Hapo vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hapo vipi?

Discussion in 'Jamii Photos' started by Invisible, Jun 2, 2010.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Jun 2, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 2. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duh, hii picha inasema mambo mengi!!

  1. Kuna wanaume wawili wanatuonesha chupi zao, hapo suruali ikimshuka mmoja zaidi inabidi ategee wenzake apandishe kwanza

  2. Abiria bado wamo ndani ya gari!! Kuna kipepsi cha mtu kimechomoza dirishani

  3. Hili basi linauzwa, kuna tangazo hapo kwenye kioo cha nyuma. Nadhani mwenyewe alishashtukizia ubovu

  4. Mmoja tu kati ya hao wanaosukuma gari ndiye anayeonekana walau msafi, labda ni mmoja wapo wa abiria, hao wengine ni utingo, kondakta, mpiga debe nk
   
 3. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #3
  Jun 2, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Mkuu umegusa mengi kati ya yaliyo kichwani mwangu; naamini kuna watakaogusa zaidi... Picha hii inajenga mengi vichwani!
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Picha inaonesha jinsi CCM na serikali yake ilivyofanikiwa kuweka maisha bora kwa kila mtanzania toka Kiwete aingie madarakani!!
   
 5. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #5
  Jun 3, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Jamani kwa usawa huu tutafika kweli?
   
 6. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Picha hii inaonyesha ni jinsi gani polisi wa usalama barabarani wanavyozembea na kuacha magari yasiyonasifa ya kubeba abiria kuendelea kuhatarisha usalama wa wananchi na mali zao.
   
 7. kmp

  kmp Member

  #7
  Jun 3, 2010
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  AK 47 umesahau ule usemi usemao "mazoea hujenga tabia"?
   
 8. Ambassador

  Ambassador JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2010
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 932
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Bila shaka huyo aliyeko katikati (wa pili kutoka kulia, mwenye Tshirt ya blue) ndie konda. Si uancheki ameshikilia ankra mkono wa kushoto?
   
 9. M

  Magezi JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  mkuu hapo limebuma na mafuta ya kidebe
   
 10. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Wanafanya makusudi! Wanafanya makusudiiii! Kuacha magari mabovu njiani. Serikali ya mkwere!
   
 11. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,427
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kibongobongo iko poa. Maisha bora kwa kila M-Tz ndo hayo.
   
 12. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  1. yawezekana kabisa gari lilimetoka gereji na dereva akaamua kusanya wakati wa kufanyia majaribio.
  2. staili inayotumika kusukuma inaonyesha ni kana kwamba jamaaa wametumia muda mrefu kulikwamua lakini mashine haiendi..hapo wanatafuta tu sehemu ya kuipaki.
  3. Kila mmoja ni kama anahisia za mbali sana kwani wote wainamisha vichwa chini. Lakini kwa upande wa Konda sina shaka anafikiria jinsi gani biashara ya siku ilivyobuma na uwezekano mkubwa wa kurejesha mafao ya abiria.
  4. Huyo jaamaa wa kwanza kushoto yaonyesha ni mtanashati na anapenda kuchomeka kwa staili ya kipapaaa, (shati ndani ya kufuli kisha unapiga, short na suluali juu). Shati ikivuta juu kama hivi, inavuta na mambo yote ya ndani na kuweka hadharani.
  5. Kwa kuwa wanafunzi upenda kupanda DCM, na hapa haonekani kuwepo student kwenye kutoa tafu, ni kiashirio pia kuwa hilo daladala ni yale ambayo madereva wake hawataki kubeba wanafunzi kama sio yanayokatiza katiza rutis kwa kukwepa wanafunzi.
  6. Kwa kuwa bado kuna watu ndani ya gari wakati wengine wanahangaika, inaonyesha ni jinsi gani viumbe wengine wanavyopenda starehe hata kwenye matatizo hasa wa jinsia ya upande wa pili ambayo haipo kwenye safu.
   
 13. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #13
  Jun 4, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Kinachonishangaza pia ni kua mbona abiria hawashuki ili uzito upungue wakati wa kusukuma hilo gari?
  Yaani watu wanne wanasukuma gari lenye tani kibao na watu juu?...kipepsi unakiona hapo dirishani!...Jamaa hata hana habari na dhiki wanayopata wanaosukuma gari.

  Waliomo ndani pia need to be called out for their lack of compassion....ama ndivyo tulivyo?
  We simply dont care!
   
 14. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #14
  Jun 4, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Duh!...nilikua sijaona hio 'for sale' sign. Kweli mwenye gari anajua lishachoka....Hii ndio ile unasikia "Buyer beware".
   
 15. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2010
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Umesahau mteja ni mfalme, kibaya zaidi abiria wana hasira na makonda kwa lugha chafu na jeuri, wametuli tuli kieleweke kitu.
   
 16. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  halafu huyo wa kwanza kulia anategea tehe tehe. waangalia tu ushuzi usiwatoke. ha ha ha
   
 17. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #17
  Jun 6, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Ukiangalia picha kwa haraka kuna vitu ni vigumu kuviona!

  Mfano:

  [​IMG]
   
 18. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  kuna mjamaa juu ya ukuta anataka kurudishia kitambaa kilichoanguka wakati hakuna mtu wa kumpa hicho kitambaa.
  Ngazi mbili nyekundu na nyingine kulia kwake.
   
Loading...