Hapana Chezea mkurya

Mtamile

JF-Expert Member
Aug 2, 2011
2,838
1,267
Mkutano wa mwaka wa Chama cha Walioolewa Duniani (CHAWADU) ulikuwa inaendelea, na akina mama kutoka nchi mbali mbali walikuwa wanatoa ripoti ya utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa mwaka uliopita;
MAMA UK: Baada ya maazimio ya mkutano wa mwisho kuwa lazima waume zetu waanze kujipikia wenyewe, nilipofika London nilimueleza mume wangu maamuzi hayo, siku ya kwanza sikuona kitu, siku ya pili pia sikuona kitu, siku ya tatu akaelewa kuwa niko serious, mwenyewe aliingia jikoni na kuanza kupika (Makofi na vigelegele)

MAMA USA: Baada ya maazimio ya mwaka jana niliporudi Boston, nilimwambia mume wangu kuwa sitampikia wala kumfulia tena. Siku ya kwanza sikuona kitu, siku ya pili alifua nguo chache, siku ya tatu mwenyewe alifua nguo zote pamoja na zangu na akaingia jikoni kupika (Makofi vifijo na vigelegele)

MAMA TZ: Baada ya maazimio ya mwaka jana, niriporudi kwetu Musoma, nikamwambia mume wangu kuanzia reo, razima ujipikie mwenyewe, ufue nguo zako mwenyewe, ufagie nyumba na kutandika kitanda mwenyewe, tumeshaamua na hata wazungu ndio wataenderea kufanya hivyo kwao. Siku ya kwanza sikuona kitu, siku ya pili sikuona kitu, siku ya tatu sikuona kitu, siku ya nne kwa mbari nilianza kuona kwa jicho ra kushoto, maana uvimbe usoni urianza kupungua, ira jicho rangu ra kuria mpaka reo bado rinatoa machozi harijapona sawasawa

 
Ngocha, reo mama Bhoke rasima atanichua maana amesidi sana siku hisi kisa eti kawa mhesimiwa tiwani.
 
Wewe HOUSE WIFE nakupa Big up sana kwani uwezo wako wa kufafanua mambo ni mkubwa sana. sio vema kudraw conclusion hasa kwa mambo ya msingi kimaisha. Je, unadhani kweli ndivyo wakurya tulivyo? picha hiyo na mentality ambazo watu wengi wanazo juuu ya kabila hili zinatia simanzi sana katika jamii za kitanzania kwa kuwa na mitazamo hasi juu ya kabila la wakurya.
 
Back
Top Bottom