Hapakuwa na haja ya kuwaondoa wamachinga na kuvunja vibanda pembezoni mwa mji

Nadhani aliyepewa jukumu la kusafisha mji hakuelewa vyema mji unaanzia wapi na kuishia wapi.

Yeye alijua Dar nzima kila mahali ni mji.

Kumbe anayekaa mbagala akitaka kwenda posta anasema nakwenda Mjini, wa mbezi naye hivyo hivyo.

Posta ndio Mjini ak.a Centre Business District na ndiko kulikotakiwa kusafishwa na si kwingineko.
 
Tutafute permanent solution ya hili tatizo.
Mfano pale Mbezi mwisho kutokana na kua na Wafanyabiashara barabarani kitendo cha kutoka stand ndogo mpaka Morogoro road ilikua inachukua mpaka dakika 15 au zaidi wakati kiuhalisia ni sehemu ya chini ya dakika 5.

Au sehemu nyingine ni Arusha kutoka pale friends corner mpaka round about ya Krokoni wafanyabiashara walikua wanapanga bidhaa hadi barabarani. Kuna siku walivunja kioo cha nyuma cha gari la dada la watu na bado wakamharass kisa alikanyaga nyanya za watu wakati ukiangalia kiuhalisia barabara is almost impassable.

Tutafute permanent solution ya matatizo yetu. Yes it's painful but tupate muarobaini wa hili tatizo.
Tatizo watu wabishi sana

Anaangalia urahisi na sio usalama wala usafi nk
 
Kusema ukweli sioni sababu ya kuwaondoa wafanyabiashara ndogo ndogo waliokuwepo huku pembezoni mwa mji kwenye vituo vya daladala kama vile Banana, Mombasa, Gongo la mboto, Mbagala, Mbezi etc.

Huku pembezoni walikuwa wanaathiri nini mpaka mumewaondoa pia? Kuwaondoa katikati ya mji kama Posta na Kariakoo ilikuwa sahihi lakini sio huku pembezoni mwa mji ambako ndio makazi ya watu.

Viongozi jaribuni kulifikiria upya hili swala. Hawa jamaa licha ya kujipatia kipato walikuwa wanasaidia sana. Wengine hatuna muda wa kwenda sokoni kununua matunda au yale mahitaji madogo madogo tuliyokuwa tunayapata kwenye vituo vya daladala tukiwa tunaelekea nyumbani tukiwa tunatoka makazini.

Sasa hivi vituo vya daladala vimepoa sana utadhani tupo vijijini. Binafsi wafanyabiashara kwenye vituo vya daladala naona walikuwa wanaupendezesha mji na wanarahisisha sana maisha.

Badala ya kupoteza muda kwenda sokoni tulikuwa tunapata mahitaji yetu bila shida kabisa na kwa bei nafuu.

Viongozi hebu jaribuni kuliangalia hili suala kwa mapana, sioni tatizo la machinga kufanya biashara pembezoni mwa mji na zaidi ya yote sisi raia wa kawaida tunawahitaji.
Kwanza nasapoti 100% kuondolewa kwa machinga maeneo yote ambayo si rasmi na mengine yalikua hatarishi kiusalama barabaran. Pili.. hakunaga utaratib wa hivyo watu wamejaa kando ya barabara kuchuuza bidhaa zao. Imagine pale zakhiem walivyokua wanajaa mpaka magari yanapishana na watembea kwa miguu papo kwa papo. Tatu.. kuwajaza machinga kila sehem ile ilikua kutafuta popularity kisiasa tu hata hayati ni lazima angekuja kuwatimua na kuwatafutia maeneo rasmi. NB: Kikuwa na maeneo rasmi ya kununua nyanya, maembe, viatu, na mahitaj mengineyo tutazoea na tutaenda tu!! Cities planning muhimu na sio kufanya jambo ili ufurahishe umma!!!
 
Kusema ukweli sioni sababu ya kuwaondoa wafanyabiashara ndogo ndogo waliokuwepo huku pembezoni mwa mji kwenye vituo vya daladala kama vile Banana, Mombasa, Gongo la mboto, Mbagala, Mbezi etc.

Huku pembezoni walikuwa wanaathiri nini mpaka mumewaondoa pia? Kuwaondoa katikati ya mji kama Posta na Kariakoo ilikuwa sahihi lakini sio huku pembezoni mwa mji ambako ndio makazi ya watu.

Viongozi jaribuni kulifikiria upya hili swala. Hawa jamaa licha ya kujipatia kipato walikuwa wanasaidia sana. Wengine hatuna muda wa kwenda sokoni kununua matunda au yale mahitaji madogo madogo tuliyokuwa tunayapata kwenye vituo vya daladala tukiwa tunaelekea nyumbani tukiwa tunatoka makazini.

Sasa hivi vituo vya daladala vimepoa sana utadhani tupo vijijini. Binafsi wafanyabiashara kwenye vituo vya daladala naona walikuwa wanaupendezesha mji na wanarahisisha sana maisha.

Badala ya kupoteza muda kwenda sokoni tulikuwa tunapata mahitaji yetu bila shida kabisa na kwa bei nafuu.

Viongozi hebu jaribuni kuliangalia hili suala kwa mapana, sioni tatizo la machinga kufanya biashara pembezoni mwa mji na zaidi ya yote sisi raia wa kawaida tunawahitaji.
Unaongelea wamachinga au wafanya biashara ndogondogo. Japo haileti mantiki mtu kuuza majora ya vitambaa, au stationery ukaiita eti ni machinga.
Halafu huu uvivu wa baadhi ya wabongo kuwa muuzaji ndo amfwate mnunuaji barabarani tena stendi ni uwehu tu.
Wakipangiwa maeneo rasmi mbona wateja wanawafuata tu. Kumekuwa na maeneo maarufu kutokana na bidhaa hizo kupatikana huko mfano Mahakama ya ndizi. Wanaohitaji mdizi wanaenda pale na hutowaona wakizifuata goba. Hebu jiongezee kidogo.
 
Nadhani aliyepewa jukumu la kusafisha mji hakuelewa vyema mji unaanzia wapi na kuishia wapi.

Yeye alijua Dar nzima kila mahali ni mji.

Kumbe anayekaa mbagala akitaka kwenda posta anasema nakwenda Mjini, wa mbezi naye hivyo hivyo.

Posta ndio Mjini ak.a Centre Business District na ndiko kulikotakiwa kusafishwa na si kwingineko.
Cha kusikitisha watu hata hawatoa sababu ya kuwasafisha hadi pembezoni mwa mji.
 
Cha kusikitisha watu hata hawatoa sababu ya kuwasafisha hadi pembezoni mwa mji.
Kwa bahati mbaya tuna viongozi ambao wanapenda kutafuta sifa kwa wakuu wao hawajali nani anaumia mradi yeye kibarua chake kiko salama na mkuu kafurahi.
 
Sijui kulikuwa na logic gani kuwasafisha hadi huku pembeni.
Tumewasafisha ili kuweka usawa na wale wa mjini kati! Huku pembeni walikuwa pia wanapanga bidhaa zao mpaka barabarani! Naiunga mkono serikali katika hili!
 
Banana, Mombasa, Gongo la mboto, Mbagala, Mbezi

Kwa jiji letu la Dar es Salaam, inapendeza na ni salama kuwa Chinga hawatakiwi kuwepo pembezoni mwa barabara zote kuu ktk jiji la Dar es Salaam kama New Bagamoyo, Morogoro Road, Kilwa, Kawawa na barabara zote zinazotumiwa na watu wengi iwe Mwananyamala kwa KomaKoma, Toure Drive , Haile Sellasie, Shekilango, Mandela Express way, Sam Nujoma, Tabata Kimanga, Kinondoni Road, Temeke Wailes, Tandika kwa Kondo n.k
 
South Africa kwa kina Khumbu kulikuwa pia na huu ujinga wa wamachinga kuuza mchicha kwenye lami ya watembea kwa miguu?
 
Back
Top Bottom