Uchaguzi 2020 Hapa Mtaani CCM hawapo tena siwaoni

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,944
3,820
Sio kama siku za mwanzo za mwezi huu wa hekaheka za uchaguzi njano na kijani utafikiri msimu wa maua, ila hivi sasa wanaovaa njano na kijani hapa mtaani wamekuwa adimu sana.

Wengi niliokuwa nawafahamu wamebadilika kimawazo na fikra zao sasa zinaona mbali,wamegundua shida na dhiki za maisha sababu ni kuitukuza CCM na kuwapigia makofi wenyeviti na meza.

Wameanza kuwa huru kifikra mambo ya kupewa fulana na suruali za kijani na njano na kikofia cha kijani wanasema wale wakinunua utu wetu kwa vipande vya vitambaa tu.Kumbe huwa wameficha ubaya wao.

Jamani kukataliwa kubaya CCM sasa inakataliwa kila sehemu ya Tanzania hii,wakubwa,vijana wazee na watoto wanaikwepa CCM ,CCM msiwe wabishi kubalini hii hali inayotokea. Ni mabadiliko ya tabia nchi lazima myakubali.
 
Inasababisha hasira lakini jiwezesheni kuyakubali matokeo na hasira zitawaondoka na kuwa raia watiifu sio mnaandaa mbinu hatari za kulazimisha kuchaguliwa au kujichagua mtaumia umma sasa upo upande mwengine hamtopata pa kujificha..
 
Toka 2010 haya maneno mnayasemaga, lakini ukifika wakati ku face sanduku la kura, hao ambao huwaoni mtaani utawaona. Mlihamashishwa kwenda kujiandikisha mka sepa. We jipe moyo ukidhani ni utani. Bashiru aliwaonya kuwa alisha set mitambo ya ushindi
 
Kwa mtu yeyote mwenye akili, anajua wanaoshabikia sisiem ni wale wajinga wasiojua kupambanua mambo, wasio na maamuzi yao binafsi, wanaotegemea fulani aseme jambo ili wao wakubali.....

watru kama hawa ni rahisi sana kuwayumbisha, huwa wakipata mtu anayeweza kuwasemea vyema, ni rahisi sana kubadili misismamo yao....

fursa hiyo iliminywa kwa miaka mitano, hivyo wakapata mtu anayeendesha mambo kipropaganda, asiye muwazi aliyeamua kufuta sheria ya uwazi na uwajibikaji huku akieneza propaganda ya kwamba yeye anawajibika...

Sasa kaja mtoa mwanga wa fikra, muwazi, mwenye kunena na kutenda kweli kwani matendo yake yalidhihirika tangu alipowatetewa masikini kwa vitendo....

Kwa hiyo lazima hao watu wabadilike... na hii ni mwezi mmoja na nusu tu....

Hata ikitokea lisu hakutangazwa, naamini 2025 anachukua ikiwa mazingira ya kufanya siasa hayataminywa.
 
Hata humu jukwaani wengi wao pumzi zimewakata! Ujasiri wa kuisifia serikali yao kandamizi, umepungua! Bia yetu hajulikani yuko wapi!! Hali ni tete.
Jiwe kakataa proposal ya kuwalipa wapiga debe wa ccm mitandaoni .
Screenshot_20200915-230851.png
 
Sio kama siku za mwanzo za mwezi huu wa hekaheka za uchaguzi njano na kijani utafikiri msimu wa maua, ila hivi sasa wanaovaa njano na kijani hapa mtaani wamekuwa adimu sana.

Wengi niliokuwa nawafahamu wamebadilika kimawazo na fikra zao sasa zinaona mbali,wamegundua shida na dhiki za maisha sababu ni kuitukuza CCM na kuwapigia makofi wenyeviti na meza.

Wameanza kuwa huru kifikra mambo ya kupewa fulana na suruali za kijani na njano na kikofia cha kijani wanasema wale wakinunua utu wetu kwa vipande vya vitambaa tu.Kumbe huwa wameficha ubaya wao.

Jamani kukataliwa kubaya CCM sasa inakataliwa kila sehemu ya Tanzania hii,wakubwa,vijana wazee na watoto wanaikwepa CCM ,CCM msiwe wabishi kubalini hii hali inayotokea. Ni mabadiliko ya tabia nchi lazima myakubali.

Ni Kweli Kipindi cha Rais Mstaafu JMK CCM 'ilichokwa' sana na Watu ila kwa CCM hii ya Rais JPM sasa 'imeshakinaiwa' na wale Walioiamini sana tu.
 
Wanasubiri NEC ifanye yake
 
Ni Kweli Kipindi cha Rais Mstaafu JMK CCM 'ilichokwa' sana na Watu ila kwa CCM hii ya Rais JPM sasa 'imeshakinaiwa' na wale Walioiamini sana tu.

Huwa ninapokuelewa ni hapa tu! Wewe ni CCM kindakindaki! Na pia ni shabiki lialia wa Simba! Lakini kwenye kusema ukweli, huwa unajitahidi sana!

Hongera sana kwa hilo. Hakika ukweli utakuweka huru. CCM ya awamu ya Magufuli imechokwa na kila mtu! Mpaka wanachama wenyewe nao wameichoka! Huku Mwenyekiti akichangia karibia nusu ya huko kuchokwa kwake.
 
Back
Top Bottom