Happy Birthday kwako Profesa Emeritiusi Muadhama Askofu Mkuu Dkt. Desmond Mpilo Tutu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
HUYU NDIYE ASKOFU MKUU DESMOND TUTU

Happy Birthday kwako Profesa Emeritiusi Muadhama Askofu Mkuu Dkt. Desmond Mpilo Tutu, Askofu Mkuu mstaafu wa Capetown, Kanisa Anglikana Afrika Kusini na Katibu Mkuu mstaafu wa Jumuiya ya Makanisa ya Afrika Kusini. Kupitia sauti yako dunia ilielewa uovu na madhara ya Sera za Ubaguzi wa Rangi (Apartheid) za Afrika Kusini.

Wewe uliutendea haki wito wako kama Askofu! Ulichafua Joho la Kiaskofu ili kuambatana na waliokuwa wakikandamizwa na kunyimwa haki katika nchi yao wenyewe! Katika mahubiri yako siku ya kumuaga mwanaharakati Steve Biko aliyeuawa kinyama na vyombo vya usalama, wewe hukusita na wala hukuogopa kukemea waziwazi udharimu wa watawala ingawa watu wa usalama walijaa kama manyigu siku hiyo.

Sauti kama yako ni adimu katika zama zetu hasa katika Bara la Afrika kwa sababu ya hofu, unafiki, woga, na maslahi binafsi. Maaskofu wengi wanaogopa kutetea haki na kukemea maovu kwa kuogopa kuambiwa kuwa wanachanganya dini na siasa. Wanasahau kuwa kuwasifia watawala pia ni kuchanganya dini na siasa.

Kwao dhambi ni uzinzi na ulevi tu. Hawaoni kama ukandamizaji, uuaji, unyanyasaji, utekaji, na utesaji ni dhambi iliyo kuu. Kwao wanaona kukemea mambo hayo ni kuingilia siasa. Wamesahau kuwa hata wewe Serikali ya Ki-Kaburu ilikutuhumu kuwa unachanganya dini na siasa na kwa sababu hiyo ulijikuta ukiishi katika hali ya mashaka muda wote na wakati mwingine ulinyang'anywa Passport (Hati ya Kusafiria) yako!

Unapotimiza miaka 90 tangu ulipozaliwa tarehe 7 Oktoba 1931, tunapenda kukitakia heri na maisha yenye siha na fanaka njema. Maisha yako yatukumbushe thamani ya mwanadamu na haki yake ya kuishi, haki ya kujieleza, haki ya kusikilizwa, na haki ya kushiriki katika maamuzi yanayoathiri uhai wake.

Sisi Askofu tunawaomba watu wasambaze ujumbe huu kila mahali ili Maaskofu na Wachungaji wao waone jinsi ulivyojitoa katika kutetea haki katika zama zako ili wapate somo jinsi ya kutetea haki katika zama zao!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani (World Fellowship of Moravian Revival Churches)

A0A15226-9738-4566-8364-471BEC23C000.jpeg
 
Hawa ndio maaskofu sasa. Achana na hawa wahuni wachumia tumbo
Tutu huyu mtetezi wa ndoa za jinsia moja? Huyu aliyevuliwa uaskofu kwa sababu ya kuzaa nje ya ndoa?

Mleta mada Desmond Tutu sio askofu alivuliwa
 
Back
Top Bottom