Hapa wanaadhimisha miaka 95, kule polisi anampiga mtuhumiwa risasi kiunoni kwa makosa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hapa wanaadhimisha miaka 95, kule polisi anampiga mtuhumiwa risasi kiunoni kwa makosa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nzi, Aug 25, 2011.

 1. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
  Katika hali isiyo ya kawaida polisi mmoja kule Mara amempiga risasi kiunoni na kumuua mtuhumiwa mmoja wa ujambazi aliekua anakimbia. Mtuhumiwa huyo mwenye jina la Ochieng' pamoja na wenzake wawili walikua wamepanga kufanya tukio la ujambazi katika moja ya maeneo yaliyo karibu na mwambao wa Ziwa Victoria.

  Lakini kutokana na whistleblowers katika maeneo hayo, polisi walipewa taarifa na kwenda kuwakabili majambazi hayo, ndipo ndugu Ochieng' akaanza kukimbia, polisi alimtaarifu asimame la sivyo atampiga risasi, Ochieng' akaendelea kukimbia...

  Polisi akaamua kupiga risasi tatu juu hewani ili amshtue mtuhumiwa, lakini haikusaidia. Ndipo polisi huyo akaamua kukumbushia mazoezi ya kulenga shabaha, akampiga ndugu Ochieng' kiunoni!! (Haya ni maelezo toka kwa kamanda wa polisi wa eneo husika). Kutokana na maelezo ya kamanda wake, polisi yule alikosea kumlenga mtuhumiwa!!

  Chanzo
  : TBC1

  Sasa nimejiuliza sana hivi huyu polisi alipitia mafunzo ya kulenga shabaha kweli? Kama ndio alifuzu kweli? Kama hakupata mafunzo kwa nini amepewa silaha?

  Je, kuna hatua gani za kinidhamu na kisheria anapaswa kuchukuliwa? Je, ndugu za Ocheing' hawastahili kupewa fidia?! Nasema haya kwa vile kulikua hakuna majibizano ya risasi baina ya polisi na mtuhumiwa, hivyo the preferable option aliyokua nayo yule polisi ni kumpiga risasi ya mguuni mtuhumiwa ili asiendelee kukimbia!!

  Haya yametokea leo huku jeshi la polisi likiadhimisha miaka 95 toka kuanzishwa kwake!! Na muhishiwa rais amesisitiza suala la polisi kuheshimu haki za raia.
   
 2. M

  Maengo JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh! Mi napita tu...!
   
 3. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa uelewa wangu huyu Polisi hana HATIA, na alipitia mafunzo ya kazi yake ndio maana alitenda alivyotenda
  Kiutaratibu alishamuonya aliyekuwa akikimbia, kwa kupiga risasi tatu hewani
  Mtoa hoja Unatakiwa ujue pia jinsi silaha hasa ya SMG na tabia zake, huwa inapaa kwenda juu
  Kwa maelezo yako inaonesha kabisa Polisi alilenga kwa ufasaha na kupiga, akiwa amesimama (inavyoonekana, ni vigumu kulenga ukiwa unakimbia) na matokeo alimpiga kiunoni eneo karibu na miguu, kwani alielengwa alikuwa akikimbia, kwa maana kuwa alikuwa akiongeza umbali wa target kila second
  Ingekuwa risasi imempiga kichwani au mabegani hapo kidogo ingekuwa sio weledi
  Kwa kumalizia tu, marehemu alitakiwa asimame ajisalimishe mara risasi tatu kupigwa hewani, kama ulivyoeleza
  Alipoendelea kukimbia Polisi hakuwa na jinsi ila tu kumsimamisha kwa kutumia silaha aliyopewa na Jeshi.
  Marehemu alikuwa jambazi kama ulivyosema suala la fidia HALIPO, kwani hiyo ni probable consequence ya tendo la ujambazi, kuua au kuuliwa.
  Tuwaache Polisi wafanye kazi yao ya kulinda raia na mali zao, sio kuwalaumu kwa kila jambo.
  HONGERA JESHI LA POLISI KUTIMIZA MIAKA 95
   
 4. l

  lebadudumizi Senior Member

  #4
  Aug 26, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera jeshi la polisi kazi nzuri mtuhumiwa angefanikiwa kutoroka angetusumbua mitaani afadhali katangulia.
   
 5. B

  Bweri Member

  #5
  Aug 26, 2011
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  hongera sana cha moto kwamaelezo mazuri yasiyotia shaka juu ya majibu wa polisi،matumizi ya silaha pia wajibu wa raia.hongera sana askari huna kosa katika hilo.
   
 6. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #6
  Aug 27, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
  Mkuu! Kwani wakati wa mafunzo hawajifunzi kulenga shabaha katika hali hiyo?! Unafahamu umbali wa kutoka kwenye mguu hadi kiunoni? Kweli polisi aliefuzu vyema anaweza kufanya kosa kama hilo?!
  Fidia inapaswa kuwepo kwakua polisi alifanya makosa katika kutimiza majukumu yake..pia huyu mtuhumiwa alikua innocent until proven guilty by the court..
   
 7. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Nadhan wakati wa mafunzo wanajifunza kulenga shabaha katika hali kama hiyo!......umbali wa kutoka kwenye mguu hadi kiunoni!!!!!!!!!! Polisi aliefuzu vyema haweza kufanya kosa kama hilo!!!!!!!!!!!!!!!!
  Fidia inapaswa kuwepo kwakua polisi alifanya makosa katika kutimiza majukumu yake..pia huyu mtuhumiwa alikuwa bado hajahukumiwa, so ni innocent
  [
   
Loading...