Hapa Rais wetu anakagua gwaride au anaonyesha gwaride?

Wife sijamuona mwenzenu au bado mgonjwa? M/Mungu amu afu Amin
 
Aisee,nimecheka sana,
Yeye kama kiongozi mkuu wa majeshi,anatakiwa kuwakagua vijana wake ka kweli wamepikwa na wameiva ikiwezeka kwa kuwakagua mmoja mmoja ,lakini sio yeye kuwaonyesha vijana kua yeye ni mkakamavu,asimame yeye basi wamkague.
 
Naona kuna mnaomsifia alichofanya Rais na kuna mnaomponda. Kwani nini maana ya kukagua gwaride? Rais akiwa amiri jeshi mkuu na akipewa kazi ya kukagua gwaride anatakiwa akague gwaride na si vinginevyo. Alichokifanya Rais ni kupita mbele ya gwaride huku akipiga kwata kana kwamba yeye ndiye anakaguliwa. Tuache masihara kwenye mambo ya muhimu,sifa nyingine zinaiaibisha nchi.
Wewe lofa hapo alikuwa ameshamaliza kukagua gwaride....
 
usitumie nguvu kutetea point, kitu sahihi huwa kinaeleweka haraka saaana
 
Kila jambo analolifanya mkuu wa nchi ni habari na ni somo!! Nimeshuhudia sherehe za uhuru nyingi na pia sherehe za kitaifa nyingi sana. Na pia rais wetu msataafu alikua mwanajeshi yamkini anajua kupiga kwata kuliko rais wetu magufuli. Lakn alitembea kawaida akikagua gwaride.

Twende kwenye hoja. Kwani kukagua gwaride inatakiwa utembee vipi??

Binafs nimezoea kumwona kiongoz yeyote hata katika nchi tofaut kupita karibu na wanajeshi na kukagua walivosimama kuashiria kukagua ukakamavu wao sasa hapa rais wetu alikua anakagua au apiga kwata??

Kutokana na mantiki ya kukagua umahili wa wanajeshi husika ilipelekea kusoma story za nchi ya ujeruman chini ya dicteta hitra. Kwamba ili kunyosha msitari wa gwaride alinyoosha na risasi japo sijui kama kweli. Ila nikajifunza kitu kimoja kwamba kwenye gwaride kama hilo haitakiwi kuwakuta watu wazembe wazembe na wenye matumbo aka vitambi.sasa rais wetu upande huu kuna mlinzi wake upande huu kuna mkuu wa majeshi yeye yuko kati na kainua kichwa juu pasipo kutizama anaowakagua akipiga gwaride balaa!! Ni kama waliopemben yake ndio ilitakiwa wakague japo wao hawakufanya hivyo maana si kaz yao. Alikua anakagua au anafundisha??

Tunajifunza nini kwa alivyofanya rais wetu ?? Kuna haja ya wanajeshi kujipanga na kukaguliwa??

Binafsi sijamwelewa naomba kueleweshwa.
Angalia video mwenyewe



hivi kwenye hiyo video uliyoweka inaonesha amesha maliza kukagua gwaride au anaendelea?
 
Mbona kafanya hilo akiwa ameisha maliza!!!!.

Na hata angefanyia katikati ndicho kwanza anatakiwa kufanya, wewe hukuona hata cdf, adc,pc hawakupata taabu kufuata step za mkuu wakati wanatembea pamoja.
 
Back
Top Bottom