konda msafi
JF-Expert Member
- Sep 5, 2018
- 1,666
- 8,561
Kusema ukweli sioni sababu ya kuwaondoa wafanyabiashara ndogo ndogo waliokuwepo huku pembezoni mwa mji kwenye vituo vya daladala kama vile Banana, Mombasa, Gongo la mboto, Mbagala, Mbezi etc.
Huku pembezoni walikuwa wanaathiri nini mpaka mumewaondoa pia? Kuwaondoa katikati ya mji kama Posta na Kariakoo ilikuwa sahihi lakini sio huku pembezoni mwa mji ambako ndio makazi ya watu.
Viongozi jaribuni kulifikiria upya hili swala. Hawa jamaa licha ya kujipatia kipato walikuwa wanasaidia sana. Wengine hatuna muda wa kwenda sokoni kununua matunda au yale mahitaji madogo madogo tuliyokuwa tunayapata kwenye vituo vya daladala tukiwa tunaelekea nyumbani tukiwa tunatoka makazini.
Sasa hivi vituo vya daladala vimepoa sana utadhani tupo vijijini. Binafsi wafanyabiashara kwenye vituo vya daladala naona walikuwa wanaupendezesha mji na wanarahisisha sana maisha.
Badala ya kupoteza muda kwenda sokoni tulikuwa tunapata mahitaji yetu bila shida kabisa na kwa bei nafuu.
Viongozi hebu jaribuni kuliangalia hili suala kwa mapana, sioni tatizo la machinga kufanya biashara pembezoni mwa mji na zaidi ya yote sisi raia wa kawaida tunawahitaji.