Hapa ndipo pa kuwatambua wabunge wenye kufahamu wajibu wao bungeni. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hapa ndipo pa kuwatambua wabunge wenye kufahamu wajibu wao bungeni.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WATANABE, Apr 14, 2011.

 1. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Si wabunge wengi hususan kutoka CCM wanatambua wajibu wao ndani ya jengo lile kwa mujibu wa KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
  TANZANIA YA MWAKA 1977
  ibara ya 63.-

  (2) Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha
  Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa
  niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri
  ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa
  majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.


  Laiti kama wabunge wetu wangekuwa wanatambu wajibu wao kwa mujibu wa Ibara ilioyotajwa hapo juu wangefanyia kazi taarifa kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali aliyoitoa hivi karibuni wangembabana Waziri Mkuu na mawaziri kwa kushindwa kutekeleza mapendekezo ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali yaliyolenga kupunguza matumizi ya serikali na kuongeza mapato; na kukaiidi kutoa taarifa mbali mbali zilizohitajika.

  Ni dhahiri kuwa ili wabunge waweze kuibana serikali kwa kutumia taarifa kama hizi ni lazima wabunge wafanya utafiti wa kina na kusoma nyaraka mbali mbali ili kwanza waweze kujielimisha vya kutosha kuhusu uzembe na ufisadi ulioko ndani ya serikali ili waweze kuuliza maswali yenye kuweza kuwabana waziri mkuu na mawaziri ipasavyo.

  Kwa hali hiyo mbunge yeyote ambaye kila kukicha anawaza atakavyoweza kupata fedha za kupelekea maji. elimu, barabara, zahanati, hospitali n.k kwa wapiga kura wa jimbo lake ili aweze kuchaguliwa tena hawezi kuwa na muda wa kuwekeza katika kujielimisha ipasavyo ili aweze kuuliza maswali yatakayoweza kuwabana watendaji wa seikali ipasavyo. Hivyo basi kutokana na wabunge wetu wengi kushindwa kujielimisha vya kutosha kuhusu taarifa mbali mbali za utendaji wa serikali hushindwa kuuliza maswali yenye kuweza kuwabana waziri mkuu na mawazsiri wake hali ambayo hufanya serikali kupoteza fedha nyingi sana kama anavyolalamika Mkaguzi kuu wa Hesabu za Serikali.

  Wananchi wana mchango mkubwa sana katika kukuza tatizo hili kutokana na kuwapima wabunge wao kwa huduma na miradi ya maji, elimu, barabara, zahanati, hospitali n.k itayoletwa na wabunge katika jimbo fulani hata kama huduma na miradi hiyo inatokana na wabunge wao kushiriki ufisadi wa taifa kama iivytokea katika majimbo ya Monduli kwa Lowassa, Igunga kwa Rostama Azizi na Bariadi kwa Andrew Chenge.

  Vyama vy Upinzani vinapaswa kutoa elimu ya uraia kwa wananchi ili wafahamua kuwa sio jukumu la mbunge kuleta huduma na miradi ya maji. elimu, barabara, zahanati, hospitali n.k katika jimbo lake bali mbunge hutakiwa kusimamia mapato ya serikali nzima na upatikana ji wa huduma hizo kwa uwiano nchi nzima baada ya raslimali za taifa hili kutunzwa na kutumika vyema.  CAG ‘alalamika kupuuzwa’ na Serikali.

  Imeandikwa na Na Shadrack Sagati; Tarehe: 13th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 21; Jumla ya maoni: 0

  SERIKALI haikutekeleza mapendekezo yote 15 yaliyotolewa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) mwaka 2010, hali aliyoieleza kuwa inakwamisha ufanisi serikalini na katika mashirika ya umma.

  CAG amelalamikia hatua hiyo ya Serikali katika ripoti yake ya mwaka 2010, iliyotolewa wiki hii na kuorodhesha mapendekezo yote aliyotoa huku akionya kuwa kudharauliwa kwake, kutasababisha kukwama kwa shughuli za maendeleo.

  Baadhi ya mapendekezo aliyosema hayakufanyiwa kazi ni pamoja na ushauri wa kuitaka Serikali ipunguze ununuzi wa magari ya kifahari na kupunguza gharama za warsha, ili mapato yanayokusanywa yatumike kwenye shughuli za maendeleo.

  Pia alilalamikia kutotekelezwa kwa mapendekezo ya kuondoa wabunge kuwa wajumbe wa bodi za wakurugenzi wa mashirika ya umma, ili kuepuka mgongano wa maslahi kwa kuwa ni wabunge hao hao wanaosimamia utendaji kazi za mashirika hayo kupitia Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC).

  Mapendekezo mengine aliyolalamikia kutotekelezwa na Serikali ni kuboresha ukusanyaji mapato kutoka vyanzo mbalimbali, kuziba mianya ya ukwepaji kodi hususani kwenye mafuta ya magari na mitambo, kupunguza misamaha ya kodi na kupanua wigo wa kodi.

  CAG alisema katika ripoti hiyo, kuwa hata alipoomba maelezo ya kina kuhusu uhalali wa malipo ya dola milioni 4.8 za Marekani kwa kampuni ya M/s Dowans kwa ajili ya kukodisha ndege maalumu, Serikali haikumpa majibu yoyote sasa yapata mwaka.

  Mbali na maombi ya kupata taarifa za Dowans ambayo hayajatekelezwa, CAG alilalamikia pia ushauri wake wa Serikali kuligawa mara mbili Shirika la Maendeleo ya Petroli la Tanzania (TPDC); shirika moja lishughulikie biashara na lingine litoe leseni, ukaguzi na kufanya kazi za udhibiti, ili kuleta ufanisi katika biashara ya mafuta, haukutekelezwa.

  Mapendekezo mengine aliyosema yalipuuzwa ni kuruhusu Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC), kusimamia hesabu za mashirika na kampuni zote ambazo Serikali ina hisa.

  Mkaguzi huyo pia alipendekeza bodi za wakurugenzi za mashirika ya umma kuhakikisha watendaji wakuu wa mashirika hayo wanawajibika zaidi kwa matokeo ya utendaji kazi wao, lakini alieleza kuwa ushauri huo haujatekelezwa.
   
 2. G

  GAMA LUGENDO Senior Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wabunge wengi wameenda kwa ajili ya ulaji na siyo kuwatumikia kiukweli wananchi wa Tanzania.This explains why wanajipangia posho na marupurupu makubwa sana.Everything has got its own end, ninaamini si muda mrefu bungeni wataanza kuingia watu wengi wenye uchungu na matatizo ya raia wa nchi hii.
   
 3. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  At least Zitto ameanza kukomaa kuhusu masuala haya. Inaonyesha wazi kuwa anafahamu ni kwanini yupo ndani ya jengo hilo. Nimemsikia Waziiri Mkuu akijibu swali hakuwa nataarifa hizo kuwa Mkaguzi Kuu wa Hesabu hakupatiwa ushirikiano na watendaji wa Serikali. Majibu kama haya ndio yanachochea umaskini hapa nchini. Tunataka kuona hatua gani zinzchukuliwa dhidi ya Afisa aliyeshindwa kumpatia Mkaguzi Mkuu taariofa alizohitaji.
   
 4. m

  magiri Member

  #4
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ugonjwa unaoikabiri nchi hii ni kutojali, na kuishi maisha ambayo siyo principled. mpaka viongozi wetu wakuu watakapojali na kuishi maisha yakanuni ndipo tutakapofanikiwa. waziri mkuu kutojua aliyokumbana nayo CAG,wala mimi sishangai maana he is too diplomatic pamoja na rais wake. ndiyo maana magufuli amezuiwa kubomoa barabara ingawa alikuwa anatekeleza sheria.(principle). he really knows how to play with words though at the end you dont see anything tangible on the ground. mashangingi aliyokataa ndo yamezidi, wizi na ubadhirifu wa mali za umma ndo umeongezeka. people dont care how much you talk,they want to know how much you care. viongozi wetu wasipojali hakuna atayeogopa, na ole wetu kwa sababu tunajenga ujasiri wa kifisadi ndani ya watu maana baada ya maneno tupu ya watawala wetu huwa hakuna utekelezaji wowote.
   
 5. k

  kakini Senior Member

  #5
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hakuna uwajijibikaji hapo katika serikali ya CHICHIEMU
   
 6. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kamati ya bunge ya hesabu za serikali chini ya Cheyo ingelikuwa makini ndiyo ingelitakiwa kuwaweka wahusika kwenye kiti moto kuhusiana na kupuuza hoja hizi za ukaguzi; lakini ni dhahiri mwenyekiti huyo tayari kishawekwa mfukoni , mdiyo maana serikali ilikuwa ikimgangania aendelea kubakia na wadhifa huo.
   
 7. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Sasa kama Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali imewekwa mfukoni sisi wananchi tunafanya nini kuhusu hilo. au na sisi tumewekwa mfukoni?
   
Loading...