Hapo zamani... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hapo zamani...

Discussion in 'Entertainment' started by Ibrah, Feb 13, 2009.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Nimeanzisha thread hii baada ya kutafakari mambo mengi sana ya zamani na wakati huohuo nikitafakari hali ya sasa katika nyanja mbalimbali za maisha yetu Watanzania.

  Nawakaribisha wana JF kupost mambo ya zamani tunayoyakumbuka.
   
 2. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Hapo zamani, kujiunga na shule za Sekondari za Serikali ilikuwa ujiko mkubwa sana maana shule hizo zilikuwa na kiwango cha juu ukilinganisha na shule binafsi (ondoa seminari).

  Nakumbuka ilinipasa kurudia shule ili niweze kufauli kwa kuchaguliwa kwenda shule ya Seikali. Nilipomaliza mara ya kwanza 1985, sikuchaguliwa ikabidi nirudie na ndiposa nikafaulu na kujiunga na Shule ya Serikali. Ilikuwa Bonge la Ujiko!

  Hivi sasa wazazi hawataki watoto wao wajiunge na shule za Serikali hata kama wakifaulu, wenye uwezo huwapeleka shule za private za gharama kubwa maana inasemekana elimu inayotolewa na shule hizo ni ya hali ya juu kuliko inayotolewa na shule za Serikali.
   
Loading...