Happy birthday Mwenyekiti Taifa CHADEMA, KUB na mbunge wa Hai ndugu Freeman Mbowe

Mjema Vushanje

Senior Member
Sep 24, 2017
159
500
Leo ni siku muhimu sana, Siku aliyozaliwa mtu Mtu muhimu sana.

Mtu ambaye wengi wanafaidi harakati zake bila hata kujua hata wale wa upande mwingine pia wanatembelea kwenye harakati zake.

Ni mtu jasiri kuliko hata wewe, Mwanaharakati wa ukweli. Angekuwa na tamaa leo hii angekuwa na cheo kikubwa sana huko Serikalini kuliko hata wengine wengi tu lakini akaamua kusimamia mageuzi kwa virungu,mabomu ya machozi,kuwekwa mahabusu na biashara kuharibika.

Huyu hafiki bei.

Happy Birth Day FREEMAN MBOWE!

 

chuuma

JF-Expert Member
May 19, 2015
353
1,000
Na Boniface Jacob

Heri ya Kuzaliwa Kamanda wa Anga *FREEMAN AIKAEL MBOWE*......

Kwenye Chama ni Mwenyekiti wetu.
Nje ya Chama ni Mzazi na Mlezi wetu.
Kwenye siasa Ni alama ya Mageuzi Tanzania.

Kiuchumi ni Mtu aliyetoa kila kitu chake kwa ajili ya Taifa lake,Umekuta kwenu Kuna magari,Majumba. Ya kifahari na Chama Tawala walimuheshimu Baba yako Mzee Mbowe......mpaka leo najiuliza hukulizika na nini? Ukajiingiza Kwenye vita hii ya kisiasa iliyochukua kila Kitu chako? Umepoteza Mali,Marafiki,Ndugu,na Amani umebakia nafuraha Kujiamini tuh.

Nakushangaa hata Malipo yako Mengi ni Kejeli,dharau,kushambiliwa na Matusi kwa Unaowapigania ila Ujali!!!!!! Sasa we Mtu gani?

Ningali kijana Mdogo tuh pale UDSM kukaa karibu yako lilikuwa kosa kubwa,Nikajikuta siogopi Mtu yeyote,Wala siogopi tena watawala na Mahakama zao,Jela zao wala Bunduki zao,Nikaanza Kiongea kwa kibesi kama Wewe,Ghafla na Mimi Nahutubia Mageuzi,Hata Mama yangu anajua Ujasiri na Kujiamini kupita kiasi havimo Kwenye Ukoo Wetu,Bali ni zao la Kazi yako.

MUNGU anijalie nione Mwisho wa Kazi uliyoipokea kutoka Mikononi Mwa wazee wetu,Mtei na Bob Makani....Mali zako zimepotea ila Jinalako litadumu Enzi na Enzi.Amin
 

Nyanko

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
399
500
Umenigusa sana kwa maneno yako Mungu alimleta Mh Mbowe kwa makusudi maalumu na lazima yatimie HAPPY BIRTHDAY Shujaa Mbowe!
 

REDEEMER.

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
8,948
2,000
Hahaha hili eneo limenichekesha sana "

Ningali kijana Mdogo tuh pale UDSM kukaa karibu yako lilikuwa kosa kubwa,Nikajikuta siogopi Mtu yeyote,Wala siogopi tena watawala na Mahakama zao,Jela zao wala Bunduki zao,Nikaanza Kiongea kwa kibesi kama Wewe"


Mugabe kwa kupenda sifa hajambo mpoozeni tu kupigwa kibuti na sepenga ni msiba kwake
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
26,715
2,000
Umekuta kwenu Kuna magari,Majumba. Ya kifahari na Chama Tawala walimuheshimu Baba yako Mzee Mbowe......mpaka leo najiuliza hukulizika na nini?
Haya MBOWE jibu swali hilo uliloulizwa na meya wako.
 

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,311
2,000
Desemba 9, 1961, alizaliwa mwanasiasa shupavu na Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania CHADEMA ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni KUB, mh Freeman Aikaeli Mbowe.

Kutokana na kuzaliwa siku ya Uhuru wa Tanganyika ndio sababu ya kuitwa 'Freeman'.

Leo ametimiza miaka 56 sawa na umri wa Uhuru wa nchi yetu.

Andika neno lolote kumtakia heri ya kuzaliwa.
 

jaywacnza

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
993
1,000
Ushupavu wake ushaexpaya.....
Sahv anambwela sana 2015 vijana waliitaji kauli yake akawakimbiaaa....msaka tonge tu huyu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom