Hapa Kwetu mtendaji wa kata mwenye elimu ya cheti ni bora kiliko mwalimu mwenye masters degree

Sekta ya elimu ndio in awatumishi wa uma wenye elimu ya juu kabisa. Kwa mfano kwa shule za sekondari mwalimu mwenye elimu ya chini kabisa ni diploma. Wapo walimu wana Masters na PhD . Lakini cha kushangaza mtendaji wa kata mwenye elimu ya cheti kutoka Hombolo ana mamlaka na hadhi kuliko hawa wasomi waliobobea kwenye masomo yao kama Physics, Mathematics , Biology,Chemistry na n.k .

Kwa macho yangu nikiwa kwenye kikao cha wazazi katika shule moja ya Sekondari. Nilimuona mtendaji wa kata husika akiwachimba mkwara walimu na kuwaambia kuwa yeye ni boss wao kwenye hiyo kata.
90% ya waratibu wa wizi wa kura za ccm ni walimu mkuu.hawa wanajua kila kilichotokea 2020. Pale yule raisi kichaa aliyekuwa na betri kwenye moyo wake alipora kura.
Hawa wanapaswa kuchapwa kabisa. Ndiyo wanaongoza kulala kwenye mwenge
 
Wewe jamaa umenichekesha sana... nikakimbilia kweli nikijiuliza (nikitaka kujua) ni bora kwenye nini? Tena akili yangu nikaenda mbali kweli ila kusoma maudhui khoo...!
 
AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA II (WARD EXECUTIVE OFFICER GRADE II) – NAFASI 20

1.1 MAJUKUMU YA KAZI

Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika kata na atashughulikia masuala yote ya kata

• Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbal.i ya uzalishaji,

mali, kuondoa njaa na Umasikini.

• Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.

• Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya kata, vijiji na Mtaa.

• Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibu na kusimamia shughuli za Uchaguzi katika Kata.

• Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo lake.

Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katikangazi ya Kata.

• Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na nakala kwa Katibu Tarafa.

Atakuwa mwenyekiti katika vikao vinavyowahusisha wataalamu na watendaji wa vjiji, na NGO’S katika kata yake.

• Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika vijiji, vitongoji, na kata yake.

Kwa kuongezea pia WEO ndo msimamizi mkuu wa ulinzi na usalama ngazi ya kata.
 
Sekta ya elimu ndio in awatumishi wa uma wenye elimu ya juu kabisa. Kwa mfano kwa shule za sekondari mwalimu mwenye elimu ya chini kabisa ni diploma. Wapo walimu wana Masters na PhD . Lakini cha kushangaza mtendaji wa kata mwenye elimu ya cheti kutoka Hombolo ana mamlaka na hadhi kuliko hawa wasomi waliobobea kwenye masomo yao kama Physics, Mathematics , Biology,Chemistry na n.k .

Kwa macho yangu nikiwa kwenye kikao cha wazazi katika shule moja ya Sekondari. Nilimuona mtendaji wa kata husika akiwachimba mkwara walimu na kuwaambia kuwa yeye ni boss wao kwenye hiyo kata.
Hata bwana Yesu alikuwa Mwalimu (Rabi) lakini taaluma yake ilichezewa vivyohivyo
 
nadhani mtoa mada haelewi mifumo ya serikali ilivyo, huyo mwalimu sio kuwa anaonewa , ni suala la hierarchy tu

mwalimu yuko chini ya headmaster wake, headmaster yuko chini ya afisa elimu kata, afisa elimu kata yuko chini ya huyo ward executive officer

😀😀
💯
 
Tatzo ujui majukum ya mtendaji wa kata ndio maana umeandika hvyo.
Tunataka watu waheshimiane kwa kiwango cha taaluma. Mbona wanajeshi wana utaratibu mzuri tu. Kazi anazozifanya Huyo WEO ,hata darasa la saba anaweza kuzifanya. Tatizo hili taifa linapuuza sana wanataaluma , dio maana ujinga ni mwingi.
 
Mwalimu anafundisha shule yake moja lakini mtendaji kata anafuatilia maendeleo kata nzima yenye taasisi zaidi ya moja,ukitaka utambulisho wa barua za kiserikali ngazi ya kata ni mtendaji kata atakutambulisha na sio mwalimu,sijui ulitaka kumaanisha nini?so mtendaji anamamlaka kiutawala kuliko mwalimu
Mtendaji wa kata/kijiji ndiye kama waziri mkuu wa eneo husika.

Mambo yote yanayohusu utendaji yako chini yake na ndio maana serikali imempatia wataalamu wa kufanya naye kazi.
  • Afya ( Afisa Afya aka Bwana au Bibi Afya )
  • Ustawi wa Jamii ( Afisa maendeleo ya Jamii )
  • Elimu ( MEK, Mratibu Elimu Kata )
  • Kilimo ( Bwana Shamba na Afisa Mifugo )
  • Biashara ( Afisa Biashara )
  • Siasa na utawala ( Mwenyekiti wa serikali ya mtaa/kijiji ) - huyu huchaguliwa na wananchi wenyewe.

Sasa kuhusu upande wa elimu, Mtendaji wa Kata/kijiji anafanya kazi na MEK ambaye ni boss wa Walimu, kwanini asiye juu ya mwalimu ?

Kumbuka MEK ni Afisa Elimu ngazi ya kata. Sema mara nyingi MEK huwa wanapewa walimu wa primary na hivyo kwa walimu wa sekondari kuona kama wananyanyasika kuwa chini ya watu wanaowazidi sometimes kielimu.
 
Tunataka watu waheshimiane kwa kiwango cha taaluma. Mbona wanajeshi wana utaratibu mzuri tu. Kazi anazozifanya Huyo WEO ,hata darasa la saba anaweza kuzifanya. Tatizo hili taifa linapuuza sana wanataaluma , dio maana ujinga ni mwingi.
Issue siyo taaluma.

Tofauti ni majukumu.

Hata Nurse akiwa na Masters bado huko hospitali atatakiwa kumsikiliza tabibu.

Usitafute ukubwa kwa kuvimba, tekeleza majukumu yako kwa mujibu wa mkataba wako.
 
Tunataka watu waheshimiane kwa kiwango cha taaluma. Mbona wanajeshi wana utaratibu mzuri tu. Kazi anazozifanya Huyo WEO ,hata darasa la saba anaweza kuzifanya. Tatizo hili taifa linapuuza sana wanataaluma , dio maana ujinga ni mwingi.
Tatizo sio kiwango cha elimu ulicho nacho issue ni majukumu.
 
Back
Top Bottom