Happy Birthday CCM, Tunawashukuru kwa mema yote mliyolitendea taifa ikiwemo kuukubali mfumo wa vyama vingi!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,560
141,377
Namtakia kila la kheri mwenyekiti wa CCM Dr Magufuli

Nawatakia kila la kheri makamu mwenyekiti mzee Mangula, Katibu mkuu Dr Bashiru na sekretarieti yote

Namtakia kila la kheri kada mkongwe na asiyechoka Mzee Mgaya

Nawatakia kila la kheri wanaccm wote

Mwisho lakini siyo kwa umuhimu nawatakia kila la kheri wapinzani wote kwa kuiunga mkono CCM na hasa Mzee Shibuda, mzee Cheyo, Prof Lipumba, KUB Mbowe, Mzee Mrema na James Mbatia

Mungu ibariki Tanzania na uibariki pia CCM!
Amen!
 
Bado hawajakukumbuka kwenye teuzi?

Sent from my SM-J700H using Tapatalk
 
Umesahau kuutaja ubaya na uovu wote uliotendwa na CCM dhidi ya Wa Tanzania iwe kwa kukusudia au bila kukusudia lawama zote kwa CCM.

Ukikutana na mwenyekiti mueleze kwa kina jinsi Wa Tanzania wanavyomchukia Makonda na kumtaja katika kila ovu japo hawaweki ushahidi Ila hisia zaidi, hivyo authibitishie umma ukweli Wa hizo tuhuma ambazo mpaka mataifa ya nje yametoa reactions zake nao kihisia maana hawajatuonyesha ushahidi nasi kiukweli tunawaamini hao Wa nje kutokana na chuki zetu dhidi ya CCM.

Lakini umwambie mwenyekiti tena kwa kumnong'oneza wakati mnalishana keki kuwa huyo makonda a.k.a Bashite aache ukuda kwenye mambo yasiyomuhusu mbona hajielewi?

Kubwa zaidi huyo mwenyekiti autizame uchumi unazidi zorota kwa makusudi kabisa, diplomasia ndio usiseme yaani tunarudi nyuma.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marafiki wakuu wa CCM hongera zao ie Tundu Lissu, Zitto na wengine. Aidha washabiki wa CCM wa JF akina Sky Eclat , Erythrocyte Informer et al. Endelea kuisapoti CCM ili izidi kujivua gamba. Gamba la kwanza ni Bashite. Sie watazamaji yetu macho
Bashite kama mtoto Wa mizimu vile, hasemwi kwa wazazi aisee!
Kijana jeuri kama jini vile yaani anajikuta yeye ndio mtoa pumzi pumbavu zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Happy birthday CCM

Mkitoa vitisho vya mauaji tafsiri yake inabadilishwa na kufanywa mauaji ya kisiasa.

Lkn wengine hata wakitoa kejeri tu kwenu, TISS, POLISI, JW, wote wanawavamia kama magaidi.

Mtu akiwakosoa nyinyi pamoja na serikali yenu, mnamfungulia kesi ya Utakatishaji.

Kwa haya mnayotutendea hatuwezi kuwa na dua njema. Mjirekebishe
 
ccm mrudieni Mungu acheni kumkumbatia huyo 'aliye kinyume na Mungu'. matendo maovu yataandamana nanyi hadi jehenamu na huko ndio kutakuwa makao yenu!
 
(1) Kweli bila ccm kuruhusu vyama vingi wewe john usingeishi kwenye vitundu vya hapo Lumumba na kuingiza buku saba kila jiwe linapoteleza kwenye tiles.

(2) bila ccm kuruhusu vyama vingi usingepata nafasi ya kufuatilia nyuma ya mat...Ako ya jiwe likienda shato wewe upo tu nyuma yake likienda chamwino upo tu mgongoni utafikiri li drone LA matak..ya jiwe.

(3) bila ccm kuanzisha vyama vingi ulivyomaliza tu shule pale highland iringa ukapata ajira Lumumba wewe badala kwenda shycom kwenda kusoma mabookkeeping na ungekuwa na PhD 4 sasa umebaki kutembea na ilani ya fisiemu na ile bookkeeping uliokuwa umesoma pale highland sekondari school iringa umeiacha imechochora hapo mnazi mmoja Stendi ya zamani ya mabasi ya kurudi iringa ukakimbili kwenye vitundu Lumumba
 
MABAKULI,
Bwashee mimi sikusoma Book keeping mwalimu wangu wa kemia alikuwa Mfalamagoha Kibassa mbunge wa kwanza wa upinzani mkoani Iringa kupitia Nccr mageuzi.

Nashukuru mate wangu Salim Assas anaitendea haki CCM hapo Iringa na muuza mitumba maarufu enzi zetu pale miyomboni Mchungaji Msigwa aka Wagada sasa anayafaidi matunda ya CCM kuruhusu vyama vingi!
 
Ninakumbuka siku CCM inazaliwa, uwanja wa karibu uliitwa Sabasaba. Jioni tukisha oga ndiyo tunapelekwa kwenye maonyesho. Mabanda yalikuwa na vitu vingi. Kumbukumbu yangu kubwa ni banda la Maliasili, kulikua na simba.

Tuliwasubiri kaka na dada wao walikuwa chipukizi. Walituringishia mchana walipewa wali na pofu.
 
Screenshot_20200204-134540.jpeg
tapatalk_1580804070179.jpeg


Jr
 
Namtakia kila la kheri mwenyekiti wa CCM Dr Magufuli

Nawatakia kila la kheri makamu mwenyekiti mzee Mangula, Katibu mkuu Dr Bashiru na sekretarieti yote

Namtakia kila la kheri kada mkongwe na asiyechoka mzee Mgaya

Nawatakia kila la kheri wanaccm wote

Mwisho lakini siyo kwa umuhimu nawatakia kila la kheri wapinzani wote kwa kuiunga mkono CCM na hasa Mzee Shibuda, mzee Cheyo, Prof Lipumba, KUB Mbowe ,mzee Mrema na James Mbatia

Mungu ibariki Tanzania na uibariki pia CCM!
Amen!
mfumo wa vyama vingi aliukubali akili kubwa mwalimu JKN.
hawa wengine wasingeweza kuruhusu na sasa hivi nchi yetu ingekuwa Somaliland. tumshukuru mwalimu!
 
Back
Top Bottom