Hapa kazi tu! Strategists yapaswa wamkumbushe raisi apange vema team zake la sivyo...!

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Najaribu kuiangalia kauli mbiu ya Magufuli na kinachotokea mjini!
Hadi sasa ameshamaliza karibu theluthi nzima ya mwaka akiwa ofisini Magogoni. Yes anapiga kazi tena ni one man show, Ila kazi anayoifanya ni aina moja tu, sasa hata ktk jeshi la siafu, nyuki, mchwa utaona kuna mgawanyo mkubwa wa shughuli, wengine wanazaa tu, wengine wanategemea au kuleta chakula, wengine wanaolinda, yaani ktk kazi watu wako busy kila kona!
JPM anafanya kazi moja tu, kupambana na ufisadi!
Muda unaenda na unaanza kuona watu wanavyokuwa desperate, maisha yanaanza kuwa tight kwa kuwa serikali mpya kila mtu anahofia kubuni mbinu mpya, watu hawathubutu kujaribu chochote na unakuta hata maeneo ya huduma za jamii, muda mwingi ni kujaribu kutafutiana makosa kuliko kuibua ushawishi wa mbinu mbadala za kuboresha utendaji!
Gharama za bidhaa masokoni hazijashuka, huduma za jamii hazipatikani kwa uraisi na yet mapato ya mtanzania ngazi zote yameenda chini!
Nitatoa mifano nieleweke!
Afya: watu waliaminishwa huduma zitaboreshwa na kila mtanzania atapata access ya huduma bora kwa gharama nafuu! Hadi sasa sio kama zimeboreshwa lkn hata mwanga wa nini kitafanyika kufikia hatua hizo hamna! Hakuna hata mikakati ya awali ya universal health insurance, hakuna kusubsidize gharama za wagonjwa wa misamaha, hivyo kuleta mizigo zaidi kwa hospitali na wananchi! Matokeo ni kuongezeka kwa migogoro kati ya muajiri (serikali), mteja (mgonjwa) na watendaji (Dr,nurses, wafamasia)
Elimu: hakuna mbinu mbadala, kinachoonekana ni harakati za kubomoa shule zilizobora ili tukose wote! Serikali imeshimdwa hata kufufua kwa aawamu shule zake, hata zile walizosomea ndugu zetu waosemaga special schools, huku wakielekea kwa shule za kata! Shule za umma zinaporomoka kutokana na vitu vingi ikiwemo kutopatikana kwa vitendea kazi, mazingira hovyo ya kieleimu, mlundikano wa wanafunzi huku walimu, vyumba vya madarasa vikiwa hakikidhi haja, ukosefu wa maabara, library na vitabu vya kufundishia na miongozo inayobadilikabadilika!
Labda tungenza kutengeneza education zones katika kanda vunavyoweza kutoa miongozo ya utendaji! Bei elekezi za ada ni uchochezi mbaya na unaweza kufanya elimu kuporomoka ghafla kama hatutojipanga! Serikali haitoweza kuabsorb collapse ya Taasisi binafsi ikiwa wataamua shule zao wafugie nguruwe kuliko kushusha aada haadi "laki 1" kwa mwaka!
Gharama za bidhaa: Bado hazibalika hata kidogo, suala la mfumuko wa bei bado upo palepale!
Ajira: zinazidi kupungua na hakuna dalili yeyote kuwa kuna eneo jipya linaloweza kumeza vijana zaidi ya mil 2 wasio na ajira mitaani, huku wengi kati ya wale wenye ajira zisizo rasmi wakizidi kupoteza kazi kwa kuweka na kusimamia sheria Kali zilizopo (sio tatizo though) ingawa ajira kama hazijatengenezwa hizi zinazozuka often huwa zinaanza holela na control in terms of kuzingatia sheria na taratibu huwa very much compromised!
Ushirikiano wa kimataifa: tunazidi kupoteza links na nchi na agencies "rafiki" hata wale waliokuwa wanapiga pesa! Wabaya tuachane nao, lkn waliowema tuambatane nao! Kuchagua upande wa China pekee si jambo jema, tunapaswa kubalance, hata Nyerere hakuwa akifungamana na upande wowote, ingawa alikuwa mjamaa! Tricky ni kuwa ukiwa na rafiki mmoja uñakuwa very limited ktk kuout source technologies, mitaji, mikopo, !masoko etc! Tuliangalie hili nalo pia!
Kuna maeneo mengi yanapaswa kutazamwa!
Lengo sio kupoint fingers kwa kulaumu awamu hii, Bali kukumbushana wigo mpana wa uongozi wa nchi, lazima kubalance!
Baba hutosifika kwa kusimamia nidhamu tu nyumbani kwako! Peleka watoto shule, simamia afya zao, wape nafasi watoto wacheze etc!
 
Back
Top Bottom