Happy besdey to ME!

snochet

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
1,405
1,095
Ninapenda kumshukuru Mungu for a special day like this to me,kwa kuwa na uzima na afya njema.28th November ambapo nimetimiza miaka (kadhaa).na mwaka huu,birthday imenikuta mbali na home so ningependa nisherekee na wanaJF wenzangu na kuwatambua kwa wale niwapendao humu.kwanza naomba niutambue uwepo wa dada yangu Mwali,nakupenda sana,you have made me an incredible character(out of JF),kaka wa mbali watu8 The Boss AshaDii pretta Madame B, charminglady Arushaone Erickb52 Puppy Mzee wa Rula Mzee Mwanakijiji-ur articles rock me kila siku....my geeks MziziMkavu Paje e2themiza,mmenifundisha mengi sana... LARA1 FirstLady Zinduna Ciello Kaizer PakaJimmy,@figaniga Mtambuzi Bujibuji Boflo Bishanga Puppy Mfupa eka mangi,.....nina list ndefu sana ya ku-mention,ngoja niwahi kibaruani,nitaimalizia baadae kidogo.




karibuni haka ka-halfkeki,special for the JF people,nimekanunua kwa wakimbiza maboxi nikachomeka mishumaa tule wote humu
cupcake.jpg
tumblr_mdqjtoOQNd1rnnvr5o1_500.png
 
Last edited by a moderator:
Happy birthday to you, asante kwa kutukaribisha kakeki. Tule basi kabla wajuba hawajafika manake tutaambulia mishumaa tu.
 
Snochet Ninakupa Zawadi ya Happy Birthday yako Maisha yako ya baadae au maisha yako ya kila siku unatakiwa uwe hivi soma kwa makini sana.hii ndio nyota yako wewe Snochet NYOTA YA MSHALE (SAGITTARIUS)

NYOTA YA MSHALE (SAGITTARIUS)

  • Hii ni nyota ya tisa katika mlolongo wa nyota 12.
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 22 November na 21 December ya mwaka wowote.
  • Sayari yao ni Jupiter (Attarid).
  • Siku yao ya Bahati ni Alhamisi.
  • Namba yao ya Bahati ni 3.
  • Rangi yao ya Bahati ni Hudhurungi.
  • Asili yao ni MOTO.

KIPAJI CHA MSHALE (Prophetic)

Wenye nyota hii wana kipaji cha kutabiri na kujua mambo ambayo yatatokea mbele au muda utakaokuja, na mara nyingi wanalolisema huwa linatokea hata likiwa la kipuuzi.

TABIA ZA MSHALE


Wenye nyota ya mshale ni wenye tabia ya kuwa na matumaini ya mafanikio kwa lolote wanalolitegemea. Wanapenda kuwa na uhuru wa kupenda na kuchagua na wanapenda watu wengine wawe kama wao.

Hawapendi mambo nusunusu na ni watu ambao wako wazi na wanaopenda kusoma. Ni wakweli na ukitaka kuelewana nao na wewe uwe mkweli.
Ni watulivu na ni waaminifu na wanapenda uadilifu. Ni watu ambao hawapendi kuamrishwa kufanya jambo kwa sababu wanaamini kwamba wao wenyewe wana uwezo mkubwa wa kutekeleza jambo lolote, lakini likiwaudhi wanakuwa wakaidi na wasioweza kutii amri.
Wenye nyota hii hawaoni taabu kusema lolote bila kujali athari zake mradi jambo hilo liwe la kweli.

TABIA YA MSHALE KATIKA MAPENZI


Pamoja na kwamba wenye nyota hii wanapenda wawe huru na wenye kujiamulia mambo yao wenyewe huwa wana starehe na kuona raha wanapokuwa ndani ya uhusiano wa kimapenzi.

Wenye nyota hii wanapenda sana kujihusisha na makundi makundi lakini huwa wanapata muda wa kuwa na wapenzi wao. Ni watu wachangamfu na wenye kupenda lakini tabia yao ya kutojali inawafanya wapenzi wao wajione kwamba wanakosa ulinzi wa kimapenzi.

Wanapoingia katika mapenzi wanakuwa waaminifu. Mwanzoni wanakuwa wagumu sana kujihusisha. Wanapenda sana wakati wote kuwa na wapenzi wapya au mapenzi ya kawaida kwa sababu wanaamini mapenzi ya kudumu yanawanyima uhuru.


Wapenzi wao wanaponyesha dalili ya kuwapenda basi wao huwa wanajiondoa kwa hofu ya kubanwa na kutokuwa na uhuru.

Ni watu wanaopenda kufanya ngono kwa muda mrefu na hisia zao ziko mbali na inashauriwa kwamba wapenzi wao wawe wamekula kabla ya tendo la ndoa vinginevyo itakuwa taabu.
{mospagebreak}

TABIA YA MSHALE KATIKA FEDHA


Alama ya nyota hii ni Mshale na mategemeo yao ya kifedha yanalenga mbali na juu sana.

Wenye nyota hii fedha kwao ndio njia pekee ya kujikomboa na kupata uhuru hivyo wako tayari kufanya jambo lolote hata kama ni la hatari ili wapate fedha na wanapozipata huzitumia bila mpangilio.
Mara nyingi huwa hawapendi kutafuta fedha zao katika njia za kawaida wanapenda sana kutumia njia tofauti na kubuni mbinu mbali mbali kutekeleza malengo yao.
Ni watu ambao hawaoni haya kumtumia mtu mwenye pesa au uwezo ili watekeleze malengo yao. Kwa sababu hii wengi wao wanakuwa matapeli.
Matatizo yao makubwa ni kwamba wao ni watumiaji wabaya na hawana mipango thabiti ya matumizi ya fedha na ni watu ambao wakitoa ahadi ya fedha hawatekelezi.

MAVAZI YA MSHALE

Wenye nyota ya Mshale wanatakiwa wavae nguo zenye kuathiri na za mzaha mzaha kama koti au blauzi isiyo rasmi au nguo za kitamaduni zilizoongezwa ongezwa vitu vingi kama maua au nakshi nakshi.
Rangi ya nguo zao iwe ya Zambarau au rangi ya Hudhurungi iliyochangamka au rangi ya blue.
Vitambaa viwe vya sufu. Nguo ziambatane na mikanda, na viatu viwe vya buti.Wanawake wapendelee kuvaa sketi.

MATATIZO YA KIAFYA:

Nyota hii inatawala sehemu ya chini ya kiuno. Wenye nyota hii hawapendi kuugua. Lakini huwa wanapata maradhi kutokana na kujishughulisha kupita kiasi na kutumia nguvu zao na akili zao kwa muda mrefu bila mapumziko. Wanathamini sana mizunguko kuliko mapumziko.
Vile vile ni watu wasiopenda ushauri kuhusiana na afya zao.
Tatizo lao lingine ni kuwa wanapenda sana kula na kunywa na hiyo huwaletea unene usiotakiwa. Wakitaka kujikomboa na matatizo wanashauriwa wawe na tabia ya kujipumzisha.
Magonjwa yanayohusiana na nyota hii ni majereha na maradhi ya nyonga, mapaja, maradhi ya ini (Liver Disorder) kupooza kwa miguu (paralysis of limbs) na ugonjwa wa kuumwa mishipa au misuli ya nyuma ya paja.

KAZI YA MSHALE

Kupata au kukosa, kushinda au kupoteza, kuna uchangamfu wa asili kwa nyota hii na uzoefu katika hali yeyote.
Ni watu waaminifu wanaopenda sana mafankio na wako tayari wakati wowote katika kazi. Kutokana na hili wanakuwa na bahati ya kuwa katika sehemu muafaka na katika muda unaotakiwa.
Wenye nyota ya Mshale ni wafanyakazi waaminifu na hawapendi kuwasimamia watu katika kazi. Ni wenye kuwaamini wafanyakazi wao na wanapokuwa ofisini huleta mazingira ya urafiki na kuaminiana.
Kazi zinazowafaa ni za usafiri, kazi za sheria, Wakili au Hakimu, kazi za uandishi, ualimu, dini, sheikh au padri au makanisani au misikitini, michezo, kazi za kijeshi na uuzaji.
{mospagebreak}

FAMILIA ZA MSHALE

Wazazi wenye nyota ya Mshale ni wenye kuwachangamsha sana watoto wao. Nyumba zao zinakuwa zinajaa vitabu na vifaa mbali mbali na wanawahimiza sana watoto wao wawe huru na majasiri.
Wenye nyota hii wanapenda kuwatembeza watoto wao katika sehemu za elimu, kama vile, Makumbusho au sehemu za kihistoria.
Elimu na masomo hupewa kipaumbele na mzazi mwenye nyota ya mshale ambaye mara nyingi huhakikisha mtoto wake anasoma. Wazazi hawa wanapata matatizo makubwa kuwadhibiti watoto wasiosikia kwa sababu wao wenyewe wanapenda uhuru kwa sababu hii huwa wanavumilia tabia mbaya za watoto wao hata watoto wakiwa wajeuri.

MADINI YA MSHALE

Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa SAPPHIRE. Mawe haya nyenye rangi ya bluu yana uwezo mkubwa wa kinyota wa kumletea mvaaji afya nzuri, nguvu na kinga vitu ambavyo wenye nyota hii wanavihitaji.

UHUSIANO WA KIMAPENZI


(Mshale na Mapacha)

Tabia ya kufanya mambo haraka haraka au kukata tamaa na kupenda kuelewa mambo ya wenye nyota ya Mapacha inaingiliana vizuri na wenye nyota ya Mshale ambao ni wenye busara na subira na wasiokata tamaa.

VYAKULA VYA MSHALE

Wenye nyota hii wanashauriwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao. Nyama mwitu, kunazi za rangi ya bluu, maboga na juice ya mapera.

NCHI ZA MSHALE

Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota zao.
Nchi hizo ni USA na SPAIN na miji ni Budapest (Romania) na Cologne (Ujerumani).

RANGI ZA NYOTA

Wenye nyota hii wanatakiwa wapake nyumba zao au vyumba vyao au sehemu zao za biashara rangi zenye kusisimua na uchangamfu na zinazoashiria hali ya kumkaribisha mgeni.
Rangi hizo ni Nyekundu iliyochangamka (Warm Red) rangi ya Zambarau (Purple) na rangi ya hudhurungi au kahawia (Brown).

Hii ni zawadi toka kwangu juu yako mkuu snochet
 
Last edited by a moderator:
snochet, Mungu akupe haja za moyo wako, akuongezee miaka hapa duniani na zaidi ya yote Happy Birthday To You on your special day!
 
Last edited by a moderator:
Happy Birthday snochet Mungu azidi kukupa maisha marefu yenye baraka tele!!!
 
Last edited by a moderator:
Happy birthday snochet
Mungu akuongee furaha na maisha marefu na ya upendo!

Naomba kumwomba dada yangu kipenzi AshaDii awe mwenyekiti wa sherehe hii na hivyo awateuwe wanakamati kuanza maandalizi.
N.B
Naomba sweetlady na cielo muandae cake ya ukweli na Nicas Mtei andaa card nzuri kubwa ya mtoto huyu alozaliwa leo.
snowhite na Mamndenyi hakikisheni mtoto anaoga na kupendeza.
 
Last edited by a moderator:
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom