Hapa nimebambikizwa au nimeibiwa mtoto?

Loliondo ni 400 Km kutoka Arusha na yeye alikua ameenda mara moja kufanya biashara sitaweza kumtress maadam namba sijabadilisha nasubiria muujiza kama atanitafuta
Nani kukwambia mtoto ni wako? Huyo mtoto si wako, anakupa stress za bure ujiongeze utume hela,

Siku ukikutana nae mwambie tupime DNA uone kama hatoruka mita mia😁😁😁😁
 
Nani kukwambia mtoto ni wako? Huyo mtoto si wako, anakupa stress za bure ujiongeze utume hela,

Siku ukikutana nae mwambie tupime DNA uone kama hatoruka mita mia
Dada samani kidogo rudi kwenye post soma btn lines, comments zitakutoa nje ya mstari, plz do read again, samahani lakini
 
Wanadumaa? Akikua pia baba atakua hajarudi au ndo inakuja kauli "alikufaga" maana ukisema alikukataa watoto wakishakua watakulazimisha ukawaonyeshe hata wamuone tu
Watoto huwa ni waelewa sana!
 
Habari za asubuhi ya jumapili wadau,

Kisa kipo huvii,

Ilikua mwaka 2015 nilisafiri kwenda mkoa wa Arusha wilaya ya Loliondo sana kutafuta riziki, huko nikakutana na mdada mzuri saaana mweupe kaenda hewani na shepu ya maana ni mdada wa Kiarusha/Mmasai, tukaJUANA kwa siku kadhaa then nilipomaliza kilichonipeleka huko, nikarudi zangu kwangu Iringa, tukaendelea na mawasiliano ya hapa na pale.

Hakuwahi kunipiga mzinga hata siku moja ila nlikua najiongeza mara kadhaa nlimuwezesha kiasi kidogo cha pesa coz show zake nlizielewa sana.

Baada na miezi kadhaa akaniambia kwamba amelazwa Mt. Meru hospital, nikampa pole na kumtumia kiasi cha pesa kwa ajili ya matibabu, baada ya kama siku 4 akaniambia ameruhusiwa na anarudi kwao Monduli.

Miezi mitatu baada ya kuruhusiwa hospitalini akaniambia kwamba ana mtoto, nilishangaa maana hakuwahi kuniambia ana mimba, nikampa hongera zake, akaitikia na kuniambia kwamba mwanae anafanana sana na mimi, sikutilia maanani, nikamwambia labda kwakua alinipenda ndomana mtoto anafanana na mimi.

Baada ya wiki 1 alipoona siunganishi matukio, akaamua kunichana kwamba mtoto ni wakwangu, duuuh! Nilistuka sana na kuanza kuhesabau siku, kwa kuwa tulipiga picha na nliziweka Dropbox ikabidi nizisake kujua tarehe nilizokutana nae.(picha huwa zina tarehe na saa ya picha kupigwa)

Nikaona zinaoana na siku alizolazwa Mt. Meru, nikasema mbona hukuniambia siku zote hizi ili nijue, akadai hakutaka kujipa stress maana huenda ningekataa na pia akadai yeye alipanga kuzaa na mimi kwa sababu ya muonekano wangu na kwamba mtoto ni wakwake na sio wetu.

Nilipatwa na mshangao sana, nikawa namuomba picha ya mtoto maana alikua na miezi 3 na wiki kadhaa ili nijiridhishe kama labda anafanana ni mimi akagoma katakata. Nikamuuliza sa alikua na sababu gani kuniambia kwamba ana mtoto wangu na hali hatuka hata nimjue? akasema amefanya ivo ili nijue nina mtoto na si kwa dhumuni la mimi kuhusika na mtoto.

Nilikasirishwa sana na hiyo tabia nikapanga kwenda kumsaha Monduli maana napajua nlisomaga A-level Moringe miaka ya 2000, nlipomweleza wazo hilo akaniambia atanitumia picha.

Nikasubiri kama wiki2 akatuma picha za mtoto ananyekaribiana umri na yule mtoto ila sura, rangi na muonekano vinatofautiana sana na jinsi aliponisimulia pindi aliposema mtoto wake alizaa na mimi na kwamba anafanana na mimi rangi hadi sura, mi nina rangi nyeupe kiasi na yeye ni mweupe saana, sa picha ya mtoto aliyotuma ni ya mtoti mweusi tii ana komwe kubwa kama mkenya (sina nia ya kumdharau huyu mtoto wa kwenye picha).

Nikahisi hapa nachezewa mchezo ili nisiende, nikasisitiza nia ya kwenda, akaniambia anabadilisha namba ya simu na kweli akawa hapatikani tena hadi leo, kwa kuwa Monduli ni kubwa saana kuanzia mto wambu, Monduli Juu, vijijini na sikujua nampataje nikashindwa kumtafuta na nimepoteza mtoto.

Wanawake bwana!! Kama aliamua kuzaa mimi ili apate copy yangu si angekaa kimyaa sasa napata shida kuona sijahusika katika maisha ya damu yangu, baadae mtoto aje kunitafuta ukubwani aseme baba yake alimkataa, pengine akamuacha kwa bibi yake akaenda kusaka maisha kwingine mtoto wangu akapata taabu na baba yake nipo.

Maoni yenu wadau
Baadhi ya wadada wa kabila hilo wanatabia hiyo so we jua mtot sio wako coz haina haja ya kuficha kama anavofanya huyo binti
 
Dah! Itakuwaje kama akinitafuta ukubwani ntamwambia nini, akijanilaumu?
Baadhi ya wadada wa kabila hilo wanatabia hiyo so we jua mtot sio wako coz haina haja ya kuficha kama anavofanya huyo binti
 
Back
Top Bottom