G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,596
- 36,018
Hivi leo hii kampuni za simu zikianza kushurutishwa kutoa mawasiliano ya wateja wao, kina nani watabaki salama?
Ninachojua ni kuwa mkataba mkubwa sana kati ya hizi kampuni za simu (duniani) na wateja wao ni kulinda usalama wa wateja wao kwa namna yoyote ile.
Ipo mipaka ambayo kwa kweli kampuni za simu duniani hulazimishwa sana kutoa taarifa za wateja wao lakini si kwa hili la Neema Lema na Mrisho Gambo ambayo ni majadiliano binafsi (? )
Sasa tunavyosema kuwa nchi yetu imeingia kwenye mfumo rasmi wa udikteta mtuelewe! Kampuni ya Apple ilikataa katakata kutoa mawasiliano muhimu sana ya mteja wao kwa kuwa ni sawa na kujitia kitanzi kibiashara, sheria zikaangaliwa na ikaonekana kuwa Apple wanayo haki ya kumlinda mteja wao. Mbona hawakukurupuka kama hawa VodaCom?
Leo kampuni ya VodaCom inashurutishwa na mahakama ya hakimu mkazi kutoa siri za mawasiliano tena kwa upande mmoja, vipi mke wa Lema (Neema Lema) akija na madai kuwa alikuwa akiambiwa maneno ya kuhatarisha ndoa yake na huyo Mrisho Gambo je kampuni hiyohiyo itakuwa tayari kutoa mawasiliano?
Kampuni ya VodaCom ama kwa kikundi cha watu au huyo anayeenda kutoa ushahidi ni lazima ijichunguze na imchunguze huyo mtu. Pia ijiridhishe yenyewe kama kampuni ya kimatafia kuwa ni sahihi kutoa siri za wateja wake kwa njia nyepesinyepesi na kesi nyepesinyepesi zilizotawaliwa na chuki za kisiasa kama ya Lema. Kuna hongo au ahadi ya ulaji kwa huyo mtu au watu?
Hili kampuni ya VodaCom kwa sasa haiwezi kuliona hili lakini nawahakikishia kuwa kwa kujirahisisha kwao huko ni lazima iwagharimu mbeleni! Kampuni ya VodaCom ni ya kimataifa na hivyo inatakiwa kuegemea kwenye sheria za kimataifa na siyo kujigawa kama inavyoonekana sasa.
Waangalie mfano kwa Jamii Forum ambao nao walitishwa na kupewa kila aina ya ushawishi ili kutoa siri za watu wake, lakini wao walisimamia sheria zao za kimataifa! VodaCom naomba niwaeleze kuwa, kesi ya Lema ni ya maslahi ya kisiasa ambapo baadhi ya makuhadi wa kisiasa na wasiofuta weledi wameamua kwa dhati kabisa kuukomesha ubunge wa Godbles Lema kabla mwaka huu haujisha. Msijihusishe kwenye mambo hayo ambayo yataidhalilisha taaluma yenu ya kibiashara. Wakati unasema!