Hapa mh unatupeleka wapi?

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
505
871
Rais Magufuli unaelekea unataka kuwa kubwa la maadui!! Mimi sijapendezwa na kauli za kibaguzi ulizozitoa kwa Wabunge wa Chama chako!!

Hizi ni kauli za kichochozi na za kuligawa Taifa letu lenye misingi ya Uhuru na Umoja, hapa Rais Magufuli umekosea! ni kweli kumtemblea mbunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg Godbless Lema gerezani ni usaliti kwa chama chako CCM na dhambi?

Rais Magufuli unaanza kubomoa misingi ya Taifa letu, hii ni Ishara ya Udikteta, visasi, na ukosefu wa hekima, maarifa, busara, ujuzi na uvumilivu. Taifa hili limeasisiwa vyema na kukomeshwa kwa ubaguzi wa aina yoyote Ile sasa unataka kutuletea ubaguzi turudi enzi zile!! hapa Rais Magufuli umewakosea Watanzania!!

Hii siyo tabia ya kuigwa na Mtanzania yeyote yule wala kizazi chochote kile katika Africa!

Nafikiri Watanzania sasa mnaendelea kuona Rais tuliyemchagua kwa kura na kumpa mamlaka ya kusimamia misingi ya Taifa ikiwemo katiba na sheria zetu sasa anaanza kuleta sura ya sitofahamu katika Taifa letu! Ni yeye yule anaye hubili amani na kuwa yeye ni mpenzi wa Mungu na Maendeleo hayana chama wala itikadi! Maneno yake hayasawili rangi yake halisi hakika Taifa letu linapomoroka kwa nguvu!

Rais Magufuli hii siyo poa kabisa.

Na Nicolas Jovine Clinton.
 
Mkuu umemwambia kiziwi yaaani yeye ndo kwanzaaa pamekucha kesho utasikia kauli nyingine Kali zaid ya hiyo

Eti mkuu baba mwenye nyumba anapimwaga akili kama ziko timamu au laa kabla ya kukabiziwa nyumba??

Maana baba mwenye nyumba yetu me na wasiwasi nae
 
Hawa watu bwana wanachezea na kidhihaki majina matakatifu, ukiwasikia "inchi hi ni ya jamani! Msema ukweli mpenzi wa Mungu!"wakiwa kanisani/msikitini utadhani wana roho nzuri na za kuigwa kinyume chake roho zao zimejaa kitu za visasi na uonevu wa hali ya juu.
 
Hawa watu bwana wanachezea na kidhihaki majina matakatifu, ukiwasikia "inchi hi ni ya jamani! Msema ukweli mpenzi wa Mungu!"wakiwa kanisani/msikitini utadhani wana roho nzuri na za kuigwa kinyume chake roho zao zimejaa kitu za visasi na uonevu wa hali ya juu.
 
Back
Top Bottom