Hapa sasa TCRA mmezidi

rushanju

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
3,130
4,619
Kama mnaweka masharti naomba muwe mnaangalia uwezo wa mitambo yenu. Tangu Ijumaa wiki iliyopita watu walipa kwa ajili ya kurudisha line zao zilizoptea lakini hakuna aliyepata line yake. Matokeo yake watu wanalipa kila siku na kauli yenu ni MTANDAO uko chini. Unaambiwa lipa tena na unalipa wimbo ni uleule. Hii ni kwa Tanzania nzima.

Mnakula hela ya watu bure na hawana pia mawasiliano. Simu kwa sasa ni biashara. Simu ni chanzo cha mapato, nyie kama hamna uwezo kwanini mnaweka masharti ya kiwizi.? Najaribu kufikiria kama ingekuwa ni mtu binafsi anaifanyia hivyo serikali sijui ingekuwaje!
 
Back
Top Bottom