Hapa mama Maria kawapasha au kuwafunda wake za watawala wetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hapa mama Maria kawapasha au kuwafunda wake za watawala wetu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Father of All, Feb 27, 2012.

 1. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mwanzo » Habari

  Mama Maria ataka wake za viongozi kutambua dhamana zao


  Na Mwandishi wetu

  26th February 2012

  Mke wa Hayati Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere amewataka wake wa viongozi kutambua dhamana walizonazo na wajibu walionao kwa jamii ambayo wenzi wao wanaiongoza.

  Alitoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa akiwashukuru wake wa viongozi 25 ambao walifika nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam ili kumjulia hali na kumpa tuzo ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.

  Mama Maria alisema kuwa wake wa viongozi kunawafanya wakutane na changamoto nyingi lakini pia akawataka watambue kuwa Taifa limewapa fursa ya kuelewa mengi ambayo kama wangekuwa wanawake wa kawaida tu wasingeweza kujua mambo hayo.

  "Unapokuwa mke wa kiongozi unapata changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kutoa dira kwa wengine...unapaswa kufikiri kwa niaba ya wengine iwe ni kwenye ujasiriamali, elimu, afya au masuala ya kijamii hasa namna ya kukabili changamoto za akinamama na watoto," alisema.

  "Unapokuwa mke wa kiongozi unapaswa kumshukuru kwa kuwa umepewa fursa ya kuwaongoza wengine, umepewa fursa ya kukomaa na mawazo yanakua kwa haraka kuliko wengine wasio na fursa kama yako," alisisitiza.

  Alisema inawezekana watu wa nje wakawaonea wivu kuwa wamepata bahati ya kuolewa na viongozi lakini wajibu wao mkubwa siku zote uwe ni kuwaombea wenzi wao na wale wanaowaongoza.

  "Msichoke kumuomba Mungu kwa sababu ninyi ndiyo mna kazi kubwa, mnasimama kwa niaba ya taifa... lolote likitokea linawakumba na ninyi pia," aliongeza.

  Mapema, akitoa salamu za ujio wao, mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda alisema wameamua kumpa tuzo ya heshima Mama Maria Nyerere kwa sababu wanatambua mchango wake wakati aliposhiriki bega kwa bega na hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye harakati za uhuru wa Tanzania.

  Akizungumza kwa niaba ya wake wa viongozi mbalimbali wa kitaifa 25 ambao aliongozana nao, Mama Pinda alisema tuzo waliyompa imeandikwa "Hongera Mama wa Taifa" ikiwa ni kuthamini mchango wake. Tuzo hiyo ina umbo la ramani ya Tanzania, ina nembo ya miaka 50 ya Uhuru pamoja na picha ya Mama Maria Nyerere.

  Baadhi ya wake wa viongozi walioambatana Mama Pinda ni wake wa Marais wastaafu Mama Sitti Mwinyi na Mama Anna Mkapa, Mke mkubwa wa Makamu wa Rais, Bi. Zakia Bilal, Mama Salma Omar (mke wa marehemu Dk. Omar Ali Juma), Mama Hasina Kawawa, na wake wa Mawaziri, Naibu Mawaziri na Makatibu wakuu.

  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

   
 2. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #2
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280

  Mama Salama KIkwete ...hakuhudhuria
   
 3. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,930
  Likes Received: 1,462
  Trophy Points: 280
  alikuwa na wito maalum:nono:
   
 4. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  hajalipa ada ya kikundi wakampotezea
   
 5. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  mumewe sio mstaafu,ila mama Lowasa ne sajui alienda?au mumewe pia sio mstaafu?
   
 6. n

  ngoshas JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 710
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kawapasha
   
 7. F

  FUSO JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  katika wote mke wa rais wa awamu ya pili ni kiboko - yaani hata machoni kwake anaonekana tu.
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,325
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Akishakaa benchi atajirudi
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Mama Salma akiwa benchi atakuwa anajificha sana maana walivyoharibu sidhani kama watakuwa wana raha kukatiza hivi....subiri uone tuhuma zao hapo jan 2016 utachoka!!
   
 10. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kivipi?
   
Loading...