Hapana kwa baadhi ya mambo ndani rasimu ya katiba mpya-2103


M

Mp Kalix2

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2010
Messages
5,849
Likes
1,716
Points
280
M

Mp Kalix2

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2010
5,849 1,716 280
Kusema kweli Rasimu ya Katiba mpya ina mapungufu mengi ukiacha kosa la msingi la kuleta serikali Tatu lakini kuna hili ambalo limefichwa ndani ya hizo kurasa 240.Watanganyika na Wazanzibari wanatakiwa kupitia kipengele moja baada ya nyingine.

Tunarudishwa kule kule kupitia mlango wa Nyuma.

[FONT=&amp]Kupitishwa[/FONT]

[FONT=&amp]kwa hoja[/FONT]

[FONT=&amp]za SerikaliKupitishwa[/FONT]
[FONT=&amp]kwa hoja[/FONT]
[FONT=&amp]za Serikali[/FONT]
[FONT=&amp]115.-[/FONT][FONT=&amp](1) Endapo Bunge halitaridhishwa na mchanganuo au[/FONT]
[FONT=&amp]mgawanyo wa hoja ya Bajeti iliyowasilishwa na serikali, Bunge linaweza[/FONT]
‐ 47 ‐
[FONT=&amp]kurudisha hoja kuhusu Bajeti ya Serikali pamoja na mapendekezomahsusi[/FONT]
[FONT=&amp]kuhusiana na upungufuuliobainika.[/FONT]
[FONT=&amp](2) Serikali itawajibika kuyafanyia kazi mapendekezo ya Bunge kwa[/FONT]

[FONT=&amp]kadri itakavyowezekana na kisha kuwasilisha tena Bungeni hoja husika[/FONT]
[FONT=&amp]pamoja na maelezo ya utekelezaji wa maelekezo ya Bunge na endapo Bunge[/FONT]
[FONT=&amp]litakataa kwa mara ya pili hoja kuhusu Bajeti ya Serikali, basi hoja hiyo[/FONT]
[FONT=&amp]itahesabika kuwa imepitishwa na Bunge.[/FONT]

Updates;
Maoni binafsi ndani ya Rasimu kadri muda utakavyoruhu.

[FONT=&amp]2. [/FONT][FONT=&amp]Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara ikijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar ikijumuisha sehemu yake ya bahari.[/FONT]
2. Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanganyika ikijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar ikijumuisha sehemu yake ya bahari.


[FONT=&amp]9[/FONT][FONT=&amp].-(1) Mtu au kikundi cha watu hakitachukua au kushikilia mamlaka ya nchi isipokuwa kwa mujibu wa Katiba hii.[/FONT]

(2) Kitendo chochote kinachokiuka masharti ya Ibara ndogo ya (1) ni batili na ni kitendo cha uhaini kama itakavyoelezwa katika sheria za nchi.
9.-(1) Mtu au kikundi cha watu hakitachukua au kushikilia mamlaka ya nchi (Serikali, Bunge na Mahakama) isipokuwa kwa mujibu wa Katiba hii.

(2) Kitendo chochote kinachokiuka masharti ya Ibara ndogo ya (1) ni batili na ni kitendo cha uhaini isipokuwa Maandamano yoyote ya Amani ya Umma ya kudai haki au kuondoka madarakani kwa maamlaka ya Nchi hayatachukuliwa kuwa ni Uhaini.


[FONT=&amp]10.[/FONT][FONT=&amp]-(1) Malengo ya Taifa yaliyoainishwa ndani ya Katiba hii yatakuwa ni mwongozo kwa Serikali, Bunge, Mahakama, vyama vya siasa, taasisi, asasi na mamlaka nyingine na kwa kila mwananchi katika matumizi au kutafsiri masharti ya Katiba hii au sheria nyingine yoyote na katika utekelezaji wa uamuzi wa kisera kwa madhumuni ya kujenga jamii huru, makini na iliyo bora.[/FONT]

[FONT=&amp](2) Serikali itatoa taarifa Bungeni si chini ya mara moja katika kila mwaka, kuhusu hatua zilizochukuliwa na mamlaka ya nchi ili kuhakikisha utekelezaji wa malengo ya Taifa yaliyoainishwa katika Katiba hii.[/FONT]
10.-(1) Malengo ya Taifa yaliyoainishwa ndani ya Katiba hii yatakuwa ni mwongozo kwa Serikali, Bunge, Mahakama, vyama vya siasa, taasisi, asasi na mamlaka nyingine na kwa kila mwananchi katika matumizi au kutafsiri masharti ya Katiba hii au sheria nyingine
yoyote na katika utekelezaji wa uamuzi wa kisera kwa madhumuni ya kujenga jamii huru, makini na iliyo bora.
[FONT=&amp](2) Serikali itatoa taarifa Bungeni si chini ya mara moja katika kila mwaka, kuhusu hatua zilizochukuliwa na mamlaka ya nchi ili kuhakikisha utekelezaji wa malengo ya Taifa yaliyoainishwa katika Katiba hii na Bunge litapewa nafasi ya kuijadili na kupiga kura ya kuikubali au kuikataa taarifa husika kwa kutumia Kanuni ya Bunge katika kufikia maamuzi .[/FONT]

[FONT=&amp] [FONT=&amp]11.[/FONT][FONT=&amp]-(1) Lengo Kuu la Katiba hii ni kulinda, kuimarisha na kudumisha udugu, amani, umoja na utengamanowa wananchi wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia ustawi wa wananchi na kujenga Taifa huru lenye demokrasia, utawala bora na kujitegemea.[/FONT]

[FONT=&amp](2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), lengo hilo kuu litaendelezwa na kuimarishwa katika nyanja zote kuu,ikijumuisha nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na[/FONT]
[FONT=&amp]kimazingira.[/FONT]
[FONT=&amp](3) Katika kutekeleza malengo ya Taifa ya:[/FONT]

[FONT=&amp](c) kiuchumi, Serikali inachukua hatua zinazofaa ili:[/FONT]
[FONT=&amp](i) kuwaletea wananchi maisha bora kwa kuondoa umaskini;[/FONT]
[FONT=&amp](ii) kuhakikisha kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha[/FONT]
[FONT=&amp]kuwa utajiri wa Taifa unaendelezwa,unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya [/FONT][FONT=&amp]wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine;[/FONT]

[FONT=&amp](iii) kuweka mazingira bora kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza vyombo vya uwakilishi wa wakulima,wafugaji na wavuvi;[/FONT]
[FONT=&amp](iv) kuweka mazingira bora ya kufanya biashara na kukuza fursa za uwekezaji;[/FONT]
[FONT=&amp](v) kuweka mazingira bora kwa ajili ya kukuza kilimo, ufugaji na uvuvi kwa kuhakikisha kuwa [/FONT][FONT=&amp]wakulima, wafugaji na wavuvi wanakuwa na ardhi na nyenzo kwa ajili ya kuendeleza shughuli[/FONT]

[FONT=&amp]zao;[/FONT]

[FONT=&amp](vi) kuweka mazingira bora ya uzalishaji wa mazao kwa wakulima, wafugaji na wavuvi, utafutaji na uendelezaji wa masoko ya mazao yao;[/FONT]
[FONT=&amp](vii) kuweka utaratibu mzuri wa upangaji na usimamiaji wa mizania ya bei za mazao na[/FONT]
[FONT=&amp]pembejeo;[/FONT]
[FONT=&amp](viii) kuimarisha na kuendeleza uwekezaji wa ndani,upatikanaji wa pembejeo za kilimo, maeneo ya ufugaji na vifaa vya uvuvi;[/FONT]
[FONT=&amp](ix) kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa fursa na nafasi za wazi kwa watu wote na kuanzisha shughuli za kiuchumi na kukuza mazingira yaliyobora kwa ajili ya kuhamasisha sekta binafsi katika uchumi;[/FONT]
[FONT=&amp](x) kuhakikisha kuwa kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anapata fursa ya kufanya kazi, kwa maana ya kufanya shughuli yoyote halali inayompatia kipato;[/FONT]
[FONT=&amp](xi) kuweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kujipatia [/FONT][FONT=&amp]elimu na kuwa huru kupata fursa sawa ya kutafuta elimu katika fani anayoipenda hadi[/FONT] [FONT=&amp]kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake;[/FONT]


[/FONT]
11.-(1) Lengo Kuu la Katiba hii ni kulinda, kuimarisha na kudumisha udugu, amani, umoja na utengamano wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzingatia ustawi wa wananchi na kujenga Taifa huru lenye demokrasia, utawala bora na kujitegemea.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), lengo hilo kuu litaendelezwa na kuimarishwa katika nyanja zote kuu,ikijumuisha nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na
kimazingira.

(3) Katika kutekeleza malengo ya Taifa ya:


(c) kiuchumi, Serikali inachukua hatua zinazofaa ili:
(i) kuwaletea wananchi maisha bora kwa kuondoa umaskini;

(ii) kuhakikisha kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha
kuwa utajiri wa Taifa unaendelezwa,unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine;

(iii) kuweka mazingira bora kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza vyombo vya uwakilishi wa vikundi vya shughuli za Kiuchumi na kuwashirikisha katika hatua za kuandaa sera na Kanuni za shughuli husika.

(iv) kuweka mazingira bora ya kufanya biashara na kukuza fursa za uwekezaji;

(v) Kupitia Serikali za Washirika wa Muungano Serikali itaweka mazingira bora kwa ajili ya kukuza kilimo, ufugaji na uvuvi kwa kuhakikisha kuwa wakulima, wafugaji na wavuvi wanakuwa na ardhi na nyenzo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao;

(vi) kuweka mazingira bora ya uzalishaji wa mazao kwa wakulima, wafugaji na wavuvi, utafutaji na uendelezaji wa masoko ya mazao yao;

(vii) kuweka utaratibu mzuri wa upangaji na usimamiaji wa mizania ya bei za mazao zitokanazo na shughuli za uchumi hasa kilimo,Ufugaji na Uvuvi .

(viii) kuimarisha na kuendeleza uwekezaji wa ndani kwa kuhakikisha ,upatikanaji wa Mitaji kwa ajili ya pembejeo za kilimo, madawa na majasho ya Mifugo na vifaa vya uvuvi;

(ix) kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa fursa na nafasi za wazi kwa kila mmoja kuanzisha shughuli za kiuchumi kwa kukuza mazingira yaliyo bora kwa ajili ya kuhamasisha sekta binafsi katika uchumi;

(x) kuhakikisha kuwa kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anapata fursa ya kufanya kazi, kwa maana ya kufanya shughuli yoyote halali inayompatia kipato;

(xi) kuweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kujipatia
elimu na kuwa huru kupata fursa sawa ya kutafuta elimu katika fani anayoipenda hadi
kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake;

(xii) Serikali itahakikisha mkataba wowote utakaoingiwa na Serikali au taasisi zake na Serikali zingine au Makampuni binafsi unakuwa wa wazi kwa kuweka nakala ya mkataba husika kwenye magazeti na Tovuti ya Wizara/taasisi husika isipokuwa mikataba ya Ulinzi ambao Kamati ya Bunge ya Ulinzi ndiyo itakayo kuwa na Mamlaka ya kukagua kabla Mkataba wenyewe hauja sainiwa kuona kama masilahi ya Taifa yamezingatiwa au lah na kama Mkataba haukuzingatia masilahi ya Taifa Kamati itatoa mapendekezo ya kuzingatiwa na Wizara husika na Nakala kupewa Spika wa Bunge.
[FONT=&amp]
[/FONT]
[FONT=&amp]16.[/FONT][FONT=&amp]-(1) Kiongozi wa Umma atalazimika kutangaza, ndani ya siku thelathini baada ya kupata uongozi na baada ya kuacha uongozi,mali na thamani zake na madeni yake katika Tume ya Maadili na Uwajibikaji.[/FONT]

[FONT=&amp](2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), Kiongozi wa Umma atalazimika kutangaza mali zake na madeni:[/FONT]
[FONT=&amp](a) yake binafsi;[/FONT]
[FONT=&amp](b) ya mwenza wake wa ndoa; na[/FONT]
[FONT=&amp](c) watoto wake walio chini ya umri wa miaka kumi na nane,mara moja kila mwaka, au kadri itakavyoamuliwa na sheria.[/FONT]
16.-(1) Kiongozi wa Umma atalazimika kutangaza, ndani ya siku thelathini baada ya kupata uongozi na baada ya kuacha uongozi,mali na thamani zake na madeni yake katika Tume ya Maadili na Uwajibikaji.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), Kiongozi wa Umma atalazimika kutangaza mali zake na madeni:

(a) yake binafsi;

(b) ya mwenza wake wa ndoa; na

(c) watoto wake walio chini ya umri wa miaka kumi na nane,mara moja kila mwaka, au kadri itakavyoamuliwa na sheria.

(d) Utangazaji wa Mali za kiongozi kupitia kifungu cha 16(2); a na b ya Katiba hii utafanywa chini ya Kiapo na itakuwa Kosa la jinai kusema uongo.

(e) Bunge litatunga sheria itakayo simamia na kuwezesha Umma kuweza kuhakiki ukweli wa mali zilizotangazwa na Kiongozi wa Umma.[FONT=&amp]19. [/FONT][FONT=&amp]Masharti yaliyoainishwa katika Ibara za 13 mpaka 18 yatatumika pia kwa watumishi wa umma baada ya kufanyiwa marekebisho stahiki.[/FONT]


19. Masharti yaliyoainishwa katika Ibara za 13, 18 na 20 ya Katiba hii yatatumika pia kwa watumishi wa umma na Bunge kupitia Sheria ya Tume ya Maadili ya Uongozi wa Umma itatunga Kanuni itakayosimamia Masharti ya Katiba hii.

20.-(1) Bila ya kuathiri masharti yoyote ya Katiba hii, kiongozi yeyote wa Umma atapaswa kuheshimu na kutii maadili ya viongozi
wa umma, ikiwemo Miiko ya Uongozi.
(2) Miiko ya Uongozi inayorejewa katika Ibara ndogo (1),itakuwa kama ifuatavyo:
(a) Kiongozi wa umma hatopaswa:
(i) kuvunja au kukiuka masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano;
(ii) kutoa au kupokea rushwa;
(iii) kujilimbikizia mali kinyume cha sheria;
(iv) kusema uongo au kutoa taarifa zisizo za ukweli;
(v) kutoa siri za Serikali kinyume na sheria;
(vi) kutumia wadhifa, nafasi au cheo chake kwa manufaa yake binafsi, familia yake, ndugu, jamaa
au marafiki zake au mtu yeyote aliye na uhusiano naye wa karibu;
(vii) kufanya vitendo vya uzembe, uvivu, ubaguzi,kiburi, dharau au unyanyasaji wa kijinsia.20.-(1) Bila ya kuathiri masharti yoyote ya Katiba hii, kiongozi yeyote wa Umma atapaswa kuheshimu na kutii maadili ya viongozi wa umma, ikiwemo Miiko ya Uongozi.


(2) Miiko ya Uongozi inayorejewa katika Ibara ndogo (1),itakuwa kama ifuatavyo:(a) Kiongozi wa umma hatopaswa:(i) kuvunja au kukiuka masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano;(ii) kutoa au kupokea rushwa;


(iii) kujilimbikizia mali kinyume cha sheria;(iv) kusema uongo au kutoa taarifa zisizo za ukweli;(v) kutoa siri za Serikali kinyume na sheria isipokuwa zilizokinyume na Masilahi ya Umma kadri katiba hii ilivyoelekeza;(vi) kutumia wadhifa, nafasi au cheo chake kwa manufaa yake binafsi, familia yake, ndugu, jamaa au marafiki zake au mtu yeyote aliye na uhusiano naye wa karibu;(vii) kufanya vitendo vya uzembe, uvivu, ubaguzi,kiburi, dharau au unyanyasaji wa kijinsia.21.-(1) Mtumishi wa umma aliye katika ajira ya kudumu hataruhusiwa kuingia katika ajira nyingine yoyote yenye malipo ya
mshahara.
(2) Mtumishi wa umma haruhusiwi kuchaguliwa au kuteuliwa kushika madaraka katika chama cha siasa.
(3) Mtumishi wa umma aliyestaafu na anayepokea malipo ya pensheni kutokana na fedha za umma haruhusiwi kuwa mwenyekiti,
mkurugenzi au mtumishi zaidi ya vipindi viwili katika:
(a) shirika au kampuni inayomilikiwa au kuendeshwa kwa fedha za umma; au
(b) chombo chochote cha umma.

[FONT=&amp]
21[/FONT]
.-(1) Mtumishi wa umma aliye katika ajira ya kudumu hataruhusiwa kuingia katika ajira nyingine yoyote yenye malipo ya mshahara.

(2) Mtumishi wa umma haruhusiwi kuchaguliwa au kuteuliwa kushika madaraka katika chama cha siasa .
(3) Mtumishi wa umma aliyestaafu na anayepokea malipo ya pensheni kutokana na fedha za umma anaruhusiwa tu kuwa Mwenyekiti na si kwa zaidi ya vipindi viwili vya jumla ya miaka kumi katika;

(a) shirika au kampuni inayomilikiwa au kuendeshwa kwa fedha za umma; au

(b) chombo chochote cha umma.

(4) Mtumishi wa Umma aliyestaafu na kuwa Mwenyekiti kwa mujibu wa Ibara hii baada ya kumaliza vipindi vyake vya kuwa Mwenyekiti hatabadilishiwa aina ya Pensheni badala yake atabaki na kuendelea kupokea Pensheni yake ya utumishi wa awali.Updates;

[FONT=&amp]24.-[/FONT][FONT=&amp] (7) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria,mamlaka ya nchi itaweka utaratibu unaofaa na unaozingatia misingi kwamba -[/FONT]

[FONT=&amp](a) wakati haki na wajibu kwa mtu yeyote vinapohitajika kufanyiwa uamuzi na mahakama au mamlaka nyingine inayohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia atakuwa na haki ya kukata rufani au kupata nafuu nyingine ya kisheria[/FONT]
[FONT=&amp]kutokana na uamuzi wa mahakama au mamlaka nyingine inayohusika;[/FONT]
[FONT=&amp](b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu aliyehukumiwa kwa kutenda kosa hilo hadi itakapothibitika mahakamani kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo;[/FONT]
[FONT=&amp](c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu ya kitendo chochote ambacho wakati alipotenda kitendo hicho hakikuwa ni kosa chini ya sheria;[/FONT]
[FONT=&amp](d) ni marufuku kwa mtu kupewa adhabu ambayo ni kubwa kuliko adhabu iliyokuwapo wakati kosa linalohusika lilipotendeka;[/FONT]
[FONT=&amp](e) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wa binadamu,heshima ya mtu na faragha itahifadhiwa katika shughuli zote zinazohusu upelelezi wa tuhuma na uendeshaji wa masharti ya jinai na katika shughuli nyingine ambazo mtu anakuwa katika kizuizi cha mamlaka ya nchi au katika[/FONT]
[FONT=&amp]kuhakikisha utekelezaji wa adhabu; na[/FONT]
[FONT=&amp](f) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazotweza au kudhalilisha.[/FONT]

24.-(7) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria,mamlaka ya nchi itaweka utaratibu unaofaa na unaozingatia misingi kwamba -


(a) wakati haki na wajibu kwa mtu yeyote vinapohitajika kufanyiwa uamuzi na mahakama au mamlaka nyingine inayohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia atakuwa na haki ya kukata rufani au kupata nafuu nyingine ya kisheria

kutokana na uamuzi wa mahakama au mamlaka nyingine inayohusika;

(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu aliyehukumiwa kwa kutenda kosa hilo hadi itakapothibitika mahakamani kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo;


(c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababu ya kitendo chochote ambacho wakati alipotenda kitendo hicho hakikuwa ni kosa chini ya sheria;


(d) ni marufuku kwa mtu kupewa adhabu ambayo ni kubwa kuliko adhabu iliyokuwapo kisheria wakati kosa linalohusika lilipotendeka;(e) haki ya usawa wa binadamu,heshima ya mtu na faragha itahifadhiwa katika shughuli zote zinazohusu upelelezi wa tuhuma na uendeshaji wa masharti ya jinai na katika shughuli nyingine ambazo mtu anakuwa katika kizuizi cha mamlaka ya nchi au katika kuhakikisha utekelezaji wa adhabu; na(f) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazotweza au kudhalilisha.
[FONT=&amp]29.[/FONT][FONT=&amp]-(1) Kila mtu:[/FONT]

[FONT=&amp](a) anao uhuru wa-[/FONT]
[FONT=&amp](i) kuwa na maoni na kueleza fikra zake;[/FONT]
[FONT=&amp](ii) kufanya mawasiliano na vile vile anayo haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake;[/FONT]
[FONT=&amp](iii) ubunifu na sanaa;[/FONT]
[FONT=&amp](iv) kitaaluma na tafiti za kisayansi; na[/FONT]
[FONT=&amp](b) anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu:[/FONT]
[FONT=&amp](i) matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi; na[/FONT]

[FONT=&amp](ii) utekelezaji wa mamlaka ya nchi kuhusu sera za kitaifa na shughuli ya maendeleo ya jamii; na[/FONT]
[FONT=&amp](iii) masuala mengine muhimu kwa jamii.[/FONT]
[FONT=&amp](2) Utekelezaji wa haki zilizoainishwa katika Ibara ndogo ya (1), utajumuisha wajibu muhimu kwa mwananchi na wajibu huo unaweza kupunguza haki hizo kutokana na:[/FONT]
[FONT=&amp](a) vita au machafuko ya kisiasa; au[/FONT]

[FONT=&amp](b) propaganda kuhusu vita, ushawishi wa chuki kwa misingi ya rangi, ukabila, ubaguzi wa kijinsia, dini au masuala yoyote yanayoweza kuleta madhara kwa Taifa.[/FONT]
[FONT=&amp]
29.[/FONT]
-(1) Kila mtu:


(a) anao uhuru wa-(i) kuwa na maoni na kueleza fikra zake;(ii) kufanya mawasiliano na vile vile anayo haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake;(iii) ubunifu na sanaa;(iv) kitaaluma na tafiti za kisayansi; na(b) anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu:(i) matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi; na(ii) utekelezaji wa mamlaka ya nchi kuhusu sera za kitaifa na shughuli ya maendeleo ya jamii; na(iii) masuala mengine muhimu kwa jamii.(2) Utekelezaji wa haki zilizoainishwa katika Ibara ndogo ya (1), utajumuisha wajibu muhimu kwa mwananchi na wajibu huo unaweza kupunguza haki hizo kutokana na:(a) vita au machafuko ya kisiasa; au(b) propaganda kuhusu vita, ushawishi wa chuki kwa misingi ya rangi, ukabila, ubaguzi wa kijinsia, dini ,propaganda kuhusu shughuli za Uchumi yenye mlengo wa ubaguzi au masuala yoyote yanayoelekea kuleta madhara kwa Taifa.(c) kabla au baada ya mamlaka husika kuchukua hatua kupunguza/kusitisha uhuru wa mtu kwa mujibu wa Ibara 29;2(b) ya katiba hii basi mamlaka husika italiarifu Bunge katika kikao kijacho baada ya tukio husika kuhusu sababu na hatua za kisheria ambazo zimechukuliwa/ inatarajia kuchukuliwa ilikuliepusha Taifa na madhara.
[FONT=&amp]30[/FONT][FONT=&amp].-(1) Kila mtu anao uhuru wa-[/FONT]

[FONT=&amp](a) kutafuta, kupata na kutumia habari na taarifa na kusambaza taarifa hizo; na[/FONT]
[FONT=&amp](b) kuanzisha vyombo vya habari na njia nyingine za upashanaji wa habari bila kujali mipaka ya nchi.[/FONT]
[FONT=&amp](2) Vyombo vya habari vitakuwa huru na vile vile vitakuwa na:[/FONT]
[FONT=&amp](a) haki ya kupata, kutumia na kusambaza habari na taarifa wanazopata;[/FONT]
[FONT=&amp](b) wajibu wa:[/FONT]
[FONT=&amp](i) kusambaza habari na taarifa kwa wananchi; na[/FONT]
[FONT=&amp](ii) kuheshimu na kulinda utu, heshima, uhuru na staha ya wananchi dhidi ya habari na taarifa[/FONT]
[FONT=&amp]wanazozitumia, wanazozitayarisha na kuzisambaza.[/FONT]
[FONT=&amp](3) Serikali na taasisi zake, asasi za kiraia na watu binafsi watakuwa na wajibu wa kutoa habari kwa umma juu ya shughuli na utekelezaji wa shughuli zao.[/FONT]
[FONT=&amp](4) Masharti ya Ibara hii yatalazimika kuzingatia masharti ya sheria ya nchi itakayotungwa kwa ajili hiyo na kwa madhumuni ya kulinda usalama wa Taifa, amani, maadili ya umma, haki, staha na uhuru wa watu wengine.[/FONT]

30.-(1) Kila mtu anao uhuru wa-

(a) kutafuta, kupata na kutumia habari na taarifa na kusambaza taarifa hizo; na

(b) kuanzisha vyombo vya habari na njia nyingine za upashanaji wa habari bila kujali mipaka ya nchi.


(2) Vyombo vya habari vitakuwa huru na vile vile vitakuwa na:


(a) haki ya kupata, kutumia na kusambaza habari na taarifa wanazopata;


(b) wajibu wa:


(i) kusambaza habari na taarifa kwa wananchi; na


(ii) kuheshimu na kulinda utu, heshima, uhuru na staha ya wananchi dhidi ya habari na taarifa

wanazozitumia, wanazozitayarisha na kuzisambaza.

(3) Serikali na taasisi zake, asasi za kiraia na watu binafsi watakuwa na wajibu wa kutoa habari kwa umma juu ya shughuli na utekelezaji wa shughuli zao.


(4) Bunge litatunga sheria ya Habari yenye kulinda Usalama wa Taifa, Amani, Maadili ya Umma, haki, staha na uhuru wa watu wengine bila kuathiri masharti yoyote ya ibara ya Katiba hii.
[FONT=&amp]32.[/FONT][FONT=&amp]Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi,kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kujumuika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.[/FONT]
32.(1)Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi,kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kujumuika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.


(2)Katika kutumia uhuru binafsi kwa mujibu wa ibara ndogo ya 32(1) ya Katiba hii itakuwa marufuku kwa Mtumishi wa Umma kutumia cheo au nafasi yake kwenye utumishi wa Umma kuinufaisha Jumuiya/taasisi ya Imani kwa namna ambayo italeta taswira ya upendeleo au ubaguzi kwa kuwa naye ni mshirika wa Jumuiya hiyo au lah! lakini ananufaika/atanufaika yeye binafsi au taasisi anayoitumikia kupitia Jumuiya hiyo ya Kiimani kwa namna yoyote ile .
 
M

Mp Kalix2

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2010
Messages
5,849
Likes
1,716
Points
280
M

Mp Kalix2

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2010
5,849 1,716 280
Rasimu ya Katiba Mpya mchakato unaendelea maoni binafsi Ibara kwa ibara;


[FONT=&quot]36.[/FONT][FONT=&quot]-(1) Kila mtu anayo haki ya kumiliki mali na hifadhi ya mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria.[/FONT]

[FONT=&quot](2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kunyang’anywa mali yake kwa madhumuni ya kuitaifisha au madhumuni mengine bila malipo yanayolingana na thamani halisi ya mali hiyo na yatakayotolewa mapema.[/FONT]
[FONT=&quot](3) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara hii, haki ya umiliki na hifadhi ya mali haitahusu mali iliyothibitishwa kwamba haikupatikana kwa njia halali.[/FONT]
[FONT=&quot] 36.[/FONT][FONT=&quot]-(1) Kila mtu anayo haki ya kumiliki mali na hifadhi ya mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria.[/FONT]

[FONT=&quot](2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kunyang’anywa mali yake kwa madhumuni ya kuitaifisha au madhumuni mengine bila malipo yanayolingana na thamani halisi ya mali hiyo na yatakayotolewa mapema.[/FONT]
[FONT=&quot](3)Madhumuni yoyote ya kutaifisha mali ya Mtu, Familia, Kampuni au kikundi lazima yawe ni kwa manufaa ya Umma na mwathirika anaweza kupinga Mahakamani utaifishaji kwa madhumuni tajwa. [/FONT]

[FONT=&quot](4) Kwa madhumuni ya masharti ya Ibara hii, haki ya umiliki na hifadhi ya mali haitahusu mali iliyothibitishwa kwamba haikupatikana kwa njia halali.

[/FONT]

[FONT=&quot]37[/FONT][FONT=&quot]. Kila raia ana haki ya kutambuliwa uraia wake na kwa madhumuni haya, mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha wananchi kupata hati ya kuzaliwa, kitambulisho cha uraia wake bila ya upendeleo na ubaguzi wa aina yoyote, na pale inapohitajika, nyaraka za kumwezesha kusafiri.[/FONT]
[FONT=&quot]

[/FONT]

37.(1) Kila raia ana haki ya kutambuliwa uraia wake na kwa madhumuni haya, mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha wananchi kupata hati ya kuzaliwa, kitambulisho cha uraia wake bila ya upendeleo na ubaguzi wa aina yoyote, na pale inapohitajika,nyaraka za kumwezesha kusafiri.

(2) Gharama zitakazotozwa kwa Raia kujipatia hati hizi lazima zizingatie hali ya uchumi wa Nchi na wa mwananchi mmoja mmoja na kwa vyovyote vile gharama ya upatikanaji wa hati ya kusafiria isizidi asilimia Ishirini na tano (20%) ya Kima cha chini cha Kisheria cha Mshahara kwa wakati huo.

[FONT=&quot]38.[/FONT][FONT=&quot]-(1) Mtu aliyekamatwa au aliyewekwa kizuizini anayo haki ya:[/FONT]

[FONT=&quot](a) kuelezwa kwa lugha anayoifahamu -[/FONT]
[FONT=&quot](i) sababu ya kukamatwa;[/FONT]
[FONT=&quot](ii) haki ya kutokutoa maelezo yoyote; na[/FONT]
[FONT=&quot](iii) matokeo ya kutoa maelezo;[/FONT]
[FONT=&quot](b) kutoa maelezo;[/FONT]
[FONT=&quot](c) kuwasiliana na wakili na mtu mwingine ambaye msaada wake ni muhimu kwa mtuhumiwa;[/FONT]
[FONT=&quot](d) kutolazimishwa kutoa maelezo ya kukiri kosa ambayo yatatumika kama ushahidi dhidi yake; na[/FONT]
[FONT=&quot](e) kupelekwa mahakamani mapema iwezekanavyo.[/FONT]
[FONT=&quot](2) Mamlaka za nchi zitaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha:[/FONT]
[FONT=&quot](a) mtuhumiwa kupata nakala ya mashtaka yanayomkabili na kumbukumbu ya mwenendo wa mashtaka;[/FONT]
[FONT=&quot](b) mtuhumiwa au mfungwa kupata nakala ya mwenendo wa mashtaka baada ya shauri kukamilika mahakamani;[/FONT]
[FONT=&quot](c) mtuhumiwa au mfungwa kufikishwa mahakamani ili kuthibitisha uwepo wake.[/FONT]
[FONT=&quot]
38.[/FONT]
-(1) Mtu aliyekamatwa au aliyewekwa kizuizini anayo haki ya:

(a) kuelezwa kwa lugha anayoifahamu -
(i) sababu ya kukamatwa;
(ii) haki ya kutokutoa maelezo yoyote; na
(iii) matokeo ya kutoa maelezo;
(b) kutoa maelezo;
(c) kuwasiliana na wakili na mtu mwingine ambaye msaada wake ni muhimu kwa mtuhumiwa;
(d) kutolazimishwa kutoa maelezo ya kukiri kosa ambayo yatatumika kama ushahidi dhidi yake; na
(e) kupelekwa mahakamani mapema iwezekanavyo.
(2) Mamlaka za nchi zitaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha:
(a) mtuhumiwa kupata nakala ya mashtaka yanayomkabili na kumbukumbu ya mwenendo wa mashtaka;
(b) mtuhumiwa au mfungwa kupata nakala ya mwenendo wa mashtaka baada ya shauri kukamilika mahakamani;
(c) mtuhumiwa au mfungwa kufikishwa mahakamani ili kuthibitisha uwepo wake.
(d) Utaratibu utakaowekwa na Mamlaka ya Nchi kwa mujibu wa kifungu cha 2;a na b cha ibara hii lazima uzingatie hali ya Uchumi wa Nchi hasa suala la gharama na usiwe utaratibu wenye taswira ya ubaguzi au upendeleo


[FONT=&quot] [/FONT]
[FONT=&quot]39[/FONT][FONT=&quot].-(1) Mtu aliye katika kizuizi au ulinzi ataendelea kuwa na haki zote za msingi zilizoainishwa katika Katiba hii kwa kiwango anachostahiki katika mazingira ya kuwekwa kizuizini au katika ulinzi.[/FONT]

[FONT=&quot](2) Mtu aliye katika kizuizi au ulinzi ana haki ya kuiomba mahakama ili mamlaka ya nchi inayomuhifadhi kueleza sababu za yeye kuwekwa au kuendelea kuwa katika kizuizi au ulinzi.[/FONT]
[FONT=&quot](3) Raia wa Jamhuri ya Muungano hatapelekwa katikanchi ya nje yoyote kujibu mashtaka au kufanyiwa mahojiano ya aina yoyote kinyume cha ridhaa yake.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
[FONT=&quot] [/FONT]
[FONT=&quot]
39[/FONT]
.-(1) Mtu aliye katika kizuizi au ulinzi ataendelea kuwa na haki zote za msingi zilizoainishwa katika Katiba hii kwa kiwango anachostahiki katika mazingira ya kuwekwa kizuizini au katika ulinzi.

(2) Mtu aliye katika kizuizi au ulinzi ana haki ya kuiomba mahakama ili mamlaka ya nchi inayomuhifadhi kueleza sababu za yeye kuwekwa au kuendelea kuwa katika kizuizi au ulinzi.
(3) Raia wa Jamhuri ya Muungano hatapelekwa katika nchi yoyote ya nje kujibu mashtaka au kufanyiwa mahojiano ya aina yoyote kinyume cha ridhaa yake na anaweza kupinga hatua hiyo kupinga hatua hiyo kupitia mahakama na kueleza sababu za kupinga hatua hiyo na mamlaka ya Nchi haitachukua hatua ya kumpeleka Nje ya Nchi hadi Mahakama itakapotoa uamuzi wake .[FONT=&quot]42.-[/FONT][FONT=&quot](1) Kila mtoto ana haki ya-[/FONT]

[FONT=&quot](a) kupewa jina na uraia;[/FONT]
[FONT=&quot](b) kutoa mawazo, kusikilizwa na kulindwa dhidi ya uonevu,ukatili na udhalilishaji;[/FONT]
[FONT=&quot](c) kucheza na kupata elimu;[/FONT]
[FONT=&quot](d) kuhifadhiwa katika mazingira mazuri, kwa walio katika ukinzani na sheria;[/FONT]
[FONT=&quot](e) kupata lishe bora, makazi na huduma ya afya; na[/FONT]
[FONT=&quot](f) kushiriki katika shughuli zinazolingana na umri alionao; na[/FONT]
[FONT=&quot](g) kupata malezi na ulinzi wa wazazi, walezi au mamlaka ya nchi,bila ya ubaguzi wa rangi, utaifa, lugha, mtazamo wa kisiasa, jamii anayotokea, mali, uzazi, kabila, dini, jinsi au aina nyingine za hadhi.[/FONT]
[FONT=&quot](2) Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha utekelezaji na usimamizi wa haki za mtoto kwa kufuata msingi wa kutoa kipaumbele kwa maslahi na manufaa ya mtoto.[/FONT]

42.-(1) Kila mtoto ana haki ya-

(a) kupewa jina na uraia;
(b) kutoa mawazo, kusikilizwa na kulindwa dhidi ya uonevu,ukatili na udhalilishaji;
(c) kucheza na kupata elimu;
(d) kuhifadhiwa katika mazingira mazuri, kwa walio katika ukinzani na sheria;
(e) kupata lishe bora, makazi na huduma ya afya; na
(f) kushiriki katika shughuli zinazolingana na umri alionao; na
(g) kupata malezi na ulinzi wa wazazi, walezi au mamlaka ya nchi,bila ya ubaguzi wa rangi, utaifa, lugha, mtazamo wa kisiasa, jamii anayotokea, mali, uzazi, kabila, dini, jinsi au aina nyingine za hadhi.
(2) Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha utekelezaji na usimamizi wa haki za mtoto kwa kufuata msingi wa kutoa kipaumbele kwa maslahi na manufaa ya mtoto na jamii kwa ujumla.

[FONT=&quot]43. [/FONT][FONT=&quot]Kila kijana ana haki na wajibu wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya Jamhuri ya Muungano pamoja na jamii kwa ujumla, na kwa mantiki hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali za Washirika wa Muungano na jamii zitahakikisha kuwa vijana anawekewa mazingira mazuri ya kuwa raia wema na kupatiwa fursa za kushiriki kikamilifu katika nyanja za kisiasa, kiuchumi,kijamii na kiutamaduni.[/FONT]
[FONT=&quot]
43.- [/FONT]
(1)Kila kijana ana haki na wajibu wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya Jamhuri ya Muungano pamoja na jamii kwa ujumla, na kwa mantiki hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali za Washirika wa Muungano na jamii zitahakikisha kuwa vijana

wanawekewa mazingira mazuri ya kuwa raia wema na kupatiwa fursa za kushiriki kikamilifu katika nyanja za kisiasa, kiuchumi,kijamii na kiutamaduni.
(2)Kijana kwa mujibu wa Ibara ya Katiba hii atakuwa mtu wa Umri wa miaka kati ya 15-30

[FONT=&quot] [/FONT]
[FONT=&quot]46[/FONT][FONT=&quot].-(1) Kila mwanamke ana haki ya:[/FONT]

[FONT=&quot](a) kuheshimiwa utu wake;[/FONT]
[FONT=&quot](b) kuwa salama dhidi ya unyonyaji na ukatili;[/FONT]
[FONT=&quot](c) kushiriki bila ya ubaguzi katika chaguzi na ngazi zote za maamuzi;[/FONT]
[FONT=&quot](d) kupata ujira sawa na mwanaume katika kazi;[/FONT]
[FONT=&quot](e) kulindwa dhidi ya ubaguzi, uonevu na mila zenye madhara;[/FONT]
[FONT=&quot](f) kulindwa kwa ajira yake wakati wa ujauzito na pale anapojifungua; na[/FONT]

[FONT=&quot](g) kupata huduma ya juu ya afya inayopatikana.[/FONT]
[FONT=&quot](2) Mamlaka husika za nchi zitaweka utaratibu wa kisheria utakaosimamia masuala yanayohusu utekelezaji wa masharti ya Ibara hii ikiwa ni pamoja na kukuza utu, usalama na fursa za wanawake wakiwemo wajane.[/FONT]
[FONT=&quot]

[/FONT]


46.-(1) Kila mwanamke ana haki ya:

(a) kuheshimiwa utu wake;

(b) kuwa salama dhidi ya unyonyaji na ukatili;
(c) kushiriki bila ya ubaguzi katika chaguzi na ngazi zote za maamuzi;
(d) kupata ujira sawa na mwanaume katika kazi;
(e) kulindwa dhidi ya ubaguzi, uonevu na mila zenye madhara;
(f) kulindwa kwa ajira yake wakati wa ujauzito na pale anapojifungua; na
(g) kupata huduma ya afya inayopatikana.
(2) Mamlaka husika za nchi zitaweka utaratibu wa kisheria utakaosimamia masuala yanayohusu utekelezaji wa masharti ya Ibara hii ikiwa ni pamoja na kukuza utu, usalama na fursa za wanawake wakiwemo wajane.
[FONT=&quot] [/FONT]
[FONT=&quot] [/FONT]
[FONT=&quot] [/FONT]
[FONT=&quot]49[/FONT][FONT=&quot].-(1) Kila raia anao wajibu wa kulinda maliasili ya Taifa, mali ya mamlaka ya nchi na mali yoyote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine.[/FONT]

[FONT=&quot](2) Kila mtu ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha[/FONT]
[FONT=&quot]rasilimali za nchi na maliasili za Taifa.[/FONT]
[FONT=&quot](3) Kila mtu anao wajibu wa kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na mali inayomilikiwa kwa pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu, na kuendesha uchumi wa Taifa kwa makini kwa kuzingatia mipango endelevu na haki ya vizazi vijavyo.[/FONT]
[FONT=&quot] [/FONT]
[FONT=&quot] [/FONT]
49.-(1) Kila raia anao wajibu wa kulinda maliasili ya Taifa, mali ya mamlaka ya nchi na mali yoyote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine.

(2) Kila mtu ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha rasilimali za nchi na maliasili za Taifa.
(3) Kila mtu anao wajibu wa kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na mali inayomilikiwa kwa pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu, na kuendesha uchumi wa Taifa kwa makini kwa kuzingatia mipango endelevu na haki ya vizazi vijavyo.

(4) Ni marufuku kwa Mtu yoyote kutumia rasilimali au mali ya Umma kwa manufaa binafsi, familia yake au marafiki zake kinyume na taratibu/kanuni zilizopo za kisheria ambazo Mamlaka ya nchi itahakikisha wananchi wengi wanazijua /kuzifahamu ilikuweza kusimamia sawia ibara ya 49(1) ya katiba hii.[FONT=&quot]55[/FONT][FONT=&quot].-(1) Kila mtu anayezaliwa Tanzania Bara au Zanzibar atakuwa raia wa Jamhuri ya Muungano iwapo, wakati wa tarehe ya kuzaliwa, mama au baba yake ni au alikuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.[/FONT]

[FONT=&quot](2) Kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, mtu aliyezaliwa nje ya Tanzania[/FONT]
[FONT=&quot]atakuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzaliwa kuanzia tarehe ya kuzaliwa[/FONT]
[FONT=&quot]kwake ikiwa wazazi wake au mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa Jamhuri ya[/FONT]
[FONT=&quot]Muungano.[/FONT]

[FONT=&quot](3) Endapo mmoja kati ya wazazi alifariki kabla ya mtu huyo kuzaliwa,uraia wa mzazi huyo wakati wa kifo chake unatumika, kwa madhumuni ya kutambua uraia wa mtu huyo aliyezaliwa baada ya mzazi aliyefariki kama kwamba mzazi huyo alikuwa anaishi hadi kuzaliwa kwa mtu huyo.[/FONT]
[FONT=&quot](4) Mtoto mwenye umri chini ya miaka saba akikutwa ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muunganokatika mazingira ambayo wazazi wake hawajulikani, atahesabika kuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa.[/FONT]
[FONT=&quot](5) Mtoto aliye na umri wa chini ya miaka kumi na nane ambaye wazazi wake sio raia wa Tanzania, akiasiliwa na raia wa Jamhuri ya Muungano, kwa kuasiliwa kwake huko, kutawezesha mtoto huyo kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa kujiandikisha.[/FONT]
[FONT=&quot][/FONT]

[FONT=&quot]

[/FONT]


55.-(1) Kila mtu anayezaliwa Tanganyika au Zanzibar atakuwa raia wa Jamhuri ya Muungano iwapo, wakati wa tarehe ya kuzaliwa, mama au baba yake ni au alikuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.

(2) Kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, mtu aliyezaliwa nje ya Tanzania atakuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kuzaliwa kuanzia tarehe ya kuzaliwa kwake ikiwa wazazi wake au mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa Jamhuri ya Muungano.
(3) Endapo mmoja kati ya wazazi alifariki kabla ya mtu huyo kuzaliwa, uraia wa mzazi huyo wakati wa kifo chake unatumika, kwa madhumuni ya kutambua uraia wa mtu huyo aliyezaliwa baada ya mzazi aliyefariki kana kwamba mzazi huyo alikuwa anaishi hadi kuzaliwa kwa mtu huyo.
(4) Mtoto mwenye umri chini ya miaka saba akikutwa ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano katika mazingira ambayo wazazi wake hawajulikani,atahesabika kuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa.

(5) Mtoto aliye na umri wa chini ya miaka kumi na nane ambaye wazazi wake sio raia wa Tanzania, akiasiliwa na raia wa Jamhuri ya Muungano, kwa kuasiliwa kwake huko, kutawezesha mtoto huyo kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa kujiandikisha.
[FONT=&quot]56[/FONT][FONT=&quot].-(1) Mara baada ya kuanza kutumika kwa Katiba hii, mtu ambaye amekuwa mkazi wa Tanzania Bara au Zanzibar kwa muda uliowekwa na sheria inayotumika Tanzania Bara au Zanzibar, na ambaye ametimiza masharti yote ya sheria ya Bunge la Tanzania Bara au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, anaweza kuomba kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.[/FONT]

[FONT=&quot](2) Mtu aliyefunga ndoa na raia wa Jamhuri ya Muunganoanaweza kutuma maombi ya kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.[/FONT]
[FONT=&quot](3)Endapo ndoa iliyorejewa katika Ibara ndogo ya (2) itavunjika, kama mtu huyo hakuukana uraia wake, ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.[/FONT]
[FONT=&quot](4) Mtoto aliyezaliwa katika ndoa iliyorejewa katika Ibara ndogo ya (2), ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa kama ataukana uraia huo au ataomba na kupata uraia wa nchi nyingine.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
[FONT=&quot]
[/FONT]


56.-(1) Mara baada ya kuanza kutumika kwa Katiba hii, mtu ambaye amekuwa mkazi wa Tanzania Bara au Zanzibar kwa muda uliowekwa na sheria inayotumika Tanganyika au Zanzibar, na ambaye ametimiza masharti yote ya sheria ya Bunge la Tanganyika au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, anaweza kuomba kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Mtu aliyefunga ndoa na raia wa Jamhuri ya Muungano anaweza kutuma maombi ya kuandikishwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano na mara baada ya kukubaliwa kuwa Raia wa kuandikishwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mtu huyo atawasilisha hati ya kuukana Urai wa Nchi yake ya Awali.
(3)Endapo ndoa iliyorejewa katika Ibara ndogo ya (2) itavunjika, kama mtu huyo hakuukana uraia wake, ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano.
(4) Mtoto aliyezaliwa katika ndoa iliyorejewa katika Ibara ndogo ya (2),ataendelea kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa kama ataukana uraia huo au ataomba na kupata uraia wa nchi nyingine
(5) Kwa vyovyote vile nimarufuku kuwa na Uraia wa Nchi mbili ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

[FONT=&quot] [/FONT]
[FONT=&quot] [/FONT]
[FONT=&quot] [/FONT]
[FONT=&quot] [/FONT]
[FONT=&quot] [/FONT]
[FONT=&quot]57[/FONT][FONT=&quot].-(1) Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo wa shirikisho lenye[/FONT]

[FONT=&quot]serikali tatu ambazo ni:[/FONT]
[FONT=&quot](a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;[/FONT]
[FONT=&quot](b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na[/FONT]

[FONT=&quot](c) Serikali ya Tanzania Bara.[/FONT]
[FONT=&quot](2) Shughuli za Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kusimamiwa[/FONT]
[FONT=&quot]na:[/FONT]
[FONT=&quot](a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano;[/FONT]
[FONT=&quot](b) Bunge la Jamhuri ya Muungano; na[/FONT]
[FONT=&quot](c) Mahakama ya Jamhuri ya Muungano.[/FONT]
[FONT=&quot](3) Muundo, madaraka na mambo mengine ya kiutendaji yahusuyo[/FONT]
[FONT=&quot]Serikali yaTanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yataainishwa katika Katiba za Washirika wa Muungano.[/FONT]
[FONT=&quot] [/FONT]
[FONT=&quot]

57[/FONT]
.-(1) Jamhuri ya Muungano itakuwa na muundo wa shirikisho lenye serikali tatu ambazo ni:

(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
(b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na
(c) Serikali ya Tanganyika.
(2) Shughuli za Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kusimamiwa
na:
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(b) Bunge la Jamhuri ya Muungano; na
(c) Mahakama ya Jamhuri ya Muungano.
(3) Muundo, madaraka na mambo mengine ya kiutendaji yahusuyo Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yataainishwa katika Katiba za Washirika wa Muungano.

4;a.Washirika wa Muungano kupitia mabunge zao wanaweza kujadili na kupitisha hoja ya kuandaliwa kwa upiga wa Kura ya Maoni ya wananchi wote wa kila pande ya washirika kadri watakavyoona inafaa kuamua aina nyingine ya Muundo wa Muungano au kuvunjwa kwa Muungano.

(b) Kwa vyovyote vile idadi ya ushindi wa wapiga kura itakayo halalisha uamuzi wowote kwa mujibu wa Ibara ya Katiba ni lazima kuwa zaidi ya Theluthi mbili ya wapiga kura wote walioandikishwa kwa upande ulioamua kupiga kura hiyo ya maoni kuwezesha mabadiliko yoyote .


(c)Hoja yoyote kupitia Bunge la washirika au bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu uamuzi wa suala la Muundo wa Muungano lazima ni kwa kupiga kura ya siri na idadi ya zaidi ya theluthi mbili ya wabunge wote ndiyo itakayoamua hatima ya hoja husika.

(5) Itakuwa marufuku kwa Mtumishi wa Umma wa Jamhuri ya Muungano au wa Serikali za washirika kushabikia ,kushawishi watu,mtu au taasisi yoyote kuchagiza mabadiliko au kuvunjwa kwa Muundo uliopo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


(6) Masharti ya kufuatwa kuwezesha mabadiliko au kuvunja Muundo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lazima yazingatie;
a.kwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania kupeleka mswada binafsi ndani ya Bunge la Jamhuri ya Tanzania akieleza nia,sababu,faida,madhara yatokanayo na hatua anayopendekeza na Bunge litajadili na kupitisha Uamuzi kwa kutumia kanuni za shughuli za Bunge
(b). kwa Mbunge wa Bunge la Mshirika kupeleka mswada binafsi ndani ya Bunge la Nchi yake akieleza nia,sababu,faida,madhara yatokanayo na hatua anayopendekeza na Bunge litajadili na kupitisha Uamuzi kwa kutumia kanuni za shughuli za Bunge husika

(c).kw kikundi cha watu Raia halali wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuzaliwa au wa kuandikishwa waliokaa zaidi ya miaka Saba kuandaa madai yao ,kukusanya majina .anuani ,sahihi zao na kuziwazilisha kwa Jaji wa Mahakama ya Juu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Mawakili au Wakili.

(d) Uamuzi wowote wa Mahakama kama ni wakukubaliana na madai ya wafungua shauri basi Mahakama itaamuru Serikali ya Jamhuri au Serikali ya upande husika ya Mshirika wa Muungano kuitisha kura ya Maoni.


(e)Kwa vyovyote vile uamuzi wowote utokanao na Bunge la Jamhuri ya Tanzania , mmoja wa Mshirika wa Muungano au Uamuzi wa Mahakama kukubali ombi la wafungua shauri mahakamani kwa mujibu wa ibara 57.(6c) ya Katiba hii kuhusu kutengua Muundo wa Muungano au uwepo wake lazima kura ya maoni ipigwe kwa upande ulileta hoja husika na kama hoja imeletwa kupitia Bunge au mahakama ya Muungano basi upigaji kura ya maoni utakuwa wa pande zote za Washirika wa Muungano na idadi yenye kuhalilisha maamuzi yoyote ni kwa mujibu wa Ibara 57;(4b) ya Katiba hii.


(7) Bunge litatunga Sheria itakayosimamia ugawanaji wa Mali zitakazokuwa zikisimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa niaba ya Washirika wa Muungano kama itatokea Muungano kuvunjika kwa mujibu wa Katiba hii.

 

Forum statistics

Threads 1,275,055
Members 490,894
Posts 30,531,653