Happy Birthday wanaojilimbikizia mali na wachoyo

Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,797
11,890
Ndugu zangu, pamoja na hekaheka za maisha, inapendeza kama jamii, kuwa na muda wa kukumbushana maswala muhimu katika maisha yetu kama binadamu.

Nimekwa na muda wa kutafakari kwa kina juu ya watu wawili. Mmoja ni tajiri sana, anazomali nyingi za kumtosha yeye maisha yake yote, watoto wake, wajukuu na hata vitukuu vinaweza kuishi bila kufanya kazi. Mtu huyu ana utajiri mwingi kuliko binadamu wa kawaida katika jamii yake. Ana nyumba nyingi na zingine hazikumbuki.

Mtu wa pili ni binadamu anayeishi kwa sababu Mungu ametoa pumzi bure. Huyu ni maskini. Akisikia kichwa kinauma, anawaza atapata wapi hela ya kununua aspirini. Watoto wakirudi mapema kutoka shuleni kabla ya muda, mzazi moyo unashtuka anawaza mtoto wake karudishwa kwa sababu hana uniform sahihi.

Akisikia hodi anawaza wageni watakalia nini hata viti hana. Wakiomba maji anafikiria kikombe gani atawapea. Lakini mtu huyu huyu akisikia shida kwa jirani, ni wa kwanza kuhudhuria hata kama hana solution sahihi. Kwenye vikao vya jamii hakosi japo mawazo yake hayathaminiwi kwa kuwa ni maskini. Lakini asipohudhuria atalipishwa faini kwa shuruti bila huruma.

Hawa watu wote ni binadamu. Wote huzaliwa na mwanamke. Huishi chini ya jua, wote huhitaji kula, kunywa na usalama. Wakiumia wote hutoa damu na hata wakiumwa Malaria, wote hupata maumivu sawa. Lakini mwisho wa siku wote hutoweka. Mwingine kama anakufa kifo cha kawaida, huzikwa na watu wengi wenye maisha ya ufahari na sherehe kubwa. Tena yamkini huzikwa na vitu vya thamani kaburini ambavyo kama vibaka hawaibi, basi bila shaka yeye huoza na kuviacha vile vitu. Huyu mwingine anaweza kuzikwa bila jeneza, pengine akafunikiwa na ngozi ya mnyama na kulazwa kaburini na watu wachache tena kwa muda mfupi. Lakini jambo la pamoja ni kwamba wote hufukiwa chini ya ardhi. Yanayotekea kuanzia hapo, Mungu ndiye anajua.

Tukijua mzunguko wetu ni mmoja na hatima yetu moja, si vyema sana tukijifunza kutenda mema kwa sababu sis sote tunapita hapa duniani na tunakoenda hatujawahi kufika?

Wewe uliyejaliwa kuwa na mali nyingi, usimdharau ambaye hana. Kila inapowezekana msaidie naye akushurkuru. Mkibaki matajiri peke yenu, nani atawashangaa ama hatakuwashangilia? Usipotenda mema nani atakushurkuru? Ni faida gani unaipata kuwa na mali nyingi peke yako katikati y awatu wenye huzuni na mateso? Hizo mali bila kushirikiana na ndugu ama binadamu wenzako wenye mateso zinakupa furaha gani?

Kuna watu wengine ni wachoyo hata kwa wazazi na ndugu zao wa karibu. Tafuta kusaidia mtu mmoja umwondoe katika hali duni ajitegemee uone namna inavyoleta amani kwako na faraja.

Kujilimbikizia mali na uchoyo wa mali unaleta huzuni na ukiwa mkubwa. Uzito wa moyo usiokoma na kujitenga na watu wenye mioyo safi kitu ambacho kinapunguza maisha yako. Mungu amekujalia ubunifu wa mali, shirikisha ndugu na majirani ili angalau wakupigie makofi na kukupokea brief case unapopita kwa mioyo iliyochangamka. Acheni kuwa vitisho kwa jamii ya wahitaji kwa sabbu mnajiumbia roho za unyama ambazo hazikupi utimlifu wowote wa furaha kama binadamu.

Ninaomba kuanzia sasa, wenye hulka zile mzaliwe upya. Tambua utoshelevu siyo wingi wa mali bali ni kiasi cha moyo. Wakumbuke ndugu zako na majirahi wahitaji ushirikiane nao kwa kuwasaidia kwa upendo na si kwa hila. Umsaidiapo mtu furahia mafanikio yake na umwache huru si kumsimanga ama kuanza kumsema kila kukicha kwamba ulimsaidia hadi afedheheke!. Unapoona watoto wako wanasoma, wafikirie na watoto wa wengine wanaonshindw akusoma. Mungu akikupa uwezo ajiri wahitaji ili nao waweze kujikumu katika maisha.

Acha kumwonea maskini na mnyonge. Wengine hadi wamefika mahala wanawasingizia uwongo wanyonge wasio na mtetezi pasipokujua kwamba Mwuumbaji wetu ni mmoja!. Wengine hata wamehukumiwa kunyongwa ajili ya kubambikizwa makosa na hawana uwezo wa kusikilizwa kwa kuwa ni maskini. Wako watu wameuawa bila kosa kwa utashi wa wenye navyo.

Kumbuka binadamu sote huzaliwa, huishi na hufa mara moja. Maisha haya na rangi zake ni mbwembwe tu na wala hayadumu. Mwisho wa wote ni mmoja. Mwili mavumbini, roho ilikotoka. Maisha ni mafupi na hakuna mwenye hatimiliki. Tutendeane mema kama binadamu.

Kwa wale wlaimbikizaji wa mali, na wale wachoyo, ninajua leo mnazaliwa upya na kujiona ni binadamu kama wengine kwa sababu sote mavumbini tutarudi.

Happy Birthday wachoyo na wanaojilimbikizia mali. Kuanzia leo acheni. Maisha ni mafupi hivyo ni vizuri kuwatendea mema binadamu wenzako ungali ukiwa hai.
 
Thread za maana kama hizi UKAWA wenzako hawachangii..wamekalia majungu tu ya lugumi lugumi...chadema badilikeni
 
bigonzo huu uzi hauna chama wala dini jamaa kaandika vitu vya msingi sana acha kupotosha au kugeuza geuza maneno...fikra pevu za kina Stive Biko safi sana mkuu
 
Thread za maana kama hizi UKAWA wenzako hawachangii..wamekalia majungu tu ya lugumi lugumi...chadema badilikeni
Usimuharibie mtoa mada uzi wake wenye ujumbe mwanana. Mizuka na mahaba yako ya siasa weka kando au anzisha uzi wako.
 
Tabby uliyoyasema ndo wengi tunayawaza ila kutoboa ubongo na moyo wa mtu si rahisi. Bigonzo nahisi unaumwa ugonjwa unaitwa UKAWA sababu there is no where Tabby hinted anything about politics. Ujue mnatuchefua wengine ambao tumo JF siyo sababu ya politics but kuelimika na kujuzana ya ulimwengu huu. Please kama unapenda siasa kaa huko huko kwenye jamvi la hayo mambo tutakufuata.

Tabby nadhani tungekuwa na mikutano ya kifamilia au kivijiji bila kusubiri misiba na harusi, haya yangekuwa yanasemeka lakini sasa hivi ukijitahidi mmoja kwenye familia, unakuwa we ndo ngazi wengine wanasepa. Msemo uliopo sasa kwa ndugu wasiopenda kusaidia ni mimi oho nina fees za watoto au kuna ujenzi fulani namalizia au Boss wetu sasa hatupi hata muda wa kufanya mambo yetu ya pembeni. Je wanaosaidia wanaupata wapi huo muda. Hawa ndo watu wanapokwenda nyumbani hufanya sherehe na kupika vyakula na kunywesha kijiji kizima lakini dhubutu uombe pesa za kununulia madaftari watoto, we utatolewa nduki au utapigwa dana mpaka jamaa naondoka saa tisa za usiku kukwepa ahadi. No plitics please.
 
Back
Top Bottom