Harakati kutafuta tiketi ya urais wa 2015: Rais tajiri vs rais kawaida, anayefaa nani?

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
Kwa sie tuishio mitaani huku Tanzania,hakika kuelekea uchaguzi wa 2015 naona kuna joto ambalo halipaswi kupuuzwa ambalo liko kwenye kada ya wenye ufahamu juu ya nani aweza kuwa RAIS WA TANZANIA 2015, sasa joto ilo linaanza kujongea kwa wananchi wa kawaida.Kwa wale strategist malengo na matakwa yao yanazidi kuonyesha kuelekea kwenye BULL na kuakikisha BINGO inapatikana.

Kuna mantiki na maudhui ambayo mfumo unapitia ambayo kwangu binafsi kama mwanajamii,nayaona na kutafakari ambayo ni TAG OF WAR kati ya nani apewe kugombea URAIS kupitia tiketi ya CCM.Kwa watu makini hawawezi kushindwa kufuatilia na kuchanganua tiketi ya URAIS kupitia CCM chama madaraka na mbio za uchaguzi wa 2015 kwa kuwa kupuuza huko na kuona haijadiliki eti kwakuwa chama fulani ni MAFISADI basi ni kujifanya mbuni,kujificha kichwa mchangani wakati mwili wote ukiwa wazi.

Kuna yanayosemwa na kuwahusisha baadhi ya wanccm ambao wanatajwa kwa majina na hata kwa haiba na uwezo wao KIUTENDAJI NA KIMAPATO.

Hivyo najiuliza kimtizamo na kujitwisha umbumbu wa mambo mengine kama UFISADI yawe constant kisha nibakize factor hizi KIUTENDAJI,UADILIFU NA KIMAPATO.Je rais wa kuliongoza Taifa hili aaweza toka kwenye kundi gani kati ya hili?

1: RAIS TAJIRI KIMAPATO
Aina hii ya Rais ambaye ambae anamafanikio binafsi kwa bidii zake binafsi ambazo sie wengine hatujui bali Serikali kupitia vitengo vyake maalumu ndivyo vyenye utambuzi, bali kwa fulsa yake aweza kujitambulisha na kujitanabaisha kwetu sie wananchi, juu ya utajili wake na kisha tumpime kwa vigezo vyake.Wananchi wana uwezo wa kumpima kupitia utajili wake na bidii zake lakini Je ni kweli akiingia madarakani kupitia mifumo yetu tuliyonayo anaweza kutimiza yale TAIFA inayoyategemea kutoka kwake kwa niaba ya Taifa au ndio atapata fursa ya kujijenga zaidi yeye na kada ya matajiri wenza [Birds of the same feather fly together] na si kutumia uchu wa kiu yake ya mafaniki kuwa kiu ya na uchu wa TAIFA kupata mafanikio anayona TAIFA linastahiki usisahau kuwa RAIS NI ALAMA YA RAIA NUMBER MOJA.

[Mfumo wa waelevu unaamini kuwa kuwa na RAIS huyu aliyepata UTAJIRI wake binafsi kwa kutumia silika binafsi ukitumia tabia yake ile ile ya passion aliyotumia kujitafutia utajiri pia ndivyo hivyo hivyo itamsukuma kutumia passion ile ile kujenga Nchi.Yani aiba ya wajasiliamali na tabia zao ambazo kwa dunia ya utandazi wa leo inaanza kuonekana kama ni aina ya sifa maalumu ambayo baadhi ya binadamu wanazo tofauti na wengine.Ndio maana kwa mataifa kama Marekani watu kama Rais George Washington, Thomas Jefferson, John F kennedy, Andrew Jackson, Theodore Roosevelt, Zachary Taylor, Franklin D. Roosevelt, Lyndon Johnson, James Madison ndio marais walio ingia madarakani wakiwa ni matajiri kwa nyakati zao na Kama Mitt Romney angechaguliwa mwaka huu 2012, basi nae angeingia kwenye group ilo.

Na hata Nchi kama Italia Ilipatakuwa na Waziri Mkuu tajiri Silvio Berlusconi ambae gazeti la takwimu za matajiri dunia FORBES MAGAZINE lilimtaja mwaka 2012 kama tajri mkubwa dunia akiwa anashika number ya 169 ya matajiri wakubwa sana duniani.

Nasisitiza RAIS TAJIRI ninaemjadili hapa ni Rais ambae kwa sifa ya UTAJIRI wake binafsi, jamii yake na serikali yake imeridhika kuwa UTAJIRI wake umepatikana kwa njia halali na hausiani na UFISADI au vinginevyo vyovyote nje na mifumo halali ya kijamii kama jumuhiya inayo mpa mtanzania yoyote ruksa ya kutafuta kipato chake kwa njia halali kwa mujibu wa sheria.

2: RAIS WA KAWAIDA [NDANI YA SIFA ZA UADILIFU, UWAJIBIKAJI NA UTENDAJI]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Rais wa kada hii ni Rais anaetokana na sifa zake binafsi nje ya mfumo wa kimapato na msukumo wa kuvutwa, kupata mapato kabla ya kuingia ofisi kuu kama Rais.Aina hii yaweza kuwa ni aina ya Candidate ambae binafsi mpaka anaingia kwenye kinyanganyiro cha kugombea Urais hakupata kuwa na tabia za kijasiliamali [Entrepreneurship] bali amekuwa Mtendajia, Mwadilifu na Mwajibikaji kimtizamo wa jamii katika majukumu yake kwenye jamii,yaweza kuwa katika shughuri zake kwenye idala za umma, mashirika,NGO, Serikalini na hata Sekta binafsi. [/FONT]

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Candidate huyu anaweza kuwa na sifa ya UADILIFU, UWAJIBIKAJI na UTENDAJI katika kada mbalimbali kwenye jumuhiya zetu kama sifa hizo zinazotathimika kwa vigezo vya mitazamo na si vya kushikika na hivyo kuwa na vigezo halisia, kama ambavyo tusivyo kuwa na vigezo halisia kwa baadhi utajiri wa yeyote ambae atagombea akitoke kwenye kundi la UTAJIRI.vinginevyo tuthibishiwe na Serikali kuwa utajiri wa muhusika ni genuine na hauna mashaka yatakayo ibuliwa na mwanaumma yoyote kama pingamizi lenye kuleta doa dhidi ya mteule yoyote ile iwe ni wa tiketi ya UADILIFU au UTAJIRI.[/FONT]

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Msukumo ambao jamii inao katika kuchagua Rais wa kada hii ni kupitia niliyoyataja hapo juu Uadilifu, Uwajibikaji na Utendaji, lakini vigezo hivyo baadhi vyaweza kuwa sivyo katika ualisia yani sio Tangible ni Intangible kitu ambacho pia chaweza kuwa ni artificial kukidhi mahitaji ya muhusika.Hivyo wana JF yupi kati ya hawa aweza kuwa tiketi inayokustahiki kwako Rais Tajiri au Rais wa kawaida?
[/FONT]
Tumefika kizazi ambacho UJASILIAMALI NI SOMO DALASANI ivyo mitizamo yetu pia kwenye eneo hilo umetupanua kuona kuwa TAJIRI PIA SIO KIGEZO CHA KUKOSA DHAMANA YA UMMA KUONGOZA NA HIVYO MUHUSKA KUWAJIBIKA KWENYE UJENZI WA TAIFA LAKE KWA KUPIMWA KWA VIGEZO KAMA WENGINE.

Karibu kwenye kufikilia!!!!
 
Sifa za utajiri wake ni useless!! Tutaangalia anavyojali utajiri wa nchi yetu kumnufaisha kila mwananchi,kusimamia katiba yetu na kuwa na uwezo wa kuongoza kwa kuratibu na kuwaelekeza vyema viongozi walio katika serikali yake. Awe tajiri au wa kawaida hayo kayaangalie wewe maana hatutegemei atukopeshe fedha zake au utajiri wake wala hatutegemei tumuhurumie eti kwa vile anaishi maisha ya kimaskini maana hiyo si sifa ya kuwa Rais.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Sifa za utajiri wake ni useless!! Tutaangalia anavyojali utajiri wa nchi yetu kumnufaisha kila mwananchi,kusimamia katiba yetu na kuwa na uwezo wa kuongoza kwa kuratibu na kuwaelekeza vyema viongozi walio katika serikali yake. Awe tajiri au wa kawaida hayo kayaangalie wewe maana hatutegemei atukopeshe fedha zake au utajiri wake wala hatutegemei tumuhurumie eti kwa vile anaishi maisha ya kimaskini maana hiyo si sifa ya kuwa Rais.


Kwa hiyo Hon MP!!! kipimo chako dhdi ya Candidate mtalajiwa vigezo vyako vitakuwa nini?Manake tumefika hapa tulipo kwa kuwa tuliangalia kwa kuchagua watu kwa sura ya "anavyojali utajiri wa nchi yetu kumnufaisha kila mwananchi,kusimamia katiba yetu na kuwa na uwezo wa kuongoza kwa kuratibu na kuwaelekeza vyema viongozi walio katika serikali yake.".

Niachojadili nataka vivid details za Rais mtalajiwa sio dhana za Rais Mtalajiwa [theory ]. Mfano tumeona waamerika na mchanganuo mzima wa Rais wao anavyofikishwa kwenye umma na kuamua sanduku la umma anapatikana rais ambae ni vivid sio natharia binafsi naona bado watanzania wengi tuko kwenye natharia ambayo wewe pia ni mfuasi kupitia mchango wako huu "
Tutaangalia anavyojali utajiri wa nchi yetu kumnufaisha kila mwananchi,kusimamia katiba yetu na kuwa na uwezo wa kuongoza kwa kuratibu na kuwaelekeza vyema viongozi walio katika serikali yake."huo mchango utaona vipi how?
 
Kwa hiyo Hon MP!!! kipimo chako dhdi ya Candidate mtalajiwa vigezo vyako vitakuwa nini?Manake tumefika hapa tulipo kwa kuwa tuliangalia kwa kuchagua watu kwa sura ya "anavyojali utajiri wa nchi yetu kumnufaisha kila mwananchi,kusimamia katiba yetu na kuwa na uwezo wa kuongoza kwa kuratibu na kuwaelekeza vyema viongozi walio katika serikali yake.".

Niachojadili nataka vivid details za Rais mtalajiwa sio dhana za Rais Mtalajiwa [theory ]. Mfano tumeona waamerika na mchanganuo mzima wa Rais wao anavyofikishwa kwenye umma na kuamua sanduku la umma anapatikana rais ambae ni vivid sio natharia binafsi naona bado watanzania wengi tuko kwenye natharia ambayo wewe pia ni mfuasi kupitia mchango wako huu "
Tutaangalia anavyojali utajiri wa nchi yetu kumnufaisha kila mwananchi,kusimamia katiba yetu na kuwa na uwezo wa kuongoza kwa kuratibu na kuwaelekeza vyema viongozi walio katika serikali yake."huo mchango utaona vipi how?

Mkuu jaribu kuangalia track record ya wanaotajwatajwa unaweza kusikia kichefuchefu. Lakini naamini kuwa kama CCM itaweza kutoa mgombea mzuri basi ni yule ambaye hatajwi tajwi, ataibuka siku chahce kabla ya uchaguzi. Hawa unaosikia wautafuta Urais kwa nguvu basi ujue hawana nia ya kutumia utajiri wa nchi kuwanufaisha wananchi, inawezekana kuwa wao tayari ni matajari na urais hautabadilisha sana uwezo wao kiuchumi,lakini watatumia kuiba kwa nguvu zaidi na kujidai kuwa tuko juu.

Tukisema tuangalie chama na itikadi na sera za chama, hatutakuwa na lolote kwa kuwa kama itikadi na sera za CCM za sasa ni nzuri sana, lakini utekelezaji wake ni kinyume kabisa na yale yanayoelezwa.


Hata ukisikia kwenye kampeni wakati wanaomba kura, wanayosema huwa ni kwa jili ya kupata kura tu, wanayofanya ni tofauti kabisa. Mifano ipo mingi sana kwa wabunge wetu, na wote wanakuwa na uwezo wa kuongea na sio kuongoza.

Usiwasikilize hata kidogo ma-demagogue politicians jukwaani hodari lakini katika hali halisi ni wezi kweli.
 
Kwani mtu tajiri sio mtu wa kawaida? Mtu anaweza kuwa na sifa zote mbili.
 
Back
Top Bottom