Hapa ndipo wanasiasa wetu uchwara wametufikisha watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hapa ndipo wanasiasa wetu uchwara wametufikisha watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KasomaJr, Oct 30, 2012.

 1. KasomaJr

  KasomaJr JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ni majira ya saa 12 asubuhi ya leo, naamka tayari kwa kujiandaa kama mtanzania mwingine yeyote mwenye kujituma, tayari kwa majukumu yangu ya leo, bila kusahau kuwa masuala ya kijamii nayo ni jukumu langu, nililazimika kuanzia hospitali kumwona baba mkwe wangu (mkubwa wake na baba wa mke wangu).

  Nilijianda tayari kwenda hospitali ya mkoa (wanasiasa wameipa jina-hospitali ya rufaa) nimefika na kumjulia hali mgonjwa wangu, huku nikitaka kujua ni huduma gani amepewa, na nini kinatakiwa kufanyika baada ya hapo, hakika mgonjwa bado aliendelea kulalamika kwa madai huduma si nzuri kwani tatizo ambalo limemfikisha hospitali bado halijafanyiwa uchunguzi na sababu kubwa hospital haina x-ray.

  Niliamua kuchukua hatua kujua ukweli toka kwa daktari mwenyewe, ukweli habari ilikuwa ni ile ile, hospitali haina x-ray, hivyo tunapaswa kwenda hospitali nyingine umbali wa kilometa 5-7( iliyokuwa hospitali ya kanisa na imetaifishwa na serikali muda si mrefu sana).

  Kama ndugu tusiopenda kumpoteza mgonjwa wetu, tulikubali kuchukua hatua (mimi na mdogo wake-Baba mkwe)..........nikiwa katika harakati za kujianda tumpeleke mgonjwa huko, nikabanwa kidogo kwenda haja ndogo, nilichokutana nacho ni hizo picha nilizo bandika hapa.

  Ni aibu na hatari sana kwa wagonjwa ambao wanahitaji tiba, wanahitaji kuwa mahali safi, kutumia vyombo na vitanda safi (vifaa vyote kwa ujumla wake), lakini badala yake mazingira ndiyo kama hayo.

  Hii ni sehemu tu ndogo tu ya matatizo yaliyojaa katika hospitali zetu. Imekuwa jambo la kawaida pia kusikia hakuna huduma ya ultra-sound badala yake tuifuate hospitali binafsi, hakuna huduma ya x-ray badala yake twende hospitali fulani.....sasa huu umekuwa utamaduni wa kawaida kabisa....sasa maswali yangu ni je:

  1. Hawa wakuu wa taasisi hizi muhimu ambao walaipwa kodi ztu watanzania, inakuwaje wanashindwa kusimamia hata usafi basi ukiachilia huu uhuni wa kuelekezwa wapi pa kupata huduma hizi muhimu?
  2. Je wizara ya afya inachukua hatua zipi kuondokana na huu upuuzi a eti hospitali ya serikali inakosa kifaa (ukarabati) wa vifaa hivi muhimu badala yake taasisi binafsi tena zilizo vichocholoni waweze kuwa nazo?
  3. Je ninyi wanasiasa ambao mnapigana kuchukua nafasi za hao walioshidwa kuwatumikia wananchi, mbona hatuo hatua zozote za makusudi kuikemea na kuiwajibisha serikali?
  4. Kwanini mmeamua kuwaongopea wananchi kuwa mnazipa hadhi hospital kadhaa kuwa za rufaa hali mkijua kabisa hazina vifaa muhimu kama hivi?

  Mtazamo wangu:
  Nadhani tunapaswa kufika mahali ambapo nchi yetu iongozwe kijeshi huenda tunaweza kupata ahueni, kwani sioni nia ya dhati ya wanasiasa (wapinzani na hata watawala) katika kuwasaidia wananchi katika hiki kidogo tu ambacho wananchi wanahitaji.
   

  Attached Files:

 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Duuuh! unapona ugonjwa na kupata ugonjwa mwingine! Ndio maana wenzetu wanaenda INDIA!
   
 3. mooduke

  mooduke JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Ndio sababu huwa nasema tuliingia choo cha kike kukubali Demokrasia
   
 4. W

  Wizzard Wweed Senior Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NCHI YA KITU KIDOOOOGO,ndo wimbo wa nchi yetu huo kila mtu kapewa kitu kidogona mwananchi nae anapewa kahuduma kadogo,Jeshi nao si wamo humohumo ! hawataki magamba yaondoke na wanatumiwa sana kuhakikisha magamba wanaendelea kuwepo.
   
 5. t

  tenende JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  vyoo hivyo mbona cha mtoto? Kipo choo kimoja Udsm karibu na ATB lecture room, na hospitali ya wilaya Bagamoyo (nilikuwa huko wk 3 zilizopita) hali ni mbaya. Magogo yanaelea kila mahali.
   
 6. Umslpogaaz

  Umslpogaaz Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 14, 2008
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ili tupate mabadiliko, ccm lazima iondoke. Vinginevyo tutabakia hivyo hivyo!
   
 7. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Wenyewe madaktari wanayaita haya magonjwa unayopata hospitali unapokwenda kuugulia huko "nosocomial infections". Ni hatari hasa kwa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji. Nilikuwa nashangaa sana, kwa nini waganga wa mifugo wanampasua ng'ombe kwenye zizi na anapona, lakini binadamu anafanyiwa kwenye chumba maalumu, kwa kuzingatia taratibu zote za usafi lakini kidonda kinapata infections!
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Umeona, eeh?
   
 9. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  kwa yanayoendelea ndani ya vyama vya upinzani ambavyo bado havijashika dola napata wasi wasi kama hata wakishika dola leo watafanya lolote au wataiba kwa nguvu zaidi
   
 10. mathcom

  mathcom JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,402
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  kama wanasiasa wanaenda India kucheki malaria wafikiri watayaona haya! hii ni hatari ni ajabu kusikia mtoa msaada
  wa chakula
  kafa kwa njaa hii ndio hali ya usafi ya wapenda usafi... crazy...
   
 11. mathcom

  mathcom JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,402
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Wakikusikia..... lakini ni suala zuri la kujiuliza, jee kila mpinzani ana lengo la kuwahudumia watanzania ambao walio
  wengi ni masikini!!!!
   
 12. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Kikwete akipata habari hii, atakwambia huo ni uongo. X-ray zipo kila hospitali na zinafanya kazi hata CT Scan zipo za kutosha... Labda wewe ni chadema ndiyo maana hausifii jitihada za CCM na serikali iliyoko madarakani.

  Kuhusu hospitali ya mkoa kuitwa ya Rufaa, uliza nini kiliongezeka kuonesha kuwa imepandishwa hadi!!!!!! Hakuna ni jina tu. Nakubaliana na wewe kuwa ni kisiasa ili watu waseme "Tuna hospitali zaidi ya 20 za Rufaa nchini.

  Pole Mheshimiwa JK
   
 13. S

  SJUMAA26 JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 611
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wewe unampa pole M.k.w.e.r.e ambaye kila baada ya siku mbili yuko Ughaibuni akiendeshwa na mkokoteni wa farasi badala ya kujipa pole wewe na maskini Watz ambao ukosefu wa chandarua cha Shs. 8,000/= tu kunagharimu masha yake? Mama zetu wanapoteza maisha kwa kukosa elfu 5 tu za kununulia vifaa vya kujifungulia, wakati M.k.w.e.r.e anapangisha vimada kwenye kila mji ndani na nje ya Jamhuri yetu hii, sasa hapo nani wa kupewa pole?
   
 14. andate

  andate JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 2,655
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni kwamba mtanzania anataka mageuzi bila yeye kubadilika na bila yeye kuchangia hayo mageuzi. Hata hao waangalizi wa usafi wa hivyo vyoo ukikutana nao uraiani watakwambia wanataka mageuzi wakati wao hawafanyi kazi yao ipasavyo.
   
 15. k

  kaguru Member

  #15
  Oct 31, 2012
  Joined: May 11, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  duuh!!!!!jamani mafagio na dawa za kusafishia choo nazo pia zahitaji kuundiwa tume??????????au ndio vipo kwenye mchakato wa kununuliwa???????????????????????????????AIBU KWA UONGOZI WA HOSPITALI KUBWA KAMA HIYO.
   
 16. YAGHAMBA

  YAGHAMBA JF-Expert Member

  #16
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 538
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  CDM imefanya bidii matatizo ya sekta ya afya yajadiliwe bungeni wakati mgomo wa madaktari lkn serikali ya CCM ilikataa
   
 17. K

  Kirokolo Senior Member

  #17
  Oct 31, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 196
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Kweli hali hii ni hatari na inatisha. Ni hospitali gani hiyo ya rufaa ndugu? Tuaomba jina tafadhali ili tuanza na huyo daktari mkuu. Hali hii haivumiliki hata kidogo.
   
 18. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Hizo hospitali zetu ziko hivyo kwa vile viongozi wetu hawazitegemei kutibu afya zao
   
Loading...