Happyness Magesse anaulizwa Kiswahili anajibu Kiingereza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Happyness Magesse anaulizwa Kiswahili anajibu Kiingereza

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Mzizi wa Mbuyu, Jun 22, 2009.

 1. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,496
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa nafuatilia matangazo ya TBC1 Jumamosi jioni tarehe 20 Mwezi huu, nikaona mahojiano kati ya mtangazaji wa TBC1 na miss Tanzania wa zamani na mwanamitindo Happyness Magesse yaliyofanyika huko Afrika ya kusini.
  Jambo moja lilinishangaza, kila mtangazaji alipokuwa akimuuliza kitu (kwatumia lugha yetu ya taifa), basi Happyness alikuwa anajibu kwa
  ung'eng'e wa hali ya juu! ikawa kama kituko hivi, ........

  Mfano;
  Swali..."Hebbu tuambie, nimafanikio gani umepata toka ulipojiunga na fani hii......"?
  Happyness..." You know, if your talented and you want to succeed, yuo "kudu, kudu, kudu be zis o zat.........."
  Ilikuwa hivyo kipindi kizima!!

  Sasa hapa nauliza jamani, dada yetu huyu kiswahili hajui? au amekisahau baada ya kukaa sana 'Sauzzi'! Au toka alipokuwa huku alikuwa hakijui amezaliwa nje ya bongo!?
  Ninini hiki??
   
 2. k

  kela72 Senior Member

  #2
  Jun 22, 2009
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 168
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aaaah! wewe ndiyo ushangawe! mbona hata humu JF tabia hiyo ipo tele?
  In short ni kwamba, kuna watu wanadhani wakiongea kiingereza hadhi yao inaongezeka.
   
 3. K

  Kampton Member

  #3
  Jun 22, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uelewa mdogo wa sisi wabongo hasa kama umekuwa maarufu ktk nchi yetu bila kuvunja mayai kwa kukuuliza kama 'unajua' amesoma kama 'u know'
  Na siye yeye mwenyewe na baadhi ya maprofessor wetu unamuuliza swali ambalo ni jepesi hujifanya kutoa vipengele vingi vinavyohusiana na swali ulilomuuliza kuonesha anajua hii ilitokea ktk kipindi cha pima joto kilichokuwa kinahusiana na bajeti yetu ya bongo.
   
 4. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #4
  Jun 22, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  ...Hii imeniacha naangua kicheko ile noma!!!!...Bongo kazi tunayo!:):):)
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  hahahaha mkuu Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.
   
 6. Miwani

  Miwani Senior Member

  #6
  Jun 22, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 182
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hadhi haiongezeki kwa kujua Kiingeleza, muhimu ni muongezeko wa fedha
   
 7. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,496
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Mh, basi tuna safari ndeefu sana kufikia kujitambua kuwa na sisi ni watu kama watu wengine wenye lugha yao, utamaduni wao n.k
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Jun 22, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Jamanieeehh... TUmchukulie poa, ndio anapractice ili akihojiwa na wenzetu aweze japo kututoa kimasomaso

  Ila hiyo ya kudu...kudu kiboko; she kudu make it big time and kudu also be interviewed na Oprah...
   
 9. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #9
  Jun 22, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Kisha baadae unasikia...'of kosi yesi!'...mmmh!!!..Kiswahili au Kiingereza?
  Lugha za wenyewe zinakazi kweli.
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Lazima aonyeshe yeye yuko na mambo fulani hata lugha ya mchicha anaitema vile vile....anajipaisha matawi ya juu....Keep it up Magese.....usitusahau jamaa zako wa Mtibwa!
   
 11. F

  Froida JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nilimsikia nikasikitika sana,kwani angejibu kiswahili angechubuka kweli ni limbukeni,halafu alikuwa na pointi nzuri sana za kuhamasisha vijana wanaotaka kuingia kwenye fani ya urembo,lakini mmh kimombo kingi watanzania waondokane na utandu wa fikra kuonyesha kuwa wanaweza kwa kujua kiingereza ni watanzania waliompa kura akawa hapo alipo awe na nidhamu ya kuzungumza kiswahili kwa kweli,ni lugha yenye hadhi kubwa tu duniani
   
 12. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #12
  Jun 22, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  haaa nilikuwa cna mpango wa kucheka leo, u made ma day mzizi wa mbuyu!
   
 13. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #13
  Jun 22, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kama tunathamini sana Kiswahili kwa nini wakati wa mashindano ya kumtafuta Miss Tanzania mtu anapewa uhuru wa kuzungumza Kiingereza au Kiswahili? Na hili halionekani kama ni ajabu? Tena hapa nyumbani! Leo hii akiwa huko ughaibuni - nadhani sina uhakika - akiongea Kiingereza tunalalamika. Tuwe wakweli. Wengi - kama si wote Watzania - tuna matatizo.

  Tena kwenye mashidano ya kumsaka Miss Tanzania, binti akichagua kuongea Kiswahili anaonekana wa kuja ile mbaya. Ndo maana unaona wengi - kama si wote - wanajitutumua kuongea huo Umombo hata kama haupandi. Watanzania aibu yetu! Tuna matatizo ya fikra. Tujikomboe ndipo tumlaumu huyo binti. Yeye kwa kiwango kikubwa ni taswira ya jamii yetu. Pole yetu.
   
 14. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #14
  Jun 22, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Watu kama Happyness Magesse ni watu wa kuonewa Huruma. Kizungu chenyewe hakijui. Kwa mfano akiwekwa Abonge laivu na watu kama Wakina Shayo na Mashaka, hicho kiinglishi chake si atajiaibisha? Ndo kawaida zetu wabongo. Mtu akitoka tu nje ya Tanzania hata kwa wiki kiswahili anakuwa amekisahau. Hata na mimi kiswahili nilikisahau nilipoenda kwa mzee Madiba
   
 15. S

  Sep New Member

  #15
  Jun 22, 2009
  Joined: Apr 2, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Teh teh teh,wadau mmeniacha hoi kwa kicheko! hii ndo Bongo. Mtajuaje kama yeye ni "matawi" na kiswahili kimempotea kwa ajili ya kukaa muda mrefu sauzi? Siyo mara moja nimesikia wadau wakiongelea hili huku uswazi.
   
 16. ram

  ram JF-Expert Member

  #16
  Jun 22, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,200
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Jamanieeehh... TUmchukulie poa, ndio anapractice ili akihojiwa na wenzetu aweze japo kututoa kimasomaso

  Ila hiyo ya kudu...kudu kiboko; she kudu make it big time and kudu also be interviewed na Oprah...

  Duh! humu ndani kuna kazi, nimecheka mbavu sina
   
 17. a

  agika JF-Expert Member

  #17
  Jun 22, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 381
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hahahahhahahhahah mie mwenyewe mbaaaaavu sina mkuuu sikuwezi
   
 18. a

  agika JF-Expert Member

  #18
  Jun 22, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 381
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  nakubaliana na wewe Babu Yao coz tupende tusipende hayo ndiyo yaliyojiri Kiswahili hakitukuzwi kutoka Miss Uchochoroni hadi Miss Tanzania, lakini pia tusisahau kwamba sisi humu JAMVINI tuko huru kuongea lugha yeyote kwasababu hatumwakilishi mtu yeyote zaidi ya kujiwakilisha sisi wenyewe , ila Happiness ana jukumu la kuwakilisha nchi yake tanzania duniani, sasa yeye akiwa anahojiwa mbele ya TBC1 ambayo inatizamwa na nchi mbalimbali kupitia DSTV alitakiwa akitangaze kiswahili kwasababu ile ni television ya Taifa na sisi lugha yetu ya taifa ni Kiswahili ,Kile kingereza asubirie akihojiwa na Televion za nje, na pia alikuwa anapoint nzuri sana za kuwapa moyo wale wenye kupenda fani hiyo hata waliopo nje ya miji mikubwa lakini inawezakana kabisa ujumbe wake ukawafikia wachache kuliko ingepaswa iwe kwasababu tu ya kutumia lugha ambayo si ya taifa, kama angekuwa anahojiwa na Kituo cha Television kama East Africa ingekuwa ni case nyingine kwasababu wale tunajua ni KiswEnglish kwa kwenda mbele, so naungana na wale wote wanaosema dada yetu kachemka jamaniii japo namfagilia sana kwa hatua aliyopiga but ukweli ni kwamba ANA JUKUMU KUBWA KUTANGAZA NCHI YETU ,LUGHA YETU NA UTAMADUNI WETU nje ya NCHI YETU.
   
 19. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #19
  Jun 22, 2009
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Nakubaliana na wote ambao hamkufurahishwa na interview ya Happiness (MILLEN ) magesse na Mtangazaji wa TBC1 (Mwangaza). nafikiri tatizo kubwa zaidi si kuchanganya lugha kama wengi tufanyavyo, hata hapa JF; wakati mwingine watu hukosaa maneno sahihi ya kiswahili(tunaweza kuwasamehe) lakini , Happiness alikuwa anaulizwa maswali Kiswahili, anajibu kwa Kiingereza kitupu, hadi pale anaposhindwa kujieleza vizuri anachomeka maneno ya Kiswahili. Alijua kabisa primary audiance(hadhira) yake ni watanzania,(waswahili) inapoangaliwa TBC 1. Alikuwa anshauri mabinti wa kitanzania, kwa kiingereza??? Kwangu alionyesha uelewa mdogo mno wa mambo ya kawaida kwa mtu wa daraja lake (mwanamitindo wa kimataifa). Pia inashangaza TBC1 kurusha interview ya ajabu kama ile; kila upande unaongea lugha tofauti na hakuna tafsiri?! Fikiria unaangalia ALJAZEERA mtangazaji anamuuliza maswali mtu kwa kiingereza halafu yeye anajibu kiarabu na hakuna tafsiri! Sijui watanzania tuna matatizo gani, ilishindikana nini kuweka tafsiri ya maandishi? haraka ilikuwa ya nini?
   
 20. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #20
  Jun 22, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Ndivyo tulivyo.......tukiula kidogo????nashangaa sana....ila ndio bongo celebrity walivyo
   
Loading...