Hapa ndipo ninapowadharau na kuwapuuza Viongozi na Mashabiki baadhi wa Simba Sports Club

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,542
108,852
Kwa aina hii ya ' Upuuzi ' ninaouona ndani ya Klabu ya Simba kuna uwezekano nikajipa ' Mapumziko ' ya Kuishabikia na nikabaki tu kushabikia Klabu yangu ya Liverpool ya nchini Uingereza kwani nimechoka japo tunajitahidi Kushauri.

Hivi inaingia akili leo hii unamuacha Beki bora, mahiri, makini na katili kwa ' Mafowadi ' Juuko Murshid na unamchukua Pascal Serge Wawa?

Kuna mfuatiliaji na mdau wa mpira leo unaweza ukamshawishi kwa kumwambia kwamba Pascal Wawa ni mzuri kuliko Juuko Murshid? Hivi Mchezaji ambaye panga pangua katika Kikosi cha Timu yake ya Taifa ya Uganda ( The Cranes ) yumo unaweza ukamfananisha na Mchezaji ambaye hata hajawahi kufikiriwa kuwemo katika Kikosi chake cha Taia cha Ivory Coast?

Viongozi wa Simba SC msidhani na sisi akina GENTAMYCINE labda hatujacheza mpira au hatuujui na pengine kuna uwezekano mngeniona enzi zangu nikikamata Dimba la Chini namba 6 au nikicheza ' Shavu ' la Kulia na Kushoto basi leo hii mngenisajili kwa ' Mamilioni ' ya Pesa sema tu ' Majukumu ' ya Kitaaluma / Kielimu yalinizidi na kupeperusha ' ndoto ' yangu Kimpira.

Kama Mchezaji Juuko Murshid anataka ' dau ' kubwa mpeni haraka tafadhali kwani bado ana umuhimu mkubwa sana Kikosini na ana uwezo mzuri ambao utaisaidia Simba SC yetu katika Ligi na michuano ya Kimataifa.

Kuna siku ' mizimu ' yangu ikipanda nitamtaja Kiongozi mmoja wa Simba SC ambaye ndiyo ana ' chuki ' zake binafsi na Mchezaji Juuko Murshid kwakuwa tu alikataliwa kupewa 10% kama ambavyo amezoea Kuchukua kutoka kwa Wachezaji wengine baadhi.

Na kamwe nyie Viongozi wa Simba SC msidhani nyie kuwa huko karibu na Timu labda Sisi wengine huku nyuma hatujui lolote linaloendelea. Binafsi nina ukaribu karibu na 75% ya Wachezaji wa Simba SC na kuna mengi tu ambayo huwa wananiambia ila kwa kuiheshimu tu Klabu yangu na nisiwape Wapinzani wetu ( Yanga SC ) faida huwa naamua tu Kuuchuna / Kupotezea lakini nina mambo mengi ' chini ya Kapeti ' yanayoendelea huko.

Naomba Mchezaji na Beki mahiri kutoka nchini Uganda Juuko Murshid asiachwe na achaneni na huyo Beki Pascla Wawa kwani hana jipya kwa sasa na nimemwona katika mechi mbili za hivi karibuni huko mbeleni atakuja kutoponza na ' kuchomesha ' mno na mtayakumbuka haya maneno yangu na huu ' Uzi ' wangu.

Nawasilisha.
 
Yaani inashangaza sana tu Mkuu na ndiyo maana uvumilivu umenishida na nimeamua kuwapa ' makavu ' yao.
Kwa asilimia kubwa viongozi wa timu zetu kubwa apa bongo wako kwa maslahi yao binafsi na si kwa ajili ya kusaidia timu kwa hiyo mkuu Genta usishangae hayo kutokea
 
Back
Top Bottom