Hapa tu anagombea Udiwani anafanya 'Unyangindo' huu, huyu akigombea Ubunge si anaweza hata Kutoa 'Kafara' Wazazi wake?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,542
108,841
Mgombea wa nafasi ya udiwani katika Kata ya Sungwizi Tarafa ya Simbo wilayani Igunga mkoani Tabora, Katambi Sospeter amejikuta katika wakati mgumu baada ya kudodosha kibuyu cha dawa za kienyeji alipokuwa akiingia kwenye ukumbi wa kupigia kura za maoni katika Shule ya Msingi Sungwizi.

Tukio hilo lilitokea jana Julai 25, 2020 ambapo mgombea huyo wakati akijaribu kupanda ngazi ili kuingia katika jengo hilo kibuyu hicho chenye dawa kilidondoka kwa bahati mbaya kutoka kwenye mfuko wake wa suruali mbele ya wajumbe.

Nipashe

Hata hivyo sijashangaa sana kwani nasikia kuna Mtu Mmoja huko Baharini alienda ' Kutia Nia ' akiwa na ' Hirizi ' Tatu na Maji ya 'Mochwari' kabisa.
 
Kibuyu hicho kilikuwa na ukubwa gani mpk kikatosha lwenye mfuko wa suruali?
...
JamiiForums-616102249.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom