujibu wao, Bw. Sitta alikuwa mliberali sana na kuruhusu mijadala tete kujadiliwa bungeni. Baadhi ya mijadala hiyo ilikuwa tete kwa chama tawala na hata serikali yake.

Katika moja ya kikao cha juu mwaka jana, Bw. Sitta waliwekwa "kikaangoni" kwa kile kilichoelezwa miongoni mwa mengi ni kumharasi Rais kwa kumkatisha katikati ya hotuba yake na kumtaka agues moja kwa moja masuala ya msingi zaidi
Akiongea muda mfupi baada ya Rais Jakaya Kikwete kulihutubua bunge, Spika Sitta alisema, Rais alipaswa kuwa jasiri na madhubuti zaidi katika kushughulikia masuala dhidi ya rushwa mambo ambayo yalikuwa ndani ya uwezo wake.

Hilo lilielezwa na baadhi ya wanachama watiifu wa CCM kama ishara ya utovu wa nidhamu kwa Mheshimiwa Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama tawala, CCM ambacho Bw. Sitta ni mwanachama wake.

Spika pia amekuwa akisulubiwa na wanachama wenzake kwa kuruhusu wapinzani kupata fursa katika mijadala bungeni kuikabili serikali na kuanika madhaifu ya kiutendaji.

Msimamo wa kipekee uliochukuliwa na wabunge wa kambi ya upinzani katika kufichua kashfa kadha wa kadha za rushwa na matumizi mabaya ya ofisi. Moja wapo ya kashfa hiyo ni ile iliyopelekea kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowasa na hatimaye anguko la kiserikali mnamo mwaka 2008.
lowassa.jpg


Bwana Sitta alikanusha kuungana na upande wa upinzani dhidi ya serikali. Bwana Sitta alifafanua kuwa staili na mtindo aliokuwa anautumia katika kuliendesha bunge ilikuwa ni moja ya mikakati yake katika kurejesha imani na umakini wa bunge. Nataka kuacha historia nzuri na heshima ya kuendesha bunge imara na lenye kusisimua kati ya mabunge yote ya Jumuiya ya Madola, alisema Spika Sitta. Hata hivyo, hili halikuwafurahisha wanaomkosoa.

Katika hatua iliyokuwa na lengo la kujenga wigo na kurejesha heshima kwa chama, iliundwa kamati ya ngazi ya juu ya CCM ikiongozwa na aliyekuwa Rais Ali Hassan Mwinyi kuchunguza tuhuma hizo miongoni mwa wabunge wa CCM na spika na kurejesha uhai na uimara wa chama. Kamati hiyo haijawahi kutoa matokeo ya uchunguzi wao kwa umma lakini kitu ambacho kamati imeweza kukifanya ni kuweza kuwaleta tena wabunge wa CCM katika mstari na muongozo rasmi wa kichama.

Kama inavyojidhihirisha hivi sasa katika mchakato wa kura za maoni zilizomalizika, wabunge wengi makini wa CCM ambao wamekuwa wakikemea rushwa wamekuwa na hali ngumu katika kampeni na kutetea nafasi zao hizo. Wabunge 7 kati ya 14 ambao walikuwa katika orodha ya kuwindwa iliyoripotiwa walipoteza nafasi zao hizo.

Mhanga wa kwanza alikuwa Bwana James Lembeli ambaye nusura ashindwe kutetea kiti chake katika jimbo la Kahama kwa mtindo wa kimaajabu sana. Bwana Lembeli, mbunge makini na aliyejitambulisha kama mpambanaji dhidi ya rushwa na kudiriki kukikosoa chama tawala CCM ambacho naye ni mwanachama aliingia katika mtego wa kuchukua fomu katika jimbo lisilokuwepo la Ushetu.

Bwana Lembeli alianguka katika mtego baada ya Katibu wa CCM Wilaya, Bwana Sospeter Nyigoti kutangaza uwepo wa jimbo jipya linaloitwa Ushetu limemegwa toka katika jimbo la awali. "Jana jioni tulipokea taarifa rasmi toka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwamba jimbo la Kahama limegawanywa katika majimbo mawili"

Hili lilimtamanisha Bwana Lembeli kuliacha jimbo lake la awali la Kahama na kugombea katika jimbo jipya. Alichukua fomu za kugombea katika jimbo jipya la Ushetu lakini wakati wa kuzirejesha alishangazwa kwa kuelezwa jimbo hilo la Ushetu halikuwepo. Bwana Lembeli kiufundi alikuwa tayari ametupwa nje ya kinyang'anyiro. Ilibidi Bw Lembeli atumie uwezo wa ziada na mbinu za hali ya juu ili kuwashinda wandalizi na wasimamizi wa uchaguzi. Bw Lembeli alishinda kura za maoni kwa idadi ndogo sana ya kura nne tuu!

Mhanga mwingine ni Bwana Lucas Selelii, mbunge aliyepita wa jimbo la Nzega, ambaye alishindwa dhidi ya mgombea mpya Bwana Hussen Bashe. Bwana Seleli ameshalia kuchezewa rafu akitaja rushwa na kukiukwa kwa taratibu cha kiuchaguzi na makada na maafisa wa uchaguzi wa CCM ambao walilipwa kufanya kazi hiyo dhidi yake.

Mfumo ulikuwa haunitaki na ulikithiri rushwa. Katika siku ya kupiga kura ilikuwa kama vile Benki Kuu ya Tanzania imehamia katika jimbo hili. Watu walilipwa na kununuliwa dhidi yangu. Mchakato ulighubikwa na matumizi ya fedha na kununua kura. Ilinihitaji niwe na zaidi ya milioni 100 kushinda, na hiki sicho nilichokuwa nimejiandaa, alisema Bwana Seleli katika mahojiano.

Bwana William Shellukindo, mbunge wa muda mrefu wa jimbo la Bumbuli na mmoja miongoni mwa wakosoaji wa serikali dhidi ya rushwa na usimamizi mbaya wa mikataba hususan mikataba ya madini alishindwa dhidi ya kijana January Makamba, ambaye ni mshauri wa rais na pia mtoto wa Katibu Mkuu wa CCM, Bwana Yusuf Makamba.

Bwana Aloyce Kimaro, mbunge mwingine ambaye amekuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya rushwa alishindwa katika kutetea jimbo la Vunjo kwenye kinyang'anyiro cha kura za maoni. Mbunge huyo anakumbukwa kwa ujasiri wake katika kutoa hoja makini na thabiti hususan alipotaka rais mstaafu Benjamin Mkapa ashughulikiwe dhidi ya kuhusika katika manunuzi tata ya Mgodi makaa ya mawe wa Kiwira.

Bwana John Shibuda, Bwana Said Nkumba na Victor Mwambalasa wote walipoteza nafasi zao katika majimbo ya Maswa, Sikonge na Lupa wakiacha watu wengi katika mshangao. Bwana Fredy Mpendazoe kada mwingine wa CCM aliyeamua kukihama chama hicho kabla ya kura za maoni alishindwa vilevile katika kura za maoni ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA alikohamia.

Bwana John Shibuda ambaye awali alitangaza kuingia katika kinyang'anyiro cha kushindania urais dhidi ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete lakini baadae akajitoa katika kinyang'anyiro akisema anaridhika na uwezo wa kiuongozi wa Rais Kikwete. Licha ya hivyo, lengo lake na umakini wake katika vikao vya bunge havikuwafurahisha baadhi ya wanaCCM. Hivyo naye akatolewa kafara.

Bibi Anne Kilango aliweza kuhimili hujuma yote dhidi yake na kutetea jimbo lake la Same Mashariki baada ya jitihada za mahasimu wake wote kugonga ukuta. Kwa maneno yake mwenyewe, Bi. Kilango alisema ushindi wake ulishinda hujuma na hila zote zilizokuwa zinafanywa na baadhi ya watu ndani ya chama waliokuwa na lengo la kung'oa nje ya bunge. Nimeshtukia hii mikakati ya chini kwa chini dhidi yetu.Nina ushahidi wa "CD" ambamo baadhi ya watu wamepandikizwa kunishughulikia, alisema, hivyo nikawaripoti kwa Katibu Mkuu wa CCM, Bwana Makamba lakini hakuchukua hatua yoyote.

Bwana Christopher Ole Sendeka, mbunge mwingine machachari katika mapambano dhidi ya rushwa aliweza kupenya kwa hali ngumu katika mikakati hii ya kumwondoa katika kiti cha uwakilishi wa Simanjiro. Kwa mujibu wa maneno yake, waliokuwa wakifanya vurugu na fujo katika mikutano yake ya kampeni walikuwa ni pandikizi dhidi yake na ni kutokana na msimamo wake mkali dhidi ya matendo ya rushwa.

Dkt. Harrison Mwakyembe, Bi. Anna Makinda na Injinia Manyanya ni miongini mwa mwachache kati ya wale wa orodha ya wabunge 14 waliotajwa kufanyiwa mizengwe, wameweza kuvuka kwa shida katika kinyang'anyiro cha kura za maoni. Jimbo la Dkt. Mwakyembe lilikuwa tayari limetajwa kuwa ni jimbo lenye mchuano mkali. Mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu, Dkt. Mwakyembe alitangaza hadharani kwamba baadhi ya watu katika CCM wanataka kumg'oa lakini atashinda. Kwa mujibu wa matokeo ya kura hizo za maoni, Dkt. Mwakyembe alipita katika kinyang'anyiro hicho kwa kushinda kura 7,658 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Bw. George Mwakalinga ambaye aliweza kupata kura 575 tu.

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba wale waliotuhumiwa katika kashfa za rushwa au kutajwa katika baadhi ya ripoti walikuwa wanafanya kazi ya kuwaengua wapambanaji dhidi ya rushwa, kwa lengo la kulibadili bunge na kujilinda tayari kujiwekea uhakika katika ushindi dhidi ya kiti cha urais ifikiapo Uchaguzi Mkuu 2015.

Aki ongea na vyombo vya habari bada ya kura za maoni Bw Sitta alisibitisha kuwepo kwa njama na watu wenye hela chafu kutaka kuvuruga uchaguzi illi asipate nafasi ya ubunge. Kwa mujibu wa tarifa kutoka ndani ya mikutano ya kamati za siasa za CCM za wilaya Bw Sitta alipewa alama ya chini ya ‘D' huku wapinzani wake kwenye kinyanganyiro hicho Bw Alli Masanya alipat alama ya ‘B' na Bw Ali Karavina akipata alama ‘C'

Bw Sitta alisema hashangai kuwepo mipango ya kufanyiwa mchezo mchafu kwani wapo watu wenye fedha chafu wlifanya hivyo tangu wakati wa kampeni na wakashindwa.

"Lakini, aaa…siwesi kushangaa sana kusikia kama watu wanajiandaa kufanya hivyo, kwasababu kuna mijitu ina pesa zao chafu na imekuwa ikijipanga kufanya mambo ya ovyo tangu wakati wa kampeni" alifafanua.


Ripoti za vyombo vya habari vinamtaja waziri Mkuu wa zamani Edward Lowasa (Mbunge wa Monduli), Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa zamani, Bwana Adrew Chenge (mbunge wa Bariadi) na mbunge wa jimbo la Igunga, Bwana Rostam Aziz kuwa ndiyo vinara waliopo nyuma ya pazia la mchezo huu.

Hawa watu wamewai kutuhumiwa kwa kuhusishwa na rushwa na kuna badi ya vyombo vya habari viliwahi kuwaita "mapapa wa rushwa"
chenge002.jpg


Vyombo vya habari vimemlenga moja kwa moja Bwana Andrew Chenge "kukitolea macho" kiti cha Uspika wakati Bwana Lowasa akiwa na malengo yake katika nafasi ya Urais mnamo mwaka 2015. Bwana Chenge alihushishwa katika kashfa nzito ya manunuzi tata ya rada wakati Bwana Lowasa walilazimika kujiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond.

Bwana Chenge amekanusha kuhusika kwa lolote katika mikakati hiyo lakini hakupinga lengo lake la kugombea nafasi ya uspika. Alipoongea na vyombo vya habari mwezi uliopita, Bw. Chenge alisema hakupenda kuchangia katika suala hilo kwani alikuwa ametingwa na shughuli za kampeni za kura za maoni.

Bwana Lowasa na Bwana Rostam Aziz, wamekuwa wakimya katika suala na wote wameamua kujikita zaidi katika kinyang'anyiro cha ubunge. Matokeo yake wote wameshinda kwa kishindo, Bw. Rostam Aziz ameshinda kiti cha Igunga kwa ushindi wa zaidi ya kura asilimia 85 za kura zote zilizopigwa. Vivyo hivyo, Bw. Edward Lowassa naye pia ameshinda kwa kishindo kutetea kiti chake katika jimbo la Monduli.

Licha ya hivyo, Bwana Ibrahim Msabaha na mshirika wake Bwana Nazir Karamagi walishindwa katika majimbo yao yaani Kibaha Vijijini na Bukoba Vijijini.Wawili hawa wamehusishwa na kasha ya Richmond na kulazimika kujiuzulu nyadhifa zao za Waziri wa Nishati chini ya baraza la kwanza la mawaziri la Rais Kikwete.

Pamoja na kwamba baadhi ya watu ndani ya chama cha CCM wanaweza kutokuwa wamevutiwa na misimamo mikali iliyokuwa ikichukuliwa na baadhi ya wabunge na inaweza kuwa ni miongoni mwa vyanzo vya anguko la baadhi ya wabunge machachari katika kumpana na rushwa, baadhi ya wananchi bado wanaunga mkono wa bunge hawa wazalendo na mashuja wa kupinga ufisadi.

Matokeo katika majimbo mawili, Kibaha Vijijini na Bukoba Vijijini yalithibitisha kwamba idadi kubwa ya watu inapenda kuona mabadiliko na hivyo kutoa ujumbe wa wazi kwamba walioshutumiwa kuhusika na matukio yenye mazingira ya rushwa hawana nafasi katika bunge lijalo. Nani atachukua nafasi ya spika, tusubiro tuone.
 
Back
Top Bottom