Happy Birth Day to me

Mtoto wa Mkulima

JF-Expert Member
Apr 12, 2007
683
122
Eeee bwana leo 01 - 03 ni BD yangu na nimefikisha zaidi ya miongo kadhaa sasa naona ni vyema nijipongeze kwa hilo. Happy Birth dei to me!
 
Happy Birthday
75910467.jpg
 
THANX mkuu

Duh eee bwana nimekula namba zinakaribia kufikia umri wa uhuru wa taifa letu mzee.

Mkuu,
Simba wa vita (RMK) kala miongo 8 na ushee juzi. (Front picha Tanzania daima leo)
May you live to surpass that number by far.
Happy bday.
 
Eeee bwana leo 01 - 03 ni BD yangu na nimefikisha zaidi ya miongo kadhaa sasa naona ni vyema nijipongeze kwa hilo. Happy Birth dei to me!

What a coincidence! I am also celebrating my birthday today. Happy Birthday MWM. I am very old!....:)
 
What a coincidence! I am also celebrating my birthday today. Happy Birthday MWM. I am very old!....:)

Happy Birthday to you "Bubu ataka kusema".

BTW, How old are you guys (Bubu ataka kusema & Mtoto wa Mkulima)? Pick a box, 15-20, 20-25, 25-30, 30-35, 35-40, 40-45, 45-50, Above 50? (Joke, ignore me)

Happy Birthday.
 
Happy Birthday to you "Bubu ataka kusema".

BTW, How old are you guys (Bubu ataka kusema & Mtoto wa Mkulima)? Pick a box, 15-20, 20-25, 25-30, 30-35, 35-40, 40-45, 45-50, Above 50? (Joke, ignore me)

Happy Birthday.

Ongeza box nyingine mbili...:)
 
BUBU Happy birth day mkuu. Yeah is coincidence mtu wangu.

what a coincidence!!..........nimetoka kumwimbia mwanangu ambapo pia ni birthday yake leo!!! tar 1/March

Happy Birthday to you Mtoto wa mkulima na Bubu ataka kusema!!!
 
duh.. na miye nusura nimiss keki! Happy Birthday to both of you Bubu na Mtoto wa Mkulima; muishi na kuona tuliyoyaona ila msije kufanya tuliyoyafanya; na kwa heshima yenu nawapa kumbukumbu shairi hili lwa gwiji wa lugha yetu na mwalimu wangu Marehemu Shaaban Bin Robert;

Ujana kitu kitamu, tena ni azizi sana
Maungoni mwangu humu, nilikuwa nao jana
Kwa wingi katika damu, tahamaki leo sina!
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.


Kichwa kimejaa mvi, kinywani meno hamna
Nikenda kama mlevi, miguu nguvu haina
Kumbe ujana ni hivi, ukenda hauji tena!
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.


Jua langu limekuchwa, na nyota nilizoona
Ukinitizama kichwa, nywele nyeusi hakina
Kama zilizofikichwa,zikang'olewa mashina
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.


Natatizika kauli, midomo najitafuna
Nimekusanya adili, walakini hali sina
Dunia kitu bahili, hiki una kile huna!
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.


Nilikuwa ni waridi, furaha ya wasichana
Neno hawakunirudi, wakati wa kukutana
Sasa nanuka baridi, wanionapo waguna
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.


Walio wakinibusu, walikuwa wengi sana
Wanawake wenye busu, uzuri na usichana
Sasa sina hata nusu, ya wanitajao jina
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.


Wazuri wenye uturi, na mikono yenye hina
Kila mtu mashuhuri, alipenda kuniona
Nilifaa kwa shauri, na sasa sauti sina
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.


Dunia bibi arusi, kwa watu kila namna
Inapendeza nafsi, wakati wa kuiona
Na leo sina nafasi, kwa uzee kunibana
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.


Kilichokuwa gizani, niliweza kukiona
Nikakijua thamani, sura yake hata jina
Sasa sijui ni nini, hata ikiwa mchana
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.


Kilichotaka fikira, niliweza kukinena
Kwa mfano na kwa sura, mpaka kikafanana
Leo tazama hasara, nguvu hiyo sina tena
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.


Kilichotaka mapimo, sikifahamu mapana
Marefu yake na kimo, siifahamu bayana
Nusu nimo nusu simo, duniani najiona
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.


Hadumu nasikitika, rafiki yangu ujana
Machozi yamiminika, na la kutenda hapana
Ni wakati umefika, uzee dawa hauna
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.


Hauna dawa uzee, mabega yamepetana
Anionaye ni"wee!, ondoka hapa laana"
Wanaposema na miye, niliyekuwa na jina!
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana.


Wakatabahu shairi, uchungu wanitafuna
Walakini nafikiri, twafuata Subuhana
Katika ile amri, ya"kuwa"na "kutengana"
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom