Hapa Rais wetu anakagua gwaride au anaonyesha gwaride?

Eleweni kuwa mh. Rais alifanya hivyo baada ya kumaliza kukagua gwaride la heshima, sasa mapovu mengine yanawatoka bure kabisaa, hajakosea chochote kwani alikuwa ameshamaliza jukumu lake kama C in C
 
Cha ajabu sasa Wazungu wenyewe wala hawamind vitu peanuts kama hivyo ni ninyi nigga tu ndiyo mnafanya maisha yawe magumu bila hata sababu ...
kada acha hizo,hilo gwaride labda ni la afande brigedia jenerali chan pa mo hu wa jeshi la kivietnam enzi wanazichapa na marekani.

hapo imekosa sigara na zile kofia kama tenga
 
Si ndo anafananaga na baba wa taifa JK nyerere eti niulize wazee nae aliwahi kufanya hivyo na mabook 7 nae mnijibu msiingie mitini
 
Kila jambo analolifanya mkuu wa nchi ni habari na ni somo!! Nimeshuhudia sherehe za uhuru nyingi na pia sherehe za kitaifa nyingi sana. Na pia rais wetu msataafu alikua mwanajeshi yamkini anajua kupiga kwata kuliko rais wetu magufuli. Lakn alitembea kawaida akikagua gwaride.

Twende kwenye hoja. Kwani kukagua gwaride inatakiwa utembee vipi??

Binafs nimezoea kumwona kiongoz yeyote hata katika nchi tofaut kupita karibu na wanajeshi na kukagua walivosimama kuashiria kukagua ukakamavu wao sasa hapa rais wetu alikua anakagua au apiga kwata??

Kutokana na mantiki ya kukagua umahili wa wanajeshi husika ilipelekea kusoma story za nchi ya ujeruman chini ya dicteta hitra. Kwamba ili kunyosha msitari wa gwaride alinyoosha na risasi japo sijui kama kweli. Ila nikajifunza kitu kimoja kwamba kwenye gwaride kama hilo haitakiwi kuwakuta watu wazembe wazembe na wenye matumbo aka vitambi.sasa rais wetu upande huu kuna mlinzi wake upande huu kuna mkuu wa majeshi yeye yuko kati na kainua kichwa juu pasipo kutizama anaowakagua akipiga gwaride balaa!! Ni kama waliopemben yake ndio ilitakiwa wakague japo wao hawakufanya hivyo maana si kaz yao. Alikua anakagua au anafundisha??

Tunajifunza nini kwa alivyofanya rais wetu ?? Kuna haja ya wanajeshi kujipanga na kukaguliwa??

Binafsi sijamwelewa naomba kueleweshwa.
Angalia video mwenyewe



Punguza kichwa maji utawaza vizuri
 
Hapo mbona alikuwavameshamaliza kukagua na alikuwa anaelekea jukwaani
Watu jamani mnakosoa na visivyokosoleka hata kama siasa siyo hivyo bhana maana mtatuchosha hata watu ambao hatufungamani na upande wowote wa siasa za vyama
 
Sasa kukagua gwaride inahitaji u-serious wa kiasi gani? Hizo ni formalities tu, Rais nae ni binadamu kama wewe na mimi.
Yes, formalities ziko pale to enhance some sort of discipline or control unwanted /unexpected behavior!

Formalities anafanya vitu viwe formal!
 
Jamani kwa hili wala sioni tatizo maana alishamaliza kukagua gwaride na pale alikuwa nakwenda jukwaani... sipendi jinsi anavyoendesha nchi lakni kwa lile la leo wala sioni tatizo.
 
bongo bhaaana.... sa kile ni kitu gani cha kukilalamikia na kukishangaa unaandika insha kabiiisa..... unalikuza na kulipamba kama jambo la listaajabisha saaana.... tuachane na hizi mambo ndogo ndogo... tafuta pesa
 
Naona kuna mnaomsifia alichofanya Rais na kuna mnaomponda. Kwani nini maana ya kukagua gwaride? Rais akiwa amiri jeshi mkuu na akipewa kazi ya kukagua gwaride anatakiwa akague gwaride na si vinginevyo. Alichokifanya Rais ni kupita mbele ya gwaride huku akipiga kwata kana kwamba yeye ndiye anakaguliwa. Tuache masihara kwenye mambo ya muhimu,sifa nyingine zinaiaibisha nchi.
kwani kaka... gwaride unakagua kitu gaaani.... unavyojua wewe
 
Back
Top Bottom