Happy Birthday Mahondaw wangu

Status
Not open for further replies.
View attachment 789137


mahondaw wangu siku hii ni maalum ya maisha yako, nataka kuona tabasamu lako kwenye hii siku yako ya kuzaliwa. Hakuna kilicho bora kuliko kushiriki siku hii maalum na wewe mahondaw wangu, wewe ndiyo furaha yangu. Hakika najivunia kupata mpenzi aliyetulia mbele ya jamii ila mtundu sana uwapo na mimi, hongera kwa wazazi wako kwa kunizalia kipenzi, zawadi yako toka kwangu ni ahadi ya kulienzi penzi lako. Happy Birthday mahondaw wangu.

Dunia yangu imekua tamu baada ya kua na wewe. Miaka huja na kuondoka. Mapenzi na Upendo wangu kwako ni mkubwa kuliko angani na kina kuliko bahari. Umeweza kuleta ubora ndani yangu, wewe ndiyo mwanga ndani ya moyo wangu.


mahondaw wangu wewe ni mtu maalum na muhimu sana kwangu na leo ni siku yako ya kuzaliwa hivyo namshukuru Mungu. Haijalishi nini kilichofanyika. Bila kujali nini tumefanya. Haijalishi nini utafanya. Nitakupenda kila wakati mahondaw wangu, daima upo katika mawazo yangu, Wewe ni maisha yangu, moyo wangu, nafsi yangu.


Happy Birthday mpenzi wangu.
Hataree
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom